PreGE2025 Simiyu wamuomba Rais Samia akafanye ziara huko

PreGE2025 Simiyu wamuomba Rais Samia akafanye ziara huko

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,568
Reaction score
2,486
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu kimemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara katika mkoa huo, kwani wananchi wake wana shahuku kubwa ya kumuona na kumpa shukrani kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo ndani ya mkoa huo.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Shemsha Mohamed wakati akizungumza na wananchi wa mkoa huo katika maadhimisho ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia.

Shemsha alisema kuwa Rais Samia ametembelea mikoa yote ya Kanda ya Ziwa isipokuwa Mkoa wa Simiyu, na akamuomba Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo, CPA Amos Makalla, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, kumweleza Rais Dkt. Samia kuwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu wanamuomba afanye ziara mkoani humo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom