Kama ni hivyo... basi shida itakua kwenye touchscreen aidha imechoka sana (imepasuka) ama touch imekaa vibaya, kama uliipeleka kwa fundi itabidi uanze nae huyo.
Kuhusu kutuma sms za matusi inaonekana wewe mwenyewe unapendelea sana kuchat jumbe zenye matusi ndani yake aidha unatumiaga kama kibwagizo ukiwa unachat na masella, au kimewahi kuumana uko ukamuwasha mtu na matusi.
Kwa kawaida hizi simu janja huwa zinatunza kumbukumbu ya maneno ambayo huwa tunayatumia mara kwa mara.
Sasa kwa maelezo hayo haiwezi kuwa sababu moja kwa moja hivyo inachangiwa sana na sababu hii, hiyo simu inaonekana ime-settiwa out select text katika keyboard hasa kwenye uwanja wa messages.
Kulitatua tatizo kwa mda mfupi hapo hapo ulipo nenda setting (SMS setting) badilisha io out select text iwe off hapa tatizo litakua limeisha.
Baadae ndio utashughulika na touchscreen, kama touch haina shiida yeyote basi hakikisha kabla hujaiweka simu mfukoni uwe umeilock(weka password/pini ili hata ikijibonyeza power button isifunguke mpaka kwenye faili lolote).