#COVID19 Simiyu: Itilima yamaliza dozi za corona ilizopewa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,803
4,463
Itilima yamaliza dozi za corona ilizopewa.

Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, imefanikiwa kumaliza dozi zote za chanjo 3,320 za Covid -19 ambazo ilipewa na Serikali kwa ajili ya kuwachanga wananchi wa wilaya hiyo ili kujikinga na ugonjwa huo.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Faidha Salim amethibitisha hayo leo Jumatatu Oktoba 4, huku akieleza kuwa walitumia mbinu ya kutoa elimu kwa makundi hasa Waganga wa tiba asili ambao wamekuwa wakiaminika zaidi kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Nini maoni yako unafikiri mbinu hii inapaswa kuigwa na maeneo mengine?

Credit: Mtanzania
 
Kwahiyo tunajipongeza kwa hilo?

Ingekuwa raha iliyoje ingetangazwa kuwa Itilima yafuta umasikini

Madawati na madarasa ni tatizo yet you're bragging on this worthless process?
 
Back
Top Bottom