Habari zenu wana JF, let me go straight to the point.
Huyu baba ni mtu mzima ambae sikatai alikuwa ananisaidia usafiri kipindi nikiwa naelekea chuo ambako nae ofisi zake zipo huko, ukiwa ndani ya gari yake anapenda sana kugusia kuhusu masomo, maisha, na kujichunga ukiwa kama kijana kuhusiana na mahusiano.
Sasa cha kushangaza hapendi kuniona hata nikiwa nasalimiana na vijana wenzangu ambao tumekuwa nao tangu utotoni.
I mean tuliochezea nao vifuu na kidali poo since we were young.
Tukikutana njiani bahati mbaya au nzuri nikiwa peke yangu au nikiwa na wa jinsia yangu anasimamisha gari ananisalimia kwa bashasha hata kwa dakika 30.
Ila kama kawaida akiniona na jinsia tofauti atanipita kama hanijui na atanikasirikia hata siku nyingine akiniona niko peke yangu.
Ila baada ya muda anakuwa tu kama kawaida.
Mimi naamua tu kumchunia vipi uamuzi huu uko sahihi au ntakuwa nakosea wana JF?
Nisaidieni nawasilisha.