Simu Ipi Bora Kati ya Tecno, Huawei na Simu ya iTel

Simu Ipi Bora Kati ya Tecno, Huawei na Simu ya iTel

Simu Ipi Bora Kati ya Simu za Tecno, Huawei na Simu za iTel..?

  • Tecno

    Votes: 8 25.0%
  • Huawei

    Votes: 22 68.8%
  • iTel

    Votes: 2 6.3%

  • Total voters
    32
takataka zote apo ni pasua kichwa...siku zote rahisi aghali...
 
Kubabake ndo kwanza nimetoka nunua itel s31 nimeona ni bonge moja la simu ila kwa maneno haya nayosoma humu hamjanishawishi kukata tamaa kirahisi
 
Nakushauri achana nazo zote hizo...

Chukua ya mezani...

Yenye receiver unayoweza kuzunguka nayo popote...


Cc: mahondaw
 
Huawei ni bora kulilko tecno,na itel.
Huawei hazipati moto,hardware zake ni ngumu kuliko ma tecno,huawei hata memory yake ikiwa imejaa touch yake haigandi gandi kama Simu za tecno
 
Tecno iko vzr... Sio pasua kichwa though simu bora inategemea na bajeti yako.
 
Habari wana JF, Najua hili ni swali la watu wengi sana, lakini ningependa, kujua ni simu gani bora kwako kati ya simu za Tecno, Huawei au simu za iTel. Ningependa kujua kwa kuchagua hapo juu, pia tukipata sababu ni kwanini pia itakuwa vizuri na itawasaidia watu wengine leo hata au hata hapo baadae.
Swali lako liko General sana hutapata majibu sahihi...
 
Kubabake ndo kwanza nimetoka nunua itel s31 nimeona ni bonge moja la simu ila kwa maneno haya nayosoma humu hamjanishawishi kukata tamaa kirahisi
hiyo simu inafanya kazi vizuri ikiwa mpya kaa nayo miezi sita itaanza ku stach
 
Nimetumia zote 3
Tecno baada ya muda flani huanza pungua quality ya picha zake!.
Huawei baada ya muda betri lake ni majanga.
iTel haina sifa ya simu.
Bora kuenda na Huawei kuliko zote hapo!.
Huawei ip?,mimi natumia mate 8 mwaka wa pili sasa ktu kama kipya
 
Back
Top Bottom