Simbachawene: Mpango wa gesi utatekelezwa

Simbachawene: Mpango wa gesi utatekelezwa

Kama ni lazima gesi kusafirishwa basi ipelekwe dodoma sindio makao makuu?mbona mpaka leo serikali haijahamia dom?kila kitu dar mnaona wana mt vichwa maji sio?
 
Amesema wasipotimiza maendeleo ya viwanda Mtwara,wawaadhibu 2015...nadhani hapa anaizika CCM yake!!
 
its funny,SO SO ridiculous those guys,,
na jeuri hiyo ya kuongea ongea huo upuuzi wanaipata kwa kuwa wanaongelea kwenye vyombo vya habari,ajabu wakija huku hawaongei na wanakuja kimya kimya nini wanahofia?
Huyo simbachawene si alikuja huku kimya kimya na alipofika msimbati akawekewa magog njian na kuamriwa ageuze zake na wananchi?kama alikuwa ana ubavu kwa nini asingeyasema hayo kipind alipokuja?
Hiyo haitsaidia watu kubadili misimamo yao hata kidogo,eti wasipotimiza tuwaadhibu 2015..?
Tuwaadhubu nyinyi 2015 huku nyinyi mkiwa mmeshatuadhibu sisi for the rest of our life..!
Nani akubali ujinga huo,hatutaki tena siasa na blah blah katika hilo,inshort tumeghairi moja kwa moja.
 
kwa sababu kuna soko kubwa la gesi na haiji kugawiwa bure!!!so tuambieni mnataka malori yatumike kuileta dar badala ya bomba?
Kama wangejenga maviwanda Mtwara na kuwapatia kazi wenyeji, ingepunguza tatizo la wamachinga kukimbilia mijini ma kutuchafulia miji yetu
 
Hivi mnataka gesi isafirishwe kwa malori?
Hakuna kitu kama hicho duniani, gesi inasafirishwa kwa bomba, sasa wasiotataka gesi ije dar wanataka ipelekwe wapi? Waziri anasema viwanda vyote vya kutengeneza gas vitakuwa mtwara sasa mnatakaje?
sasa kama viwanda vitakuwa mtwara,kwa nini gesi isafirishwe mpaka dar?
 
kwa sababu kuna soko kubwa la gesi na haiji kugawiwa bure!!!so tuambieni mnataka malori yatumike kuileta dar badala ya bomba?

Acha mbwembwe wewe.Eti viwanda vingi vinakataa kutumia umeme wanataka kutumia gesi!!!huu ni upuuzi ni viwanda gani na kabla ya hapo vilikuwa vinatumia nn?gesi haitoki mtwara na hadanