Jana mida ya saa kumi na moja nilikuwa mitaa ya Posta. Sasa wakati wa kutaka kuondoka kwenda nyumbani, usafiri wa daladala ulikuwa mgumu sana. Bahati nzuri au mbaya jamaa mmoja alikuwa na Landcruiser akawa anataka abiria, nadhani alitaka hela ya kuongezea mafuta, maana alitudai 2000/= kila mmoja.
Basi nikawa nimejitupia ndani ya gari. Nilikuwa mie, watu wengine, na wadada fulani wawili wana masura, maumbo, masauti, mattako na manyonyo mwee! Duh, niliwaangalia kwa kificho mara kadhaa bila macho kushiba. Nilikaza sana moyo, ila nikajisemea iwapo nitasafiri nao umbali wa kama meta kama 500 hivi kabla hawajashuka ningefanya lolote ili nipate namba zao za simu au namba za mmoja wao (nilianza kupanga kuwaambia nafanya biashara ya cosmetics, nguo, viatu, mikufu, mikoba, etc., high classics, tunauza kwa bei nzuri sana, mteja anapelekewa hadi kwake au alipo, ananunua akipenda kama hataki anaacha -
Smile, pia anakopeshwa kama ni mwaminifu, na bidhaa zote zinatoka aidha UK, Italy, USA, Germany au Central Europe, Thailand, Singapore, Spain - yaani kimsingi kichwa kilikuwa kinachanga kubuni drama kibao). Nilishajilipua, liwalo na liwe -@pinda!
Mie na hao wadada wawili tukawa tumekaa siti za nyuma (nikasema ilimradi nipo nao karibu, Mungu nipe ujasiri). Lahaulaah! Wadada wakawa wanacheza na simu zao (mmoja ana iphone mwingine Sumsung Galaxy). Muda si muda, kuangalia hivi nikakuta wote wapo JF, tena jukwaa la MMU, wanacomment, wanacheka, wanatoa likes na kugonga mikono (Halafu wanaitana shosti).
"@mwekundu anajifanya kauzu, nahisi alikuwa mtu fulani amebadilisha ID, halafu siku hizi
mzabzab haonekani, sijui kabadili ID!,
lara 1 leo hana thread nini! - Mwenzake akadakia, asianzishe thread augue! Mwingine: Jamani
Heaven on Earth nahisi kama tunakaa sehemu moja! Labda useme
gfsonwini, @HoE si rahisi kumjua - hatabiriki kama
Kongosho!. MmmmmHhhh
Mshinga na umbeya wake utadhani mwanamke!, mwenzake, usikute ni mwanamke kweli! Ehh makubwa, ati wanawake wenye ....! Shosti unasoma thread au upo kwenye PM? Kuna mtu huku nahisi ananichezea akili. Mwenzake, Sijui nani huyu naye kaanza hadithi kama za
Mtambuzi na
MziziMkavu!
The Boss siku hizi naona yupo majukwaa yote!!".
Yaani kulikuwa na mazungumzo yaliyojaa umbeya lukuki kama ujuavyo wanawake. Huo muda wote akili yangu imeshatengeneza drama kadha wa kadha ambazo zingeniwezesha kupata namba zao.
Mie nilishatoa simu yangu mfukoni, lengo ilikuwa niingie JF (maana mara nyingi nakuwa Jf hasa nikiwa nasafiri). Nilivyoona wao wapo busy kureply threads na kutoa likes na vituko vya MMU ikabidi nitulie (nilikaa katika hali ya kuzubaa zubaa sana, yaani nilikaa kingoroko kweli lengo wasinihofu wala kunishtukia kabisa!).
Yule aliyekuwa karibu na mimi nikafanikiwa kuona ID yake ya JF. Duh ndio huyo wa kuandika comments kama ambavyo huwa nazisoma MMU au kaiba ID na password ya mtu!
Hadi kufikia hapo wazo la kupata namba zao za simu likaisha, maana ID ya JF yatosha. Lakini nikasema haiwezekani, wa pili lazima vilevile niijue ID yake! Ndio niliponyanyuka kujifanya natoa hela mfukoni (of course nilitoa hela ya nauli) huku nikiwa nimerusha macho kwake! Kuiona ID, kichwa kikawa kama kimenyofolewa ghafla, nikamwambia dereva simamisha gari nimefika, kumbe nilikuwa bado sijafika!
Jamaa alisimama, halafu kucheki kumbe bado nipo mbali sijafika ninakoenda. Nikamwambia samahani mkuu (walishtuka, mie kusema mkuu - wakaniangalia wote paa), kumbe bado sijafika! Dereva akaniambia "ulikuwa umelala nini", mie nikamjibu majanga tu mkuu! Wakaniangalia tena na kutazamana.
Nimewaza sana juu ya vitu wanavyoandika watu hasa MMU na wenyewe walivyo. Yaani Nisingethubutu kuimagine urembo na uumbikaji wa hao akina dada na michango yao humu MMU! Nimefurahi sana kuwaona hao wadada live bila chenga, adha ya usafiri iligeuka kuwa suna-allahu akbar! Hata kama mie wakati mwingine nakomenti vibaya, lakini wao wamenifunika, kwa hiyo siogopi ng'o kuwatafuta!
Pamoja na kwamba nimejilipua, lakini najua hao madada hata wakisoma hawawezi kuvuta picha na kunifahamu kiuhalisia maana mie walikuwa wananiona tu kama gogo. Kweli nimeamini mtembea bure si sawa na mkaa bure huenda akaokota.