Simuelewi aliyekuwa shemela wenu...

Simuelewi aliyekuwa shemela wenu...

The Donchop

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
294
Reaction score
381
Habarini wadau wa humu?

Nina kama wiki tatu toka tumeachana na boyfriend wangu. Tuliachana kwa mesej zenye maneno makali sana. Yeye akinitolea laana nami nikimkashifu.

Tumekuwa watu wa kugombana kila mara hata baada ya kuachana.
Mwenzangu siku zote alikuwa akipata shida yoyote ndogo basi alikuja kwangu kuniambia na hapo moyo wake uliridhia. Hata kama siwezi kusaidia lolote ye akiniambia tu anaridhika.
Baada ya maugomvi yale muda mrefu sana hatukukaa kuongea lolote. Ilikuwa ni msg ya kejeli inarudi msg ya dharau.

Shemela wenu kunirusha roho akaniambia ye amepata mtu na ana ujauzito wake hivyo nimsahau kabisa katika maisha yangu. Akaapa kwa miungu yote haitotokea akarudi kwangu hata iweje. Wala hana future nami.

Kilichonishangaza baada ya ukimya wa siku kadhaa, jana amenitafuta kwa adabu zote. Ana shida ambayo ni mimi tu ninayeweza kumsaidia.

Nina uhakika hana mpenzi lakini nimemjibu hiyo shida hata mkewe anaweza kumsaidia.
Sijui kama nipo sahihi ndugu zangu. Ni mtu ambaye nilimsaidia kwa mengi sana kipindi ambacho hakuwa na msaada lakini baada ya kupata kazi tu akautumia msaada niliompa kama fimbo ya kunisengenya na kunichapa mwenyewe.

Nimejuta kumsaidia na ingawa namuonea imani bado nina mashaka kuwa baadae atarudi kunitukana kwa msaada nitakaompatia muda huu.

Siku zote mthamini mtu kwa kile kidogo alichokusaidia hata kama leo una kikubwa zaidi ya kile ndugu zangu.
 
Pole sana mkuu ,ila matusi na dharau si tabia njema hasa kwa ninyi ambao mmeshaonana na kuunganisha vikojoleo vyenu bila shaka mnapendana tena sana tu, tulizeni akili mulirudishe tena baiyoyo lenu
 
Matatizo mengine ni ya kujitakia. Wewe huna msimamo yaani ni sitaki nataka. Jamaa atakuchezea akili mpaka uchoke na kufilisika kifikra. Kama mmeachana block kila kona move on. Haina haja ya kutafuta ushauri mtandaoni kwa jambo dogo kama hilo
 
Masikini
Bado mnapendana akirudi mkubalie tu, ila mwambie km anakupenda akuoe
 
Ilibidi kwanza niende kuangalia profile yako, umri wako na muda ulijiunga humu JF.
Nimeshangaa sana kwa mtu wa umri kama wako kuwa na akili za kitoto kiasi hiki.

Inavo onekana hapa huyo jamaa ni wa miaka kati ya 20 hivi so wewe ni kama mlezi wake ndo mana mnafanyiana hayo na wewe nae unashindwa kuutumia utu uzima wako 36yrs bado unakuwa kama kasichana acha ujinga kadada na kama bado unampenda basi acha kelele nenda kamchukue tu dogodogo wako uendelee kumlea ni utoto tu akikua ataacha.
 
mnapendana nyie tena sana .. na hayo makejeli ni sababu moyo wenu hautaki muachane lakini akili mnailazimisha .. mnaweza badilika ila we binti mrembo hata ukipata mwingine usiwe na mdomo wa kujibu maneno mabaya bwana urembo wa mwanamke wa kwanza ni nywele (nitoboeni macho) cha pili kauli na utiii cha tatu kusali, cha nne mipango na bajeti namna ya kuzitumia vizuri ongezea na kudeka haloo ukiweza hivyo mwanaume lazima abdadilike ..
 
Bado uko kwenye penzi zito, tulia sikiliza moyo wako alafu fanya maamuzi.
 
Anakupenda sn ua inatokea watu wanatukanana hata mi ua inanitokea kuachana na mtu mliezoena kwa muda ni kazi sana unajitahidi kusahau lkn hata wiki haifiki lazma mmoja awe mpole
 
Mimi nkiachana na mtu nakata mawasiliano hayo mambo ya kuanza kuambiana vitu yanatoka wapi na tumeachana
 
Bado mnapendana nyinyi hapa hakuna cha kukushauri
 
taarifa ya upande wapili pls...
Tukishabalansisha ndo tutatoa maamuzi. Asante!
 
Punguza nyodo.acha kumsimanga mwenzio. unapopendwa pendeka bibiee!!!!
 
Habarini wadau wa humu?
Nina kama wiki tatu toka tumeachana na boyfriend wangu. Tuliachana kwa mesej zenye maneno makali sana. Yeye akinitolea laana nami nikimkashifu.
Tumekuwa watu wa kugombana kila mara hata baada ya kuachana.
Mwenzangu siku zote alikuwa akipata shida yoyote ndogo basi alikuja kwangu kuniambia na hapo moyo wake uliridhia. Hata kama siwezi kusaidia lolote ye akiniambia tu anaridhika.
Baada ya maugomvi yale muda mrefu sana hatukukaa kuongea lolote. Ilikuwa ni msg ya kejeli inarudi msg ya dharau.
Shemela wenu kunirusha roho akaniambia ye amepata mtu na ana ujauzito wake hivyo nimsahau kabisa katika maisha yangu. Akaapa kwa miungu yote haitotokea akarudi kwangu hata iweje. Wala hana future nami.
Kilichonishangaza baada ya ukimya wa siku kadhaa, jana amenitafuta kwa adabu zote. Ana shida ambayo ni mimi tu ninayeweza kumsaidia.
Nina uhakika hana mpenzi lakini nimemjibu hiyo shida hata mkewe anaweza kumsaidia.
Sijui kama nipo sahihi ndugu zangu. Ni mtu ambaye nilimsaidia kwa mengi sana kipindi ambacho hakuwa na msaada lakini baada ya kupata kazi tu akautumia msaada niliompa kama fimbo ya kunisengenya na kunichapa mwenyewe.
Nimejuta kumsaidia na ingawa namuonea imani bado nina mashaka kuwa baadae atarudi kunitukana kwa msaada nitakaompatia muda huu.
Siku zote mthamini mtu kwa kile kidogo alichokusaidia hata kama leo una kikubwa zaidi ya kile ndugu zangu.
uyakua domo
 
Utoto bhana.
Nyie bado upendo upo kati yenu. Kutoleana maneno ni sawa na "sizitaki mbichi hizi". Ingawa kunaweza kuwa na tatizo linalowapelekea nyote wawili kupata hasira na msongo wa mawazo.
Ni vema mkapeana muda mpaka pale kila mmoja atakapokubaliana na moyo wake kuwa amekosea kisha myamalize.
Kuachana kwenu ipo siku mtarudiana na kuachana tena endapo hamtaziba ufa.
 
Huyo shemela wetu ni mtu wa hovyo hovyo.. Mchinjie baharini ukamatie mtu anayejielewa.. Trust me, people never change...
 
mnapendana nyie tena sana .. na hayo makejeli ni sababu moyo wenu hautaki muachane lakini akili mnailazimisha .. mnaweza badilika ila we binti mrembo hata ukipata mwingine usiwe na mdomo wa kujibu maneno mabaya bwana urembo wa mwanamke wa kwanza ni nywele (nitoboeni macho) cha pili kauli na utiii cha tatu kusali, cha nne mipango na bajeti namna ya kuzitumia vizuri ongezea na kudeka haloo ukiweza hivyo mwanaume lazima abdadilike ..
Totoo ume maliza kila kitu

Pata Savannah hapo

Nta clear Bill
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom