[QUOTE=jaxonwaziri;925680]Watu wengine bwana, pengine huwa wanauliza ',....eeeh, mu-hesimiwa laisi, kale ka-thuti ulikokavaa wakati bushi alipokuja ulikanunua bei gani wapi...?' Ama '....eti mu-ishimiwa laisi, mbona katika kale ka mkutano ka Weldi ikonomiki foramu kalikofanyika pale jiji la mlimani ulioneka upo-tense na uncomfortable sana kama vile upo kwenye intavyuuu ya kutafuta ka-ajira ....'
Mimi nadhani simu ni kitu kizuri na itumike vizuri, ila kama hadharani, mfano pale Diamond jubilee alijibu malalamiko ya wafanyakazi kwa kutumia takwimu zisizo sahihi (ikumbukwe hotuba ya rais anayoitoa hadharani itakuwa imefanyiwa kazi kweli kweli kuhakikisha haina mushkeli) na madudu mengine kibao, je hayo majibu ya srini kwa mtu mmoja mmoja kwa kupitia sms yatakuwa na ukweli kweli? Ama ndo ile ya danganya toto kuwa watoto wanauzwa hospitalini katika maboksi??....Mie simo, ni mtazamo tu![/QUOTE]
Hayo ni mawazo yako juu ya sms zetu kwa rais wetu!!!! katu hatujipendekezi kwa mtu ambaye wala hatujui !!!! mimi nawashauri nyie ambao hajawahi kuandikiana mgs nae hebu pata hoja mwandikie halafu utajua nini huwa kinaandikwa kwenye sms kwa rais.
Rais si mjinga angeshasema jamani mkome kuniandikia mambo ya kipuuzi ya kunialika kwenye kipaimara huko majimatitu nataka msg za namna hii tu! katu hajawaji kuzikejeli hadharani msg zetu badala yake amekuwa akisema zinanisaidia endeleeni kuandika nami naamini matatizo ni mengi hawezi kuyatatua yote kwa juma au siku moja
(kwenye pink) yanakuwa na ukweli ndio maana hatuchoki kuandika
Si kila jambo lazima lifanyike kwenye mkutano wa hadhara....huwezi kumwambia rais hadharani kuwa hebu nchunguze msaidizi wako fulani katika hili tunaona anaharibu .....
'Za kuambiwa changanya na za kwako'