Simu kutoka kwa Afisa Utumishi TAMISEMI

Simu kutoka kwa Afisa Utumishi TAMISEMI

inyele

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2017
Posts
1,661
Reaction score
1,303
Habari wanajamvi! Ni matumaini yangu mko poa kabisa na mnaendelea vema na majukumu ya kila siku!

Kuna mtu wangu wa karibu yangu sana ni mtumishi wa serikali kwenye idara Fulani! Huyu ndugu kapigiwa simu muda huu na mtu ambaye anajiita yeye ni afisa utumishi TAMISEMI! Afisa huyo amemueleza ndugu yangu kuhusu taarifa zake za kiutumishi kwamba majina yake yametofautiana na pia tarehe za kuzaliwa zinatofautiana kwenye document na file lake.

Mfano: Juma Rajab Abdul badala ya juma Abdul Rajab pia kuna nakala imeandika tarehe ya kuzaliwa 27/12/19. Lakini nyingine inasoma 27/02/19.

Ndugu yangu amekiri kuhusu kutofautiana kwa majina yake matatu kwani alisema hilo alishawahi kukutana nalo wakati wa uhakiki na alilifanyia kazi hadi ofisi ya kanda alifika kula kiapo na mambo yalikaa sawa tangu 2017 na hapakuwa na shida yoyote kwenye ulipwaji wa mshahara na stahiki zake zote za kiutumishi, kuhusu utofauti wa tarehe ya kuzaliwa ndugu yangu kasema hilo ni uongo kwani hazikuwahi kutofautiana katika mafaili yake yote.

Baada ya kuelezwa yote hayo ndugu yangu alimuuliza huyo afisa namna ya kumsaidia ambako aliambiwa atume 100k ili wapitishe faili lake na asipofanya hivyo ataondolewa kwenye payroll kwani anaonekana kama mtumishi hewa na wao wanaendelea kufanya uhakiki!

Aliponieleza hivyo nilihisi kama kuna dalili za utapeli hapa, tumejadiliana na kuamua kukaa kimya na endapo atapiga simu tena atamwambia imepatikana pungufu mfano 30k, au 40k... Baada ya muda kidogo huyo afisa alipiga simu tena na kuuliza kama ametuma na ndugu yangu alimjibu kuwa imepatikana pungufu kama nilivoeleza hapo na bwana yule alikubali kupokea na kumwambia zinazobaki atamalizia taratibu.

Ndugu yangu alinipa taarifa hiyo na nikamjibu hebu asifanye haraka kutuma hata hiyo pungufu.
Inaonekana huyo afisa wa TAMISEMI alikuwa anamharakisha atume na kumpa vitisho juu ya ajira yake.
Naomba mchango wa mawazo wakuu kuhusu zoezi hili la uhakiki.

Asanteni, nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyuma vimekaza Mzee, mliambiwa kwamba" Mtalimia meno"
 
Ngoja tumuite mheshimwa Jafo, ila huyo ndugu yako nae kilaza tu, hamjui afisa utumishi wake? ok hamjui, kapigiwa simu anashindwaje kwenda ofisini confirm issue sensitive kama hiyo, mwambie atume tu kwani laki kitu gani bana
 
Ni kweli mkuu nami nilihisi ni watu tu wanaomjua vizuri tena wanaweza wakawa wa kutoka ofisi yake ya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Asitume na Wala asiwe na wasiwasi

Cha kufanya aende kwa afisa utumishi wake alipo alishughulikie suala lake Kama Kuna tatizo.

Namba ya huyo tapeli na jina lipatikane kwa ufuatiliaje zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja tumuite mheshimwa Jafo, ila huyo ndugu yako nae kilaza tu, hamjui afisa utumishi wake? ok hamjui, kapigiwa simu anashindwaje kwenda ofisini confirm issue sensitive kama hiyo, mwambie atume tu kwani laki kitu gani bana
Ha ha ha ha

Kuna watu wanakera sana

Hajui kuwa mishahara ipo kwenye system.

Atakuwa mwalimu wa kijijini huyu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja tumuite mheshimwa Jafo, ila huyo ndugu yako nae kilaza tu, hamjui afisa utumishi wake? ok hamjui, kapigiwa simu anashindwaje kwenda ofisini confirm issue sensitive kama hiyo, mwambie atume tu kwani laki kitu gani bana
Ok fine,, mkuu tunatofautiana katika kuhimili pressure kutoka nje,, jamaa alikuwa anapiga simu huku akifoka na kumpa limit ya mda wa kutuma lakini Mimi sikuona haja ya kuwa na haraka nkamshauri ndg yang aende ofisini kesho kuhakiki taarifa zake ndio tukawa tunavutana hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom