Simbachawene: Tunataka kupunguza utitiri wa vitambulisho

Simbachawene: Tunataka kupunguza utitiri wa vitambulisho

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Serikali imeanza mpango wa kuunganisha kitambulisho cha Taifa na Huduma nyingine za kiserikali ikiwemo Bima ya Afya,Leseni ya udereva na Masuala ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kuepusha utitiri wa vitambulisho pale mwananchi anapohitaji huduma mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene akizungumza katika Kikao Kazi cha Tathmini ya Utekelezaji wa Ahadi za siku Mia Moja za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kinachofanyika mkoani Pwani chini ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, Wakuu wa Wilaya na Viongozi wengine wa juu wa ngazi ya mkoa.

 
Mradi Mpya!!!

Kama kawaida ya serikali dhaifu inavyowakandamiza wananchi wake kwa kodi zisizokuwa na mbele wala nyuma!!
Hivi vitambulisho lukuki mlivyoisha vitoa, hamkujua kuwa mgeweza kutoa kimoja kikakidhi haja ya kuwa na vitambulisho vingi? Hiyo. yote ni kwasababu ya kufanya mambo bla tafakuli ya kina !! Acheni papara tumieni akili hata za kuazima.
 
National ID ijitegemee

Driving Licence ijitegemee

Bima ijitegemee

Consolidation ni mbaya
 
Kwa sasa serikali iache drama.
Leteni maji kwanza, tunashindwa kustarehe na wake zetu kisa maji.
Shame. After sixty yrs of independence Kimara hakuna maji. Manake wanawake hawachambi, hawatawazi na hawanawi.
 
Back
Top Bottom