Simbachawene: Mpango wa gesi utatekelezwa

Simbachawene: Mpango wa gesi utatekelezwa

Kwann serikali inashidwa kufanya mambo yake kwa usahihi na badala yake inakuwa inasingizia vyama vya siasa. hivi watanzania hawachoki na ahadi bubu na mipango isiyo na tija, mpaka mtu awambie au chama kitanganze? Serikal inapaswa kuwa makin; kwan maisha magum ndo chanzo cha kudai haki nchin na wala s shirikizo kutoka upande wowote.
icon6.png
 
Gama na Kyenju hawatachelewa kuwaporomoshea matusi japo mko sawa asilimia mia.

Kwenye ukweli unausema tu mkuu, kutukanwa hatuaanza leo. Lakini ukweli ni kwamba, maandamano na ushabiki utapoa taratibu na mipango ya maendeleo itaendelea.

Naichukia CCM kweli kweli, lkn bado sioni kama ni sahihi kupinga kila kinachofanywa na serikali. Tuweke uzalendo mbele, siasa ifuate. Tujifunze kwa Wamarekani
 
Hivyo viwanda vitajengwa lini?na nikwanini walianza na kuzindua ujenzi wa bomba na kufidia watu wahame kabla hata kujenga hichiokiwanda cha kuprocess hiyo gase chafu.maana walisema itakayoletwa dar ni ile safi tu.
 
CCM mtasema yote mwaka huu ila mjue mnalo!
Msije mkaahidi na ambayo hayawezekani its just 2 years to 2015 mtakosa pa kuficha. Sura zenu
 
Kwanini asingetoa elimu hii kwa wana Mtwara/Lindi mwanzoni kabla ya maandamano na uvunjifu wa amani kupotea? Na kwanini azungumzie kwenye ITV badala ya kwenda kunako husika, wakati anajua wazi kuwa siyo wananchi wote vijijini wana ving'amuzi na umeme?

Kosa la serikali hapa ni kufanya mambo kwa mazoea. Waliwachukua viongozi wengi tu kuanzia wabunge wa Lindi na Mtwara, kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na viongozi wa Halmashauri na kuwapeleka nje kujifunza mambo kadhaa yahusianayo na gesi. Baada ya kurudi ilikuwa ni kazi kwao kuyavuvia waliyoyapata kila mmoja alikotoka.

Cha ajabu, mmoja wa wabunge hao hao ndio kiongozi wa upotoshaji. Kama ndugu yangu unaishi Mtwara, hujachelewa, wahi VETA kaulizie utaratibu wa kujiunga na hizo kozi walizoziandaa kuhusu masuala ya gesi. Unaweza ukakaa unalaumu huku CCM wanatanguliza watu wao vyuoni baadae mkabaki nyuma tena sababu ya kukesha mkilaumu badala ya kuchukua hatua.
 
Huyu jamaa ni MPUUZ kabisa, anasema eti waachwe (CCM) watekeleze ahadi walizowaahid watu Kucn, anaongea UPUUZ mtupu, ni ahadi gani hiyo waliyowatekelezea watu wa Kucn zaidi ya kuwakashifu, au kuwafanyia wasichokitaka watu wa kusin ndo huo utekelezaj?
 
Hivyo viwanda vitajengwa lini?na nikwanini walianza na kuzindua ujenzi wa bomba na kufidia watu wahame kabla hata kujenga hichiokiwanda cha kuprocess hiyo gase chafu.maana walisema itakayoletwa dar ni ile safi tu.

Unaona sasa, haya ndio maswali ambayo hayakusaidii. Gesi chafu haisafirishiki kwa hiyo jibu hapo ni kwamba LAZIMA KITAJENGWA. Sasa muda huu jambo la maana kwa Mwanamtwara ni kuwahi fursa na sio kuuliza maswali ambayo majibu yake hayana direct impact kwenye future yako.

Nenda VETA kaombe mwongozo wa course, lini zinaanza, vigezo n.k ili siku kitakapojengwa upate fursa ya kunufaika.
 
unaona sasa, haya ndio maswali ambayo hayakusaidii. Gesi chafu haisafirishiki kwa hiyo jibu hapo ni kwamba lazima kitajengwa. Sasa muda huu jambo la maana kwa mwanamtwara ni kuwahi fursa na sio kuuliza maswali ambayo majibu yake hayana direct impact kwenye future yako.

Nenda veta kaombe mwongozo wa course, lini zinaanza, vigezo n.k ili siku kitakapojengwa upate fursa ya kunufaika.
wewe acha kujifanya unaujua wema wa ccm wakati hata wewe ni muhanga.hayo majibu ya pinda kwa hizo kamati za wanamtwara hayana mashiko sababu hawakutaka kuwaeleza toka mwanzo.
Na ni kwanini kiwanda cha kuchakata huo umeme kisijengwe mtwara?tunazo sehemu nyingi ambazo watu wameambulua kuathilika tu ma madhara ya kemikali ambapo hata hiyo serikali haiwajali.nenda north mara uone wananchi walivyoteseka lakini serikali ya wezi na wahuni wakubwa ilo kimya wanaangalia 10% kwa munufaa yao binafsi.kama kweli wanania ya kuwasaidia wanamtwara,basi hiyo mikataba iwekwe wazi kwa wawakilishi wao?
 
Kusafirishwa kwa gesi kutoka Mtwara mpaka Dar siyo sababu ya kupunguza ugumu wa maisha ya mtanzania. Tuna madini lukuki, makaa ya mawe, nk., mbona maisha bora hatuyaoni?

mkuu kuna kitu unamiss,madini wanauza yakiwa ghafi coz hatuna mitaji ya kujenga viwanda vya kuprosesi,but gesi inaletwa anatumia bakhresa hapa hapa bongo,badala ya kulipa gharama kubwa za umeme ussiokuwa na uhakika akipata gesi gharama za uendeshaji zitapungua so vitu anavyozalisha kama unga vitapungua bei.machomaanisha ni kuwa gesi inatumika kwenye mambo ambayo yanatuhusu moja kwa moja kwenye maisha ya kila siku tofauti na madini,though ni kweli madini mchango wake nao unatakiwa uonekane ktk maendeleo ya nchi.
 
Huyu jamaa ni chizi, yaani utumie mabavu halafu utegemee kuwa utaendelea kubaki madarakani, hawa jamaa wamelewa madaraka.

Mkuu nilileta thread kuhusu kauli hii ya kibabe ya mh. waziri lakini baadhi ya members walinikashifu na kuniita mzushi.
 
Somo yangu huyu yeye huwa ni mabavu kwendambele. Bado anandoto za kuileta gesi kwa mabomba kuja dar? CCM bwana ni waajabu sana.
 
Ndugu zangu najua mtanitukana laki palipo na ukweli lazima niseme.. na ntasema tu.
1. Mnang'ang'ania gesi ibaki mtwara ili viwanda vijengwe je mna elimu yoyote kuhusu swala la gesi? jibu ni kwamba bado wataalam watatoka nje.

2. Mnataka gesi iwe processed mtwara(na ndicho ambacho serikali yafanya) lakini si bado lazima tu itahitaji bomba la kuipeleka dar? au mwataka mbaki nayo yote mfanyie nini gesi yote ka si uchoyo?

3. Haya sasa fujo zimeshatokea najua haijawauma lakini fikirieni hao wanafamilia waliopoteza ndugu zao wanajisikiaje au ungekua ni wewe yamekukuta ungejisikiaje? na bado haitoshi mnasikiza watu waishio nje ya mtwara ambao kazi yao ni kubonyeza vitufe vya computer ili mfanye fujo kama ni kweli wana nia nzuri si waje wajiunge na nyie?

4. Je ni Tanzania pekee ndipo gesi inatakiwa kusafirisha kwenda kwenye sehemu inapohitajika sana? si nchi nyingi tu zinafanya hivo.

Wanamtwara gesi itawafaidisha tu muiamuni serikali ni kama nyamongo wanavosema hawafaidiki wakati wanafaidika kwa haya yaguatayo.
1.mgodi.umejenga shule na zahanati.
2. kuna wanaafunzi wa primary secondary na vyuo vikuu wanasomeshwa na migodi.
4. wanakijiji wa pale wamepewa ajila kama za ulinzi na kazi za usafi ambao hata hawajaoma.
5. barabara na umeme ni wa uhakika nyamongo na bado wanajenga umeme kutoka nyamongo kwenda Tarime umeme ambao.ni wa uhakika yaani aukatiki.
6. hao hao wazungu ndo wanunuzi wakuu wa bidhaa za nyamongo na ndo maana hata ukiwa na mtaji.mdogo unafaidika.

so ndugu zangu watanzania wenzangu.
Serikali.imeshahaidi kujenga viwanda na.mitambo.ya kuzalisha.umeme kuweni na imani na ni vizuri kutumia diplomacy.kuliko fujo wakishindwa kutekeleza hayo nyie ndo mliowachagua nyie ndo.mtakao wangoa 2015 madarakani.peacefully kwa kumchagua kiongozi.anayefaa tusipoteze ndugu zetu na viuongo vyetu.fujo.nyingine zitadababisha tushindwe hata kuja kuenjoy matunda ya hiyo.gesi baadaye kumbukeni sio nchi.moja inangojea tugombane ili wafaidike.
1. wapo watakaotaka kuuza silaha
2. wapo watakaotaka kututawala
3. wapo watakao tumia mwanya huo kuchukua ziwa Nyasa.
4. na nchi inaeza isijerud kwenye aman daima kama ilivo somalia mali libya misri na kwingine duniani.

Cha maana ni kila moja kwa imani yake akasalo na kuomba Mwenyezi Mungu atupe amani na solution.kwenye swala hili na sio kusikiza watu wachache ambao wanadema andamaneni wakati wako many.miles from Mtwara
Mungu Ibariki Tanzania dumisha Amani daima.
 
simbachawene ni mbulula wa kawaida,tumezoea maneno yake ya kujipendekeza kwa polisi na jeshi wakati hata kushika kisu hawezi..hivi huyu si alifumaniwa??!!!
 
Back
Top Bottom