MMU ni ya Magwiji, Mie Nimenyosha Mikono Juu!

JF2050

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
2,085
40
Nilikuja huku MMU msimu ule ambapo JF ilianza kuhit katika billboard na kupata tuzo za grammy kwa mods kupiga watu ban na kufuta threads za watu hasa jukwaa la siasa na Jamii Intel kipindi kile cha mhemko wa mapinduzi, nyakati za wizi mkubwa na projects kama za Richmond, EPA, Chenge, Karamagi, mvua za kutengeneza, Mkurabita, kilimo kwanza, Babu wa Loliondo, Nabii tito, Nabii Flora etc.,

Sasa wakati huo ilikuwa ukiweka bandiko hasa kama lina misumari lazima linyofolewe, mpaka nilianza kujiuliza hao jamaa wameiteka au kuinunua JF au nini!

Kutokana na hizo adha nikawa nimetua MMU kama mtu aliyekuja mjini kwa mbio za mwenge. Sijui ndio nilikutana na uzi wa AshaDii!

Enzi hizo hakuna mtu anamjua lara 1 (nadhani naye alikuja kwa pepo za monsoon kutoka majukwaa mengine.), The Boss anapewa heshima na kila mtu, pia nilikuwa naamini Kongosho ni mwanamke. Baadaye nilikutana na uzi wa gfsonwin, niliusoma nikaona kama una mantiki. Nilikuwa nasoma nyuzi za watu kama vile nasoma thesis ya mtu mwenye mawazo mapya kabisa.

Nyuzi hizo na zingine zilinipa imani kwamba huenda MMU ni mahali pazuri. Ukizingatia kulikuwa na sexy na romantic threads zilizokuwa zinaibuka kama uyoga, hasa Loveconnect! Basi nikasema hapa si ndio penyewe, mwaka hauishi nitaondoka na mchuchu kutoka huku na kuweka ndani kabisa, mbona wangeisoma namba!

Siku zilienda zikarudi, ndio kidogo kidogo nikaanza kustuka, MMMMMhhhhhh, nyuzi za MMU ni matango pori. Nilijipa moyo nikiamini huenda hizo siku nilikutana na nyuzi za wehu, wote wametoka baa kunywa konyagi.

Kuna siku nilipata hasira, nikawa najiuliza mods wamenipiga ban, lakini kuna watu wanaandika magarasha humu kila kukicha mbona wameachwa tu! Ndio nilipofunguka macho na kugundua, MMU hata kama ingefanyiwa tambiko, tayari ilikuwa haisafishiki!

Kwa mbali wadada walikuwa wanaonekana decent kwa avatar na michango yao. Ni kama walinimotivate kuwasiliana nao, dah, sijawahi kusogea hata hatua moja.

PM mdada, salimiana, fahamiana, mjulie hali kila asubuhi, mtakie jioni njema, mpe maneno mazuri, mkaribishe lunch! Ikija swala la kupanga kukutana, duh, nikutane na nani!

Kuna wadada washawahi kuniweka busy utadhani mie mtumwa wao - nyoooooooo zao! Yaani nakumbuka nilishawahi kulala njaa hivi hivi najiona baada ya kununulia hela ya msosi internet bundle kisa nachat nao - sasa PM nichelewe kuijibu tena si ndio ningejifukuzisha bahati!

Baadaye sana, ndipo nilipogundua kumbe MMU zaidi ya 99% ya watu ni full fake (huenda hata niliochat nao hawakuwa wanawake)! Nitashangaa sana kama misukule, mandondocha, mazombie na hata majini (MziziMkavu) humu MMU hamuna. Hata mizimu labda ipo.

MMU imenipa matumaini fake, yaani muda wa kutosha umesepa tangu 2010 mpaka leo, hakuna the way forward yoyote.

Yaani, wanawake kama sio wote waliomo humu, walio wengi wamepitia suluba za mapenzi, kama vile uchumba sugu, uchumba kuvunjika, kuibiwa wachumba, mahusiano kuisha vibaya, kupewa mimba wasizotarajia, kudanganywa; hata kama wengine wameolewa kuna majanga kama vile mwanaume kununua nyumba ndogo au kupata kiunyoya au kiunywele kutoka mtaani au chuo, etc., (angalia threads zao). Humu wanawake wamejizatiti kama Al-shabaab, nimpate nani?

