Simkumbuki Wakili mnafiki kuliko Marando

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
0
Nimeshangazwa sana na shutuma za Marando juu yangu binafsi, Mwakyembe na Mzee Samweli Sitta.. Shutuma hizi zimenukuliwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari likiwemo gazeti la TanzaniaDaima..alidai kabla ya kusema kuwa wengine wana kadi zaidi ya moja ya vyama tujiangalie. Sitawajibia kina Mwakyembe na Mzee Sitta lakini nitasema kidogo ninavyomfahamu Mzee wangu sana Marando. HILI LA MIEKUMILIKI KADI YA CHAMA ZAIDI YA KIMOJA SI WIMBO MPYA NI LA SIKU NYINGI, LAKINI NI LA KIPUUZI MAANA HATA NILIPOWAAMBIA WATOE USHAHIDI HATA WA KUSHIRIKI TU VIKAO VYA CCJ NITAJIUZULU HAWAKUWEZA MPAKA LEO WAKAISHIA KIGA KELELE BARABARANI BILA USHAHIDI..KWAHIYO HILI NI LA KIPUUZI.

NI MARANDO HUYU ANAYEWATETEA WATUHUMIWA WA KESI ZA EPA, MAHAKAMANI ANAWATETEA, JUKWAANI ANADAI NI MAFISADI NI MPAKA ALIPOTAKIWA KUJIELEZA NA BABAANGU JEETU PATEL, NI KWA KIASI GANI AENDELEE KUAMINIWA KUWA WAKILI WAKE WAKATI AMESHAMUHUKUMU KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA KUWA YEYE NI FISADI, MASIKINI MARANDO KWA UNYENYEKEVU NA UANAFIKI WA HALI YA JUU KABISA AKAAANDIKA KWA MKONO WAKE KUWA, MANENO ALIYOYASEMA KUWA MIMI NAPE NIMEKULA PESA ZA EPA KUTOKA KWA JEETU YALIKUWA YAKISIASA NA KWAMBA ALISHINIKIZWA NA CHAMA CHAKE KUYASEMA..KWAMBA ETI ALIKUTA WAMESHAANDIKA ILE STORI YA KUTUNGA NA YEYE AKATAKIWA KUISOMA KAMA ILIVYO...HATA ALIPOWAKATALIA ALILAZIMISHWA KUYASEMA YALE... NAYE KWA UNAFIKI MKUBWA AKAKAA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI NA KUROPOKA KUWA ETI Nape alikula pesa za EPA!!! Mtu mzima huyu!!!

Namheshimu sana sana Marando lakini anapofanya unafiki ni bora tuseme ili asije akawa mfano mbaya kwa vijana wasiomjua nao wakafuata unafiki wake...akibisha nitakuja na scan ya mawasiliano yake na Jeetu Patel hapa.. Tunaweza kumwamini huyu?
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,989
2,000
NI MARANDO HUYU ANAYEWATETEA WATUHUMIWA WA KESI ZA EPA, MAHAKAMANI ANAWATETEA, JUKWAANI ANADAI NI MAFISADI NI MPAKA ALIPOTAKIWA KUJIELEZA NA BABAANGU JEETU PATEL, NI KWA KIASI GANI AENDELEE KUAMINIWA KUWA WAKILI WAKE WAKATI AMESHAMUHUKUMU KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA KUWA YEYE NI FISADI

Ni kweli kabisa. Huyo mtu mimi pia namuona ni mnafiki. Anawachana kwenye majukwaa ya kisiasa hao wanatuhumiwa kuwa ni mafisadi halafu wakija kununua huduma zake za kiuwakili anakubali kuchukua hela zao na kwenda kuwatetea mahakamani.

Sawa, kisheria na kitaaluma yaweza kabisa kuwa ni sawa. Lakini kwetu sisi, kwenye mahakama ya maoni ya watu, baadhi yetu tunamwona ni mnafiki wa daraja la kwanza.

Hajui achague lipi - siasa full time au uwakili full time. Anataka kula huku na huku. Linafiki likubwa hilo.
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,838
2,000
Nimeshangazwa sana na shutuma za Marando juu yangu binafsi, Mwakyembe na Mzee Samweli Sitta.. Shutuma hizi zimenukuliwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari likiwemo gazeti la TanzaniaDaima..alidai kabla ya kusema kuwa wengine wana kadi zaidi ya moja ya vyama tujiangalie. Sitawajibia kina Mwakyembe na Mzee Sitta lakini nitasema kidogo ninavyomfahamu Mzee wangu sana Marando. HILI LA MIEKUMILIKI KADI YA CHAMA ZAIDI YA KIMOJA SI WIMBO MPYA NI LA SIKU NYINGI, LAKINI NI LA KIPUUZI MAANA HATA NILIPOWAAMBIA WATOE USHAHIDI HATA WA KUSHIRIKI TU VIKAO VYA CCJ NITAJIUZULU HAWAKUWEZA MPAKA LEO WAKAISHIA KIGA KELELE BARABARANI BILA USHAHIDI..KWAHIYO HILI NI LA KIPUUZI.

NI MARANDO HUYU ANAYEWATETEA WATUHUMIWA WA KESI ZA EPA, MAHAKAMANI ANAWATETEA, JUKWAANI ANADAI NI MAFISADI NI MPAKA ALIPOTAKIWA KUJIELEZA NA BABAANGU JEETU PATEL, NI KWA KIASI GANI AENDELEE KUAMINIWA KUWA WAKILI WAKE WAKATI AMESHAMUHUKUMU KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA KUWA YEYE NI FISADI, MASIKINI MARANDO KWA UNYENYEKEVU NA UANAFIKI WA HALI YA JUU KABISA AKAAANDIKA KWA MKONO WAKE KUWA, MANENO ALIYOYASEMA KUWA MIMI NAPE NIMEKULA PESA ZA EPA KUTOKA KWA JEETU YALIKUWA YAKISIASA NA KWAMBA ALISHINIKIZWA NA CHAMA CHAKE KUYASEMA..KWAMBA ETI ALIKUTA WAMESHAANDIKA ILE STORI YA KUTUNGA NA YEYE AKATAKIWA KUISOMA KAMA ILIVYO...HATA ALIPOWAKATALIA ALILAZIMISHWA KUYASEMA YALE... NAYE KWA UNAFIKI MKUBWA AKAKAA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI NA KUROPOKA KUWA ETI Nape alikula pesa za EPA!!! Mtu mzima huyu!!!

Namheshimu sana sana Marando lakini anapofanya unafiki ni bora tuseme ili asije akawa mfano mbaya kwa vijana wasiomjua nao wakafuata unafiki wake...akibisha nitakuja na scan ya mawasiliano yake na Jeetu Patel hapa.. Tunaweza kumwamini huyu?
Nape umeshutuhumiwa nawe ukaja hapa kujitete, ebu acha alinacha, weka ukweli na wewe acha tetesi,muda wa tetesi umeisha my fellow Tanzanian boy,hizi issue zenu za kusema nitaleta kitu fulani ushahidi kisha unachekechea jiii,ukipewa za uso unaludi jukwaani kuja kuomba sympathy ya wana JF hakika inachefua tena inachefua sana.

Ebu acha story au watoto wa kitaa wanasema acha longo longo,njooo na kitu kipachike hapa kisha mwambie Msure Tuzungumze sasa,kisha watanzania sie, tunapima nani mkweli.Pamoja na kwamba mimi sina ITIKADI ya vyama lakini kuna watu mimi binafsi uwa naaminia kwenye anga fulani fulani.Hivyo mmoja wa watu hao,namuamnia sana Mzee Marando ni mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa sana kwenye Taifa kwa kuwekana sawa hasa pale baadhi ya wakubwa walipokuwa wakienda ndivyo sivyo basi nae hakuchelewa kuwapa za uso tena kavu kavu kwa kwenda mbele.Hivyo wewe unapokuja na accusation kwa Mzee huyo ambae ni Mwanasheria mzuri bila evidence naona kama unatwanga maji kwenye kinu.

Na kwangu mimi ambae uwa ninayo yangu machache, ambayo uwa naona unanifaha uwa nakusupport kama kijana wa Kitanzania mpiganaji uliye upande wa CCM, inanipa wasi wasi kama niendelee kuamini kuwa ujabadilika na kuadapt tabia mbofu mbofu za kupindisha mambo yasiyo stahili kupinishwa kama kusema kijiko kuwa koleo dogo na Sepeto ni kijiko kikubwa.Ebu hizo zama zimeisha mwaga hivyo vitu basi tutajadiliana hapa na wengine tutajifunza na kupima kauri za Wazee wetu,Je nao ni wale wale!!!
 
Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
0
DSN,
Swala la Mzee wanguMarando kuwa mtetezi wa watuhumiwa wa EPA Mahakamani na huku jukwaani akiwaita mafisadi LINAHITAJI USHAHIDI?

Chang'o

Senior Member
Dec 21, 2012
105
0
Nape unaposema unamuheshimu sana Mzee Marando then unamwita mnafiki sidhani kama kuna heshima hapo! Hilo suala la kuwa wewe ni mmoja wa waanzilishi wa CCJ bado ujalitolea ufafanuzi wa kutosha usikimbie kivuli chako kaka na hiyo scan unayosema iweke jamvini tuione huu si wakati wa bla bla!
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,989
2,000
Kuhusu unafiki wa Marando ngoja nimtetee kidogo. Marando as a politician anayo haki ya kukemea mafisadi na ufisadi. Marando as a lawyer anao wajibu wa kutetea washtakiwa mahakamani. Sioni unafiki hapo. Ni kama vile daktari aliyekula kiapo cha kutibu kila mgonjwa hata kama mgonjwa huyo alimpiga risasi dada yake.

Unafiki upo hapo Jasusi. Tena ni dhahiri kabisa. Na kisiasa it's a bad look.

Na mimi kama mpiga kura nina haki kabisa ya kutumia sababu hiyo kumuona yeye ni mnafiki na asiyestahili kura yangu. Utapingaje ufisadi kwenye majukwaa ya kisiasa halafu mahakamani ugeuke na kuwa mtetezi wa hao hao watu unaowachana kwenye majukwaa ya kisiasa? It's stupid.

Na mfano wako wa daktari na dadaye hata haulingani na unafiki wa Marando.
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,838
2,000
DSN,
Swala la Mzee wanguMarando kuwa mtetezi wa watuhumiwa wa EPA Mahakamani na huku jukwaani akiwaita mafisadi LINAHITAJI USHAHIDI?
Ok Nape nilimaanisha kuwa tywekee hicho ulichosema ni mawasiliano yake na Mzee Jittu Patel,kisha sie wengine tunajipima kuona Mzee wetu huyo halali yake ya kukutuhumu wewe wakati anatembelea size ya kiatu asichostahiki ndipo ninapopataka na umeshasema una data hizo ndio maana nikakwambia mwaga.Kisha wengine tupime nani mkweli kati ya mtuhumiwa na mtuhumu!!!Hiko ivyo Naoe na uenda Christmas ikawa njema kwako brother.!!!Merry Christmas Nape!!
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,194
2,000
Nape Jr ndiyo mnafiki namba moja;Samwel Sitta unamuita "Mzee"lkn Dr Slaa ambaye kiumri ni mdogo kwa Samwel Sitta unamuita"kibabu"!

Then ni ww unayetakiwa uthibitishe kama sio mwanachama wa CCJ na wala sio Mabere Maucho Marando!Mbona akina Sitta wapo wazi tu na huwa wanasema kuwa"ni kweli walikuwa wanachama hai wa CCJ na walifuatwa kujiunga na chama hicho kwa sababu ya utumishi wao uliotukuka"

Sidhani kama kuna uongo kama ww hukuwahi kujiunga na CCJ otherwise unless with preponderance of evidence thibitisha kama sio kweli!
 
kagame

Senior Member
Dec 6, 2008
159
170
Kaona maswali yamemkwaza na kumzidia na wale vijana wake wa mitandaoni pale Lumumba wamelala hawamtetei Bosi wao, kwa nini asile kona Nape kilaza?
Akili nyepesi always uja na mambo mepesi yasiyo na mashiko, ni kweli angetuwekea ushahidi wa Mzee Marando kumjibu Jeetu Patel angalau leo Nape angetudhihirishia kuwa ameiva kimkakati na tusingekuwa na shaka na habari yake, Nikionacho ni kuwa ameamua kutuletea siasa kwenye hii thread! Nilicho na uhakika nacho ni kwamba ushiriki wake katika kuanzisha chama cha CCJ utabaki kuwa ukweli mpaka atakapokiri mbele ya kadamnasi.
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,971
2,000
Ni kweli kabisa. Huyo mtu mimi pia namuona ni mnafiki. Anawachana kwenye majukwaa ya kisiasa hao wanatuhumiwa kuwa ni mafisadi halafu wakija kununua huduma zake za kiuwakili anakubali kuchukua hela zao na kwenda kuwatetea mahakamani.

Sawa, kisheria na kitaaluma yaweza kabisa kuwa ni sawa. Lakini kwetu sisi, kwenye mahakama ya maoni ya watu, baadhi yetu tunamwona ni mnafiki wa daraja la kwanza.

Hajui achague lipi - siasa full time au uwakili full time. Anataka kula huku na huku. Linafiki likubwa hilo.

sasa wewe Nyani mbona unajichanganya mwenyewe? kwanza unasema marandu mnafiki pili unasema kisheria na kitaaluma yupo sawa! tushike lipi kati ya hayo mawili kama huna msimamo si ukae kimya lazima kuchangia??Nyani bwana!!
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,989
2,000
sasa wewe Nyani mbona unajichanganya mwenyewe? kwanza unasema marandu mnafiki pili unasema kisheria na kitaaluma yupo sawa! tushike lipi kati ya hayo mawili kama huna msimamo si ukae kimya lazima kuchangia??Nyani bwana!!

Kwani unafiki ni kosa kisheria? Unafiki ni kosa kimiiko ya taaluma yake? Mtu unaweza ukawa mnafiki lakini bado ukawa ndani ya sheria na miiko ya taaluma yako.

Perception often times is reality in politics. Ndiyo maana nikasema kisiasa, it's a bad look.
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,971
2,000
Mtuhumiwa ni innocent hadi hapo mahakama itakapo prove otherwise, hivo wewe ungekuwa na za kukutosha ungeacha kwanza mahakama i rule out kuwa hao watuhumiwa ni mafisadi waliotetewa na Marandu.Jambo lingine wewe ni katibu mwenezi wa chama tawala unatarajiwa uzijue na kuziheshimu sheria za nchi cha ajabu kwa kiburi unakataa kwa kuwa swala uliloanzishia mjadala lipo mahakamani na sheria zinakataza kuzungumzia nje ya mahakama swala lililo mahamani! shame on you Nape!!hii nafasi ulio nayo ni kubwa kuliko uwezo wako!!
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,971
2,000
Kwani unafiki ni kosa kisheria? Unafiki ni kosa kimiiko ya taaluma yake? Mtu unaweza ukawa mnafiki lakini bado ukawa ndani ya sheria na miiko ya taaluma yako.

Perception often times is reality in politics. Ndiyo maana nikasema kisiasa, it's a bad look.
kama hujui kuwa unafiki ni aina fulani ya maisha ya uwongo na kusingizia na ni kosa basi bwana Nyani nikuachie hapo!
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,838
2,000
sasa wewe Nyani mbona unajichanganya mwenyewe? kwanza unasema marandu mnafiki pili unasema kisheria na kitaaluma yupo sawa! tushike lipi kati ya hayo mawili kama huna msimamo si ukae kimya lazima kuchangia??Nyani bwana!!
.
Mbona Osoni hiyo iko wazi Nyani kakwambia ethically Mr Marando yuko saa but in Political moral yuko sahihi.Kila mtu anahaki ya kutafuta utetezi kwenye mahakama yoyote duniani endapo ameshitakiwa hata kama aliua.iyo ndiyo ethical ya sheria,lakini moral mtetezi wa Muuaji uenda akakabili na maadili ya utsahi wake toka kwa imani yake au dini yake.Nje ya hapo kila myu ruksa kutetewa hata kama ulikamatwa unazini na mwanao, lakini mbele ya umma [Public] ,una moral obligation lakini linapokuja ethically kisheria unastahiki utetezi kwa mujibu wa ushahid wako dhidi yw watuhumu wako.

Kwa hiyo hakuna tatizo kati ya vitu hivyo viwili,Moral & ethical kama unatambua vina maanisha nini. Morals ina kanuni na imani, wakati Ethics ina kanuni, imani na sheria.

Hivyo akiwa Kama Wakili na Mwanasiasa kitendo cha yeye kuwatetea wezi wa EPA kina picha hizi zifuatazo
1: Kisheria Mahakamani Mzee Marando hana kosa na ni haki yake anatumia Ethics kuendesha shughuri hiyo nzima.Kwa kuwa Watuhumiwa kisheria wana haki hiyo ya kutetewa.
2: Kisiasa jambo hilo hilo ni madhara kwa kuwa ni Moral.Kwa yeye kuwatetea watu ambao watuhumiwa kuibia umma
 
richone

Senior Member
Apr 3, 2012
146
195
Nappe anamtindio wa ubongo huwa anazungumza vitu asivyokuwa na uhakika navyo ndiyo maana tunasema ni manafiki. Alipanda jukwaani kuwatukana kina Lowasa na baadaye akarudi nyuma kwenda kuwaomba msamaha na kusema aliagizwa na kikwete asema hivyo. kwa maana hiyo huyu jamaa paka akifikia umri wa uzeeni ni lazima awe mchawi kwa trend inavyokwenda Nape anatusikitisha sana ni mtu wa hovyo kuliko yeyote yule awae CCM kwani huwa hafanyi utafiti huwa anaropoka ovyo
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,489
2,000
Kwa nini Nape uliongelee la unafiki wa Marando leo baada ya kukusema kuhusu kadi yako ya CCJ? je unaamini kuwa kuanika uchafu wa mbaya wako inakufanya wewe uwe msafi!??? au ndo namna ya ku divert mjadala?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom