Simu kutoka kwa Afisa Utumishi TAMISEMI

Simu kutoka kwa Afisa Utumishi TAMISEMI

Ok fine,, mkuu tunatofautiana katika kuhimili pressure kutoka nje,, jamaa alikuwa anapiga simu huku akifoka na kumpa limit ya mda wa kutuma lakini Mimi sikuona haja ya kuwa na haraka nkamshauri ndg yang aende ofisini kesho kuhakiki taarifa zake ndio tukawa tunavutana hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo kama haya hayafanywi kwa kutumia simu. Aende ofisi husika atakuta taarifa za uhakika.
 
Huo utapeli mbona upo toka kitambo sana,mwambie asitume na akimpigia tena amchane makavu,nshashuhudia watu wawili wakipigiwa simu za hivyo,uzuri wakareport kwa wakuu wao wa idara na ikajulikana kuwa ni utapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu,, nmemtumishi screen shorts kadhaa juu ya reply zenu hapa jamvini naona kaanza kucheka kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kifupi huyo ni tapeli. Umenielewa? Nimesemaje? Ni tapeli na jamaa yako asipoteze muda wa kupokea simu zake au kumpigia. Sana sana amwambie tu kwamba ameshamgundua ni tapeli na kwamba haitaji msaada wowote kutoka kwake kuhusu tofauti hizo kwenye taarifa zake za kiutumishi.
 
Hakuna Afisa utumishi anaweza risk kibarua chake namna hiyo..
 
Huyo jamaa ni kilaza.
1 hajui taarifa zake kwenye jalada?
2 hamjui afisa wake?
3 office ni mbali asiende?

Kwa haya tuu inaonesha ni hewa kweli
 
Habari wanajamvi! Ni matumaini yangu mko poa kabisa na mnaendelea vema na majukumu ya kila siku!
.
.
Kuna mtu wangu wa karibu yangu sana ni mtumishi wa serikali kwenye idara Fulani!
.
Huyu ndg kapigiwa simu muda huu na mtu ambaye anajiita yeye ni afisa utumishi tamisemi! Afisa huyo amemueleza ndg yang kuhusu taarifa zake za kiutumishi kwamba majina yake yametofautiana na pia tarehe za kuzaliwa zinatofautiana kwenye document na file lake,,,
Mfano: Juma Rajab Abdul badala ya juma Abdul Rajab pia kuna nakala imeandika tarehe ya kuzaliwa 27/12/19.. Lakini nyingine inasoma 27/02/19..
Ndg yangu amekiri kuhusu kutofautiana kwa majina yake matatu kwani alisema hilo alishawahi kukutana nalo wakati wa uhakiki na alilifanyia kazi hadi ofisi ya kanda alifika kula kiapo na mambo yalikaa sawa tangu 2017 na hapakuwa na shida yoyote kwenye ulipwaji wa mshahara na stahiki zake zote za kiutumishi ,,, kuhusu utofauti wa tarehe ya kuzaliwa ndugu yangu kasema hilo ni uongo kwani hazikuwahi kutofautiana katika mafaili yake yote..
Baada ya kuelezwa yote hayo ndg yang alimuuliza huyo afisa namna ya kumsaidia ambako aliambiwa atume 100k ili wapitishe faili lake na asipofanya hivyo ataondolewa kwenye payroll kwani anaonekana kama mtumishi hewa na wao wanaendelea kufanya uhakiki!
Aliponieleza hivyo nilihisi kama kuna dalili za utapeli hapa,, tumejadiliana na kuamua kukaa kimya na endapo atapiga simu tena atamwambia imepatikana pungufu mfano 30k, au 40k... Baada ya muda kidogo huyo afisa alipiga simu tena na kuuliza kama ametuma na ndg yang alimjibu kuwa imepatikana pungufu kama nilivoeleza hapo na bwana yule alikubali kupokea na kumwambia zinazobaki atamalizia taratibu.. Ndugu yangu alinipa taarifa hiyo na nkamjibu hebu asifanye haraka kutuma hata hiyo pungufu...
Inaonekana huyo afisa wa tamisemi alikuwa anamharakisha atume na kumpa vitisho juu ya ajira yake..
Naomba mchango wa mawazo wakuu kuhusu zoezi hili LA uhakiki.
Asanteni, nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpe pole sana

Mwambie afuatilie ofisini kwa maelezo rasmi
 
Anataka kupiga pesa kijanja huyo.......ni marafiki zake wanaojua hiyo issue wanatengeneza mchongo tu
 
Huyo jamaa ni kilaza.
1 hajui taarifa zake kwenye jalada?
2 hamjui afisa wake?
3 office ni mbali asiende?

Kwa haya tuu inaonesha ni hewa kweli
Tatizo lenu hamuelewi. Uko Manyara au Tarime ni mwalimu unafundisha huko au ni Mganga je unawezaje kuwajua maafisa walioko Wizarani Dodoma? Si mpaka upate shida ya kukufanya usafiri kuja Dodoma? Na siku hizi masuala mengi wanashughuliia maafisa utumishi wa halmashauri unakofanya kazi na sio lazima uende wewe TAMISEMI. sasa hapo unawajuaje maafisa utumishi walio Wizarani?
Cha kufanya unapopigwa simu na hao matapeli waambie unaenda kushughulikia suala hilo kwa afisa utumishi wa halmashauri. Ukisema hivyo wanakutukana wanasepa.
 
Back
Top Bottom