only83
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 5,342
- 2,528
Katika hali ya kusikitisha naibu waziri George Simbachawene anaendelea na porojo zile zile za waziri wake na serikali yake kuhusu gesi ya Mtwara.
Leo kaibuka anasema kuwa wananchi wa Mtwara watapata majibu ya hoja zao kama wataruhusu bomba ya gesi lijengwe. Anasema kuwa wanaowavuruga wana Mtwara wengi ni watu wasio na mahusiano yoyote na mkoa wa Mtwara kwa maana ya kuwa si wakazi wa Mtwara.
Nadhani hizi ni dharau kwa wana Mtwara na watanzania, maafa yale yote yaliyotokea bado hii serikali dhaifu haioni aja ya kuwasikiliza wana Mtwara.
UPDATE:

Naibu wa Wizara ya Nishati na Madini, George Simbachawene, amesema serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakuwa tayari kuhukumiwa na wananchi wa Mtwara katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kama mikakati iliyopangwa na serikali katika kutekeleza mradi wa gesi itakuwa ni ya kuwadanganya.
Alisema hayo juzi wakati akizungumza katika mahojiano kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV kila Jumatatu.
Simbachawene aliseama serikali ya CCM ni makini na inatambua kuwa msingi wa utawala ni watu, hivyo haiwezi kudhalau watu wa Mtwara na Lindi hata kama ni wachache kiasi gani, kinachotakiwa wawe tayari kuelewa, lakini wakiwa hawapo tayari kuelewa wanaipa tabu sana serikali katika utekelezaji wa mradi huu.
Alisema Serikali ya CCM ilishinda uchaguzi kihalaki, haikushinda kidikiteta, kwa hiyo iachwe ifanye kazi na ihukumiwe inaposhindwa kufanya mambo iliyoahidi, wananchi wa Mtwara kama wanasema haya tunayoyaeleza tunawadanganya watusubiri 2015 watuhukumu lakini sisi tunarudia kusema watuelewe waache tutekeleze mradi huu.
"Sisi kama serikali tunao askari, tunalo Jeshi tunaweza kutekeleza kwa nguvu, lakini hatutaki kufika huko, tunaamini tutaelewana, tunaamini katika suluhu,tunaamini huu upotoshaji uliopelekwa kwa wananchi wa Mtwara utakwisha," alisema Simbachawene.
CHANZO: NIPASHE