Simu za Halotel H6302

Simu za Halotel H6302

Kwa smartphone tayari mfano hii nnayotumia saiv nimei-unlock na natumia line ya voda coz hapa nilipo halotel haushiki ila kwa hizi simu za kawaida bado hakuna anaeweza ku-unlock.
Mkuu umewezaje ku unlock m natumia h8401.
 
Wana bodi,

Kwa masikitiko makubwa, nimeshitushwa na simu za halotel H6302 ambazo zinauzwa na halotel na mawakala wao nchini.

Simu hizi kwa kuwa ni brand ya halotel, nilitarajia zitakuwa original na hivyo siku tcra wakizima mitambo ya simu fake, basi watumiaji wa simu hizo watakuwa salama.

Chakushangaza sasa, nazo zimo kwenye orodha ya simu zitakazo shindwa kufanya kazi kwa ufake wake.

Nimeangalia kwa kutumia utaratibu wa kutuma imei no kwenda 15090 na haya ndo majibu yake.

"... Hong Kong Garland International Limited - T-max M1,M2 - Kama IMEI haioani na simu yako wasiliana na muuzaji. Usipoweza,ibadilishe kabla ya Juni 2016 kwani yaweza kuzimika...".

Wito kwa ndugu zangu, simu hizo hazioani na aina ya simu hivyo ni matatizo. Tuzieupuke kukwepa hasara. Iwapo ukinunulia ndugu zako vijijini kwa kuamini ni salama, utaumia.

Aksante
Hizo ni mtk cpu ambazo imei zake zina corrupt kirahisi lakini jaribu kuangalia imei za kwenye housing km zina fanana na za ndani lete mlejesho
 
Back
Top Bottom