Kulikuwa na Nokia fulani hivi, ina antena ya kupandisha na kushusha kama redio mkulima halafu inameza ile SIM CARD yote kama ilivyo pasipo kubandua ile Micro Chip.
Kabla hujaanza kuongea inabidi ukifunue kifuniko fulani hivi ambacho kilikuwa kinafunika keypad...
Enzi hizo ili ujulikane una simu basi unaiweka kwenye mfuko wa ghorofani "mfuko wa shati", bonge la simu kama kilo 2 hivi yaani ni kuchana mifuko ya shati mwanzo mwisho.