Simple equation inayoitesa CCM na Taifa

Simple equation inayoitesa CCM na Taifa

kagoshima

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
3,333
Reaction score
6,454
Ukweli ni kwamba wananchi wanataka chama mbadala wa CCM kuongoza inchi. Ndiyo maana kila chama cha upinzani kinapoibuka huwa na nguvu sana kiushidani. Na CCM imekua ikitumia raslimali nyingi pamoja na vyombo dola kubaki madatakani na kujaribu kuua upinzani kila unapopata nguvu. Na hapo ndipo kama taifa mtego ulipo. Hili taifa haitakuja liendee kama mfumo huu wa siasa hautobadilika. Kumbuka ili taifa liendelee tinahitaji siasa safi pia.

Anzia NCCR ya Mrema, CAF ya Maalim na Lipumba na sasa CHADEMA katika nyakati tofauti Serikali zinazo ongozwa na CCM zimetumia resource kubwa kuhakikisha opposition parties zinakufa. Resources zikitumika kudhofisha chama A chama B kinapata nguvu ukihamishia resources kuua chama B chama C kinaibuka kwani ni matakwa ya wenye inchi .

As a result miaka nenda rudi sehemu kubwa ya esources za inchi zitakua zinatumika kukandamiza na kuuwa upinzani utakaokuwa unaibuka kwa namna nyingine. Kwa kuwa hivyo Tanzania haitokuja ipige hatua kubwa kimaendeleo. Suruhisho either turudi mfumo wa chama kimoja au turuhusu democrasia ya kweli. Kubaki vuguvugu hivi ni hasara kubwa kwa taifa ingawa yaweza kuwa faida kwa CCM na familia zao.
 
Boss kagoshima Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, Tunarudi kwenye Mfumo wa Chama Kimoja, Hakuna Mpinzani atakayepewa Jimbo, Yaani tunashinda 100 % kwenye Udiwani, Ubunge na Urais. Jiandae Kisaikolojia Boss.

Kwani kuna Mtu au Watu ... Wanateseka?
 
Boss kagoshima Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, Tunarudi kwenye Mfumo wa Chama Kimoja, Hakuna Mpinzani atakayepewa Jimbo, Yaani tunashinda 100 % kwenye Udiwani, Ubunge na Urais. Jiandae Kisaikolojia Boss.

Kwani kuna Mtu au Watu ... Wanateseka??? !!!
Swa hakuna mpinzani atakaye pewa jimbo,SwaliHivi ni Nani mgawaji wa hayo majimbo? Manake inaonekana kuna mgawa majimbo yupo amekaa sehemu Fulani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swa hakuna mpinzani atakaye pewa jimbo,SwaliHivi ni Nani mgawaji wa hayo majimbo? Manake inaonekana kuna mgawa majimbo yupo amekaa sehemu Fulani

Sent using Jamii Forums mobile app

Boss Elice Elly Bwashee ... Kwani wewe ni Mgeni hapa Nchini kwetu Tanzania Shehe ??? !!! Hata kipofu ukimuuliza ... atakupa majibu ... Mubashara .... Yajayo ... Yanasikitisha na Kufurahisha kwa wakati mmoja.
 
Boss kagoshima Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, Tunarudi kwenye Mfumo wa Chama Kimoja, Hakuna Mpinzani atakayepewa Jimbo, Yaani tunashinda 100 % kwenye Udiwani, Ubunge na Urais. Jiandae Kisaikolojia Boss.

Kwani kuna Mtu au Watu ... Wanateseka??? !!!
Baadhi ya Giants wa dunia kipindi cha nyuma waliamini kama wewe lakini ghafla mambo yaliwageukia na kugharimu maisha yao na wakazikwa.

Ni lazima tujifunze kuendana na wakati.
Vazi likibana shona lingine la sivyo utavaa nguo isiyo na staha pengine ukajikuta uchi.

Ujinga wa ccm ni kudhani wanayo support ya watu wengi wenye afya ya mwili na akili nyuma yao , kumbe wamejaa watu dhaifu, wanyonge na wajinga waliokata tamaa na wasio na matumaini ya kuishi, wakidhani umaskini wao umesababishwa na watu wenye afya ya mwili na akili ambao wengi wako nyuma ya fikra huru.

Siku hadi siku kundi hili la fikra huru linazidi kuongezeka mtaani logarithmically.
Wakati hao wajinga ambao ni mtaji wao wanapungua arithmetically na sasa kuna kila dalili hili kundi la wajinga ambao ni mtaji wao linataka kulingana na hawa wenye afya ya mwili na akili, hii inamaanisha mtaji wao unaisha.

Katika mazingira hayo uchaguzi huru ni kizungumkuti na ikitokea mtu akawahakikishia ulinzi wapiga kura machafuko huwa makubwa kwa mazingira hayo ambayo kimsingi huleta mabadiliko makubwa ambayo hawata yataka siku zote.

Ni vyema ccm ijiongezee mtaji wa wapiga kura kwa kukoma kuwapa watu maisha magumu na manyanyaso kwa kibri na jeuri. Kupanga na kuunda sera rafiki kwa maisha ya watu.

Kama sivyo anguko litawaramba na kuanza kung'ang'ania madaraka na hatimaye mtavuna mnachokipanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swa hakuna mpinzani atakaye pewa jimbo,SwaliHivi ni Nani mgawaji wa hayo majimbo? Manake inaonekana kuna mgawa majimbo yupo amekaa sehemu Fulani

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapinzani watakuwepo na Chama kikuu cha upinzani kitakua ni ACT.
Wabunge wa Upinzani kutoka Zanzibar upande wa Pemba hawaepukiki.
Zanzibar hasa Pemba hakuna unafiki mkubwa wa kutafuta utajiri wadhulma kama Bara na wale wa Unguja.
Kinacholeta ubaguzi wa kisiasa sio vyama Bali ni watu wabinafsi waliopo kwenye vyama vya siasa wanaowaza kupata maslahi makubwa na familia zao na msingi wa yote ni kutumia umaskini wa watu na kujenga mazingira ya kuwa endelevu.

Bara hakuna haja ya kuwa na upinzani mpaka wananchi watakapoamka na kuweka pembeni ubinafsi wao na kupigania haki na utu wa mwanadam.

Kuwategemea matajiri kama Mbowe,Lowasa,Sumaye,Dr.Mashinji n kuleta mabadiliko ni ndoto mana wanalinda maslahi na heshima zao kwanza.

Ni lazima atokee Mtu mwenye kujitoa sana kiroho,kijamii ,kiitikadi na kisiasa.
Kidoooogo Zito anaweza na angekua na chama kama Chadema bila shaka mtiti ungekua mkubwa.

Mwingine ni Lisu.
Ni watu wenye mitizamo ya mbali kisiasa.

Hata hivyo CCM itakuja kuanguka ghafla na kabla ya 2025 patakua na katiba mpya.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono mawazo yako, ila siasa anazofanya Zito sasa alikuwa hazifanyi wakati wa Kikwete, sasa ukisema akipata chama kama cdm sijui unamaanisha nini. Lisu ni sawa ila yuko nje ya nchi. Hata Zito ni sawa, ila wakati alipopaswa kufanya siasa za mtiti alikuwa anaponda wenzake kuwa hawana siasa za kistaarabu. Mimi kwangu naona bila machafuko hakuna mabadiliko.
 
Kikarara78,
Chief . you are very wrong. Think deep. To be permanent what you are planning for october has to be constitutional . Kitakachotokea October is very temporal. Ubabe , vitisho, rushwa, manunuzi ya wapizani vitatawala je hilo ndo takwa la watanzania? Nakuambia hivi kuna kundi kubwa la raia ambao hawajawahi kupigia kura CCM hawa utawaweka wapi hiyo October.

Nakuambia serikali ya CCM hawawezi hata siku moja kubadilisha sheria ili inchi irudi mfumo wa chama kimoja. Wanaogopa mabeberu. Kitakacho tokea ni kuendelea kutumia kodi za watanzania kurubuni na kukandamiza upinzani. Jinsi tunavyoendelea ndivyo resources nyingi zitaongezeka kulinda chama dola huku inchi ikiendelea kuning'inia kwenye umaskini.
 
Magufuli ni kiski cha mpingo. Mabeberu wote duniani wanafyata mkia kwa Magu

At least you know that, and still better the history of Tanzania. Tanzania created SADC, and the country is well respected with partners who respect other countries rights.
 
kagoshima,

Wacha uongo CCM hana mbadala. Hizo SACOS hazifai Tanzania, ni swala la muda tu.
 
Back
Top Bottom