Simcard Tax

Simcard Tax

Taryx Solomon

New Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
2
Reaction score
0
Binafsi nakubaliana na Simcard Tax.... Ifike wakati tuache siasa na tuone fahari kulipa kodi kama ilivyo kwa wenzetu huko marekani mimi naamin watanzania wa kweli wote wanakubaliana na kodi hii ila wachache tu ndio wanaendeleza sumu ya kisiasa
 
Tatizo kubwa la huu mfumo wa kodi wanaotaka kuuanzisha ni kwamba hawakujipanga mapema,ni mtu kakurupuka nalo tu ili wapate mapato zaidi........kodi hii naipinga kwa nguvu zote kwa sababu ni fixed rate kwa kila mwanachi bila kujali hali yake.....kwanini hizo SIM card taxes wasiwacharge hao wanaotupa sisi huduma?...maana naamini wanatengeneza mabilioni ya fedha kila mwaka
Jambo lingine linalosababisha nipingane na hii kodi,ni kwamba kuna alternatives kibao zingine za kukusanya kodi...tena kubwa kuliko hiyo wanaotaka......kama watakuwa serious,na kama ni kweli wanajali wananchi wao.
 
Binafsi nakubaliana na Simcard Tax.... Ifike wakati tuache siasa na tuone fahari kulipa kodi kama ilivyo kwa wenzetu huko marekani mimi naamin watanzania wa kweli wote wanakubaliana na kodi hii ila wachache tu ndio wanaendeleza sumu ya kisiasa

Naona umetumwa wewe. Embu rudi ulipotoka.
 
kodi hatukatai ila kiwango cha buku1 ndicho utata. Kuna umuhimu wa kurudisha kodi ya kichwa tuachane na hizi propaganda. Yaani mwananchi ambaye kijijini kwake hakuna barabara,zahanati,sekondari,maji safi alipie elfu 1 kwa ajili ya umeme kwa wenzie? Ubinadamu utumike
 
wakuu hebu acheni siasa hili jukwaa letu ni la watu wastaarabu hebu tusaidiane kujibu maswali haya kwa faida ya wote
1. hio kodi watalipa mitandao au sisi? nimeuliza hv sababu nimeona mitandao wamepandisha bei sio kwamba wanatukaba kwenye bundle kisha watatulipia hio kodi?
2. kama tunalipa hio kodi inalipwa lipwa vp? kwa salio? je kama sjaeka vocha mwezi mzima nitafungiwa?
3. je kama nina line imepotea lakini nimeisajili na sjailipia kodi itakuwaje?

majibu yawe ni habari za kuaminika na sio rumors
 
Binafsi nakubaliana na Simcard Tax.... Ifike wakati tuache siasa na tuone fahari kulipa kodi kama ilivyo kwa wenzetu huko marekani mimi naamin watanzania wa kweli wote wanakubaliana na kodi hii ila wachache tu ndio wanaendeleza sumu ya kisiasa

Kodi ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote, hatuna budi kukubaliana na hilo tozo la sim card, kwanza hela yenyewe ndogo sana, sh. 33.3 kwa siku tu, atakayeshindwa aachane na simu si muhimu kwake, serikali isirudi nyuma kwa maendeleo ya taifa. Big up wabunge wote waliopitisha hii kodi.
 
ntamani utokee mgomo wa kugomea huduma zao.
 
Binafsi nakubaliana na Simcard Tax.... Ifike wakati tuache siasa na tuone fahari kulipa kodi kama ilivyo kwa wenzetu huko marekani mimi naamin watanzania wa kweli wote wanakubaliana na kodi hii ila wachache tu ndio wanaendeleza sumu ya kisiasa
Ni kweli unachokisema, lakini nadhani hujafanya tathmini ya kauli yako.. Umefanisha na marekani.... sawa, wenzetu kodi wanazolipa wanaona matunda yake kwenye usafiri, huduma za kijamii... etc.
 
Kodi ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote, hatuna budi kukubaliana na hilo tozo la sim card, kwanza hela yenyewe ndogo sana, sh. 33.3 kwa siku tu, atakayeshindwa aachane na simu si muhimu kwake, serikali isirudi nyuma kwa maendeleo ya taifa. Big up wabunge wote waliopitisha hii kodi.
Kuna watu milo mitatu inawashinda, we kama falsafa yako ni kuwa kama huwezi acha, basi utauwa wengi... Maana usije ukadhani huyo mtu ana kodi moja tu, hiyo ya simu... ana msululu wa kodi...
 
Kuna watu milo mitatu inawashinda, we kama falsafa yako ni kuwa kama huwezi acha, basi utauwa wengi... Maana usije ukadhani huyo mtu ana kodi moja tu, hiyo ya simu... ana msululu wa kodi...

Wewe nyamaza tu, hata kiswahili kinakushinda, si msululu, nenda shule ukajifunze umuhimu wa kodi kwa taifa.
 
tatizo hakuna faida ya hiyo kodi tunalipa kido za kuwajengea watu msata na mbezi na segerea majumba na kampeni za ccm hapo wanatengeneza hela ya kampeni mwaka 2015 wameona kuja na noti nyingine ya 3 ya thamani ile ile tutawashtukia!sasa ngoja watulie kwenye kodi hivi hamshangai kuwa na manoti mawili mawili hapa nchini?
 
Mabwenyenye waliowekeza kwenye migodi ya madini wasamehewe kutozwa kodi, halafu mwananchi, mtanzania wa hali ya chini atozwe sim-card tax! inapendeza sana.
 
Back
Top Bottom