Simu ya Rais haina tija | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu ya Rais haina tija

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 23, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Makala ya Uchambuzi
  na Na Saed Kubenea
  Mwanahalisi  RAIS Jakaya Kikwete anasema simu yake ya mkononi iko wazi kwa yeyote anayetaka kuwasiliana naye. Namba ambayo wengi tunaifahamu ni 0754 777775.

  Akizungumza na viongozi wa madhehebu ya dini nchini, mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Kikwete alisema amekuwa akiwasiliana na wananchi moja kwa moja kwa simu ya mkononi.

  Aliwaambia, "…simu yangu ile ipo wazi muda wote. Watu wananitumia sms (ujumbe mfupi wa simu), wananipigia, wengine wananieleza matatizo yao mbalimbali. Nazungumza nao. Nanyi nawaomba msisite kufanya hivyo."

  Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa viongozi hao uliolenga kufahamisha kilichomo katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi aliyosaini hivi karibuni.

  Rais aweza kuwa anajibu simu; na kama alivyosema wakati mwingine hujibu ujumbe aliotumiwa kwa njia ya kupiga badala ya kuandika.

  Hata hivyo, hadi sasa hakuna mwenye uhakika iwapo Kikwete anaitumia simu hiyo kupata taarifa kwa ajili ya umma au ni taarifa binafsi. Hii ni kwa kuwa simu ya rais inashikwa na rais mwenyewe.

  Ndiyo maana taarifa zinasema, kila anayetuma ujumbe kwa rais hujibiwa na rais mwenyewe.

  Baadhi ya wale ambao wamewasiliana naye na ambao nimehojiana nao, wanasema muda mzuri wa kutuma ujumbe kwa Kikwete; na ili ujibiwe, ni kuanzia saa saba usiku."

  Lakini je, rais anastahili kusumbuliwa na mambo kama vile mwaliko wa harusi, kipaimara au mzazi kushindwa kumcheza mtoto mkole? Je, haya hayampi kazi ya ziada ambayo inaminya muda wake kwa shughuli za umma?

  Chukua mfano wa mawasiliano ambayo Rais Kikwete alifanya mwaka 2007 na mbunge wa Viti Maalum (CCM), Amina Chifupa. Kwa maoni ya wengi hayakulenga kusaidia taifa. Yalikuwa yanamuongezea rais mzigo.

  Chifupa alilalamika kwa rais, akituhumu mmoja wa mawaziri wake kuingilia ndoa yake. Alidai waziri huyo alikuwa anamsakama kutokana na kile alichoita, "kutaka kiti cha Umoja wa Vijana CCM."

  Kikwete alijibu ujumbe wa Chifupa kwa kumwambia mengi. Lakini kubwa alisema, "Mungu yupo nawe."

  Amina hakutunza siri ya mawasiliano kati yake na rais. Alitumia mawasiliano hayo kushambulia wapinzani wake kisiasa.

  Taarifa zinasema Chifupa aliwapa wengi mawasiliano yake na rais. Alirudi hadi kwa mbaya wake na kumtambia kuwa tayari amemshitaki kwa rais. Baadhi ya mawasiliano ya rais na Chifupa yaliwahi kuchapishwa na gazeti hili.

  Hivi ni sahihi kwa rais kutolala usiku kucha akipokea sms wakati ana vyombo vya kufanya kazi ya kupokea taarifa?

  Vyombo hivi vimeundwa rasmi kwa kazi hiyo na watumishi wake wanalipwa na wananchi kupitia kodi wanayolipa.

  Sasa kwa nini rais hataki kutumia vyombo hivyo kumpa taarifa na badala yake anataka kupokea taarifa yeye mwenyewe?

  Ukweli ni kwamba, hata kama rais angekuwa na nia njema ya kuongea na kupata kila taarifa moja kwa moja kutoka kwa wananchi, asingekuwa na uwezo wa kuzifanyia kazi.

  Kwanza, ni nyingi mno. Pili, zinahitaji uratibu. Tatu, zinahitajika kuchujwa na nne, zinastahili kuandaliwa kwa vipaumbele. Mpangilio huu, hakika siyo kazi ya rais na ndiyo maana kuna vyombo vya kufanya kazi hiyo.

  Kama alivyofanya Chifupa na kama wanavyofanya baadhi ya wabunge na mawaziri "waliochati" na rais, nia imekuwa mbwembwe na majigambo kuwa waliongea na rais.

  Kuna wanaotajwa kutumia sms zao na rais kujimiminia sifa na kutafutia ubunge. Haya ni mafao binafsi, hata kama rais hakushiriki kuyaandaa.

  Naye, waziri mmoja aliwahi kunidokeza mbinu alizotumia kuangamiza wapinzani wake wa kisiasa. Alidai kuwa alipeleka ujumbe kwa Rais Kikwete, naye haraka akachukua hatua.

  Waziri huyo alijigamba kuwa ujumbe huo ulikuwa "mtaji" kwake na kwamba atautumia kujiimarisha na kumuangamiza kisiasa mbaya wake.

  Alisema kwa jinsi alivyomueleza Kikwete na rais alivyojibu, hategemei tena mbaya wake kurudi katika ufalme wa kisiasa.

  Katika mazingira haya, simu ya rais yaweza kutumika kuangamiza wengi. Yaweza kusambaza umbeya; kufitinisha na kuvunja hata ndoa.

  Kwa lugha ya vijana, hapa rais amejiachia mno, kama kweli amekuwa mpokea sms usiku kucha. Licha ya ujumbe wake kutumiwa vibaya, lakini naye aweza kupelekewa ujumbe ambao hakutarajia.

  Kwa mfano, rais aweza kupelekewa ujumbe wa kufitinishwa na wateule wake, wafanyabiashara wakubwa, wanaharakati, viongozi wa wafanyakazi na wengine wenye nia njema.

  Hili laweza kufanyika kwa kuwa mpeleka ujumbe, ama hakuwaelewa vizuri wahusika au ana nia mbaya nao.

  Si hivyo tu, rais aweza kuwekwa kiwewe kwa kupelekewa uzushi kuhusu usalama wa nchi, jambo ambalo siyo tu litashughulisha wengi, lakini pia ni ghali sana kuandaa ulinzi wa nyongeza; kwani rais hawezi kuamua kupuuza tu.

  Siyo Rais Kikwete pekee mwenye simu ya mkononi. Marais wengi wana simu za mkononi. Lakini si kila mtu anaweza kuwasiliana nao moja kwa moja.

  Hata ofisi kubwa kama zile za mashirika makubwa ya kimataifa, kuna simu ambazo huwezi kupata moja kwa moja mpaka uwe kwenye orodha ya wadau. Hii ni kupunguza usumbufu kwa kuweka mchujo muwafaka.

  Ukijumuisha yote haya, utaona kwamba ama kumpigia rais simu au rais kupigiwa; yote yanageuzwa kuwa mambo ya mbwembwe tu; na hili halipingiki.

  Rais anatumia simu moja – namba moja. Idadi ya watu wenye shida au maoni na wanataka kuwasiliana naye itakuwa kubwa sana. Kama kampuni yenye njia tano au hata kumi za simu inakuwa "bize" hadi kushindikana kufikika, itakuwaje namba moja ya rais?

  Kinachohitajika siyo kupiga mbiu kutaka watu wampigie simu rais; bali kuimarisha taasisi za serikali zilizoundwa rasmi kwa kazi ya kupokea, kuchambua na kuwasilisha panapohusika, madai, matakwa na maoni ya wananchi.

  Kwa mtindo wa kutaka kila mmoja aongee au achati na rais, basi taasisi ya urais itazidiwa na vitaarifa dhaifu badala ya hoja kuu za nchi na kwa maslahi ya wengi kupitia vyombo rasmi vilivyoundwa kwa kazi hiyo.

  Hatimaye, simu ya rais na hata sms na maongezi, vitakosa tija. Licha ya siku kutofikika, rais anaweza kujikuta anafanya kazi alizopokea kwenye simu kuliko kwa mkondo wa wazi wa asasi za dola.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Haya - wadau mliojaribu kuwasiliana na Muungwana kupitia simu hiyo twawaomba mtupatie yaliyowafika.
   
 3. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani jamani mnapenda kumsakapanya rais wetu hata kwa mambo ambayo hayagusi maslahi ya taifa kihivyo!!!! hoja ya kusema watu wanatumia msg hizo kujitafutia umaarufu au kukamdamiza wenzao nadhani si tatizo la rais ni upuuzi wa watu hao ! wameshindwa ku face realities na kukabiliana na matatizo yao basi wanatumia mawasiliano yao na mkuu kama fimbo ya kuwachapia adui zao.

  Suala la kumchosha nadhani rais ana akili timamu na anajua amechoka au lah kama zinamchosha wala halazimishwi kuzijibu au kuzisoma.....kusema ni usiku anasoma hilo pia halituhusu! yeye anajua vema anatakiwa kulala saa ngapi na kuamka saa ngapi? usidhani kila mtu hupenda kulala usiki wa manane wengine hawalali na haiwaathiri.

  Tuache kumsakama JK hata kwa mambo yasiyo na tija ya maana.....mtumieni tu msg kama yeye anavyotaka jamani.....
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Huwa anajibu msg anapopata nafasi, I have proved it personally
   
 5. kui

  kui JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  This's a joke Mr Prez.
   
 6. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Huyo rais mnamlaumu kwa kila jambo hata anapofanya mazuri?

  Kuna ubaya gani rais akiamua kuwasiliana na wananchi wake? hakuna sehemu hata moja ambapo rais amelalamika kwamba anakosa usingizi kwasababu anajibu sms.

  Tuwalaumu hao wanaotumia vibaya sms za rais na ndio wawajibike na sio rais mwenyewe.
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa hapa hata mimi nimekuwa upande wa Rais...Ni kweli tumuache rais awasiliane na wananchi maana sijawahi kusikia hata siku moja rais akisema ameshidwa kulala kwa sababu wananchi wengi wanamtumia sms au kumpigia...Hivyo nazani Hapa hakuna hoja!
   
 8. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wangu kwa hili tumuunge mkono rais
   
 9. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,752
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Nadhani pale anapojibu,kwake ndo muda muafaka.
   
 10. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Anayeweza kusema kuwa simu haina tija ni rais mwenyewe. Hakuna nayefahamu amepata simu na sms ngapi na amezishughulikia vipi. Hakuna anayejua sms au simu alizopigiwa zime-influence maamuzi mangapi aliyofanya kama rais.

  Tusiwe mabingwa wa kuandika makala za kulaumu tu!
   
 11. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zak,
  Sidhani kama Mwandishi wa taarifa hii amekosa mifano, mpaka akamtumia mtu ambae ni Marehemu ( hatuko nae Duniani).
  Hoja ni nzuri lakini aliyemtumia ni Mtu asiyeweza kujitetea au kuchangia hoja hii kwa hiyo kuanika habari zake hapa hakumsaidii yeyote mbali ya kuwaumiza Ndugu wa familia yake watakaoiona taarifa hii. WAANDISHI MUWE MAKINI!
   
 12. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi nawasiliana na rais mara nyingi kwa kutumia namba hiyo na wala hachoki kujibu yale utakayomweleza au kumwuliza.Rais wetu ni mtu wa watu na kweli amejitahidi kuwa karibu na watu japo wengine wanamchukia lakini bado wanafanya naye mawasiliano
   
 13. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #13
  May 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Muungwana anatumia suala la simu kisisas zaid...
  Labda nyie mliowasiliana nae mtueleze mmepata mafanikio gani katika masuala yenu milioya wasilisha kwa Muungwana kwa njia ya simu..je mlimuuliza nini na aliwajibu nini?..msiseme kuwa ilikuwa ni privacy kati yenu na Rais,hilo halipo..kama unataka kuwasilana na Rais kwa issue yako private..we utakuwa Mjinga aka idiot...unamuomba Rais aje kwenye Kipaimara cha mwanao...we utakuwa idiot...atahudhuria vipa imara vingap sasa!!!!
  Kama una mcontact Rais ni either kupata ufafanuzi wa masuala flan ambayo wasaidizi wake au yeye mwenyewe ameshindwa kuyatolea ufafanuzi...
  Nyie mnaotetea huu utaratibu na ambao mmeshawahi ku mcontact tuelezen mlimwambia nini na aliwajibu nini!!!!na kwanini anashindwa kuyaongea hayo hadharani...kama hamtaweza acheni ujinga wenu wa ku mcontact Rais na kumpa mialiko ya Vipaimara/harus n.k za Watoto wenu
   
 14. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Pongezi Rais, hili si jambo dogo. Na kuanzia leo mkome wote ambao mnasema mambo yasiyo na tija!
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Umenena Bramo: Kwa nini hawamuulizi masuala ya tija ya kitaifa -- kama vile kwa nini Kagoda haipelekwi mahakamani iwapo ushahidi upo kibao kwamba nani alikupua ile mihela? CRDB walitakiwa kueleza walimpa nani hiyo mihela --SIMPO!!

  Au kwa nini Chenge hasimamishwi mahakamani kwa tuhuma za kuchukuwa mlungula wa radar na huku wapelelezi wa UK -- SFO wamesha nena, na BAE wenyewe kukubali kosa?

  Halafu mwasema eti simu yake ina tija yoyote. MIAFRIKA BWANA!!!!!!
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe Counterpunch. Masuala ya kagoda au radar -- yaani ya ufisadi -- yana tija katika mustakabali mzima wa taifa hiliu, kuliko kumualika kwenye kipaimara na mambo mengine ya binafsi! SIMU YAKE HAINA TIJA YOYOTE -- ni kampeni zake tu za kisiasa.
   
 17. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kwani Prezidaa kuwasiliana na wananchi kuna shida gani??information is power na kuna njia nyingi za kupata information.

  Big Up Prezidaa endelea kuchat na kupiga na kupokea simu za Wananchi
   
 18. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dhuuuuuuuuuuu!!
   
 19. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Watu wengine bwana, pengine huwa wanauliza ',....eeeh, mu-hesimiwa laisi, kale ka-thuti ulikokavaa wakati bushi alipokuja ulikanunua bei gani wapi...?' Ama '....eti mu-ishimiwa laisi, mbona katika kale ka mkutano ka Weldi ikonomiki foramu kalikofanyika pale jiji la mlimani ulioneka upo-tense na uncomfortable sana kama vile upo kwenye intavyuuu ya kutafuta ka-ajira ....'
  Mimi nadhani simu ni kitu kizuri na itumike vizuri, ila kama hadharani, mfano pale Diamond jubilee alijibu malalamiko ya wafanyakazi kwa kutumia takwimu zisizo sahihi (ikumbukwe hotuba ya rais anayoitoa hadharani itakuwa imefanyiwa kazi kweli kweli kuhakikisha haina mushkeli) na madudu mengine kibao, je hayo majibu ya srini kwa mtu mmoja mmoja kwa kupitia sms yatakuwa na ukweli kweli? Ama ndo ile ya danganya toto kuwa watoto wanauzwa hospitalini katika maboksi??....Mie simo, ni mtazamo tu!
   
 20. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mmmmh! Mimi simo huko. Mwambie aingie na Fesibuku ili achati globale teh!teh!teh!. Uhuni mtupu, anakimbia kuongea na waandishi wa habari anakimbilia kujibu sms, Shame on him. Gud for nothing Prezidaa!!!!! I am not supporting the style!!
   
Loading...