Yaani unakuta mtu mmebadilishana PMs mwaka mzima, ikitokea siku umemwambia mkutane sehemu, majibu ni "aku, hee makubwa, mmh yamekuwa hayo tena, lol hii mpya, mmmmhh wapi!, thubutu,"

Nimeweka appointments na wadada miezi nenda rudi, ah wapi, hata wale niliowazoea kama akina King'asti, Heaven on Earth, Smile, Cynthia Chriss hawakamatiki. Preta ndio kabisa!

MMU haina maana, inaweza kukuweka pending kama kusubiria vocha ya mkopo au kufuatilia mkopo NMB! Mbona utajuta, utakaposhtuka na umri wako ndio umeyoyoma kama wa Kapuya!

MMU ina wenyewe, magwiji yaliyobobea, mie nimenyosha mikono juu.

Jamani, nilikuja MMU kwa pepo za msimu naondoka na pepo hizo hizo, maana zikinipita nitaendelea kubaki.

CC: mimi49, christine ibrahim, Sista, sister, Ablessed mdida, charminglady, Madame B, madameA madame X, tinna cute, mkunde Original, Mapi, Asnam, Evelyn Salt, Money Stunna, watu8, Himidini, Lady doctor, mwekundu, Nazjaz, Eiyer, Boflo, Mashaxizo, Mshinga, mzabzab, Bujibuji, KOKUTONA, farkhina

BCC: MMU senior bachelors

Kwa hisani ya wana MMU wote.

ufs: @Mods
 
Last edited by a moderator:
wengine kupitia apa tumepata misamiati mipya kama papuchu,kugegeda etc uko uraiani hawajui hii misamiati
 
Tangu lini mambo ya pupa yakawa na faida. Pole, humu kuna watu halisi, karata zako tu
 
Hahahahaa..
Yaani huu uzi umenchekesha mwanzo mwisho....
Samahani mkuu na pole kwa majanga yaliyokupata.
Afadhali mie sishindagi pm...mbwembwe zote nazimalizia humu humu jamvini lol.....
Wanasema "dont expect too much because that too much can hurt u much"
 
Hahahaha

Habari hii imenichekesha kwa kweli
Ulikua hujui kwamba kuna watu na viatu!
Chezea fake IDs na avatar weye! Talala hoi

Pole wee
 
Lol pole mkuu. Humu kuna watu ni "undecided gender"

hahahaha mkuu una utani na Kongosho naona.

any way bro Simplicity hizi thread za usiku wa manane hizi huwa si za kupuuza hivihivi...kuna jambo!!!

ushauri wangu; take life easy bro. hebu sema hasa shida yako nini? mimi nadhan unatakiwa kujifunza kuchukulia disappointments zako kama challenge.
wa pm akikukataa chukua mapoint huku nenda mtaani uyatumie...for sure utafanikiwa.
but i must warn u...dont get tooooooo serious kwa hili game la malavidavi...!!!

good night mkuu.
 
Last edited by a moderator:
hahahaha mkuu una utani na Kongosho naona.

any way bro Simplicity hizi thread za usiku wa manane hizi huwa si za kupuuza hivihivi...kuna jambo!!!

ushauri wangu; take life easy bro. hebu sema hasa shida yako nini? mimi nadhan unatakiwa kujifunza kuchukulia disappointments zako kama challenge.
wa pm akikukataa chukua mapoint huku nenda mtaani uyatumie...for sure utafanikiwa.
but i must warn u...dont get tooooooo serious kwa hili game la malavidavi...!!!

good night mkuu.

usihangae alikuwwa hana usingizi kwa hiyo kaamua kufanya yake na yeye..
 
Last edited by a moderator:
Kumbe MMU nayo ni kijiwe za kutafutia wachumba???

I wish I could turn the clock to 1947 na mie nijaribu bahati yangu....

Babu DC!!

tuachie vijana wewe kizee kakae na bibi tu sio kung'ang'ana na sie vijana..

shikamoo babu DC
 
Wewe umenichekesha manake nimekumbuka ile siku ya kwanza nakuona mmu na ndala zako, nikajiuliza kuna bafu humu?
Sasa ushamba umekutoka. Ndo ujue tofauti kati ya kumzoea na mtu kukusalimia tu. Mimi niko very kind, usinione nakusalimia na tabasamu ukadhani ndo ushanizoea. Nakuwa hata jina sijakujua. Muulize Paw alinifukuzia miaka 10, na ndo hata afanyeje simuwachiiii!

Nenda mwana kwenda. Rip
Nimeweka appointments na wadada miezi nenda rudi, ah wapi, hata wale niliowazoea kama akina King'asti, Heaven on Earth, Smile, Cynthia Chriss hawakamatiki. Preta ndio kabisa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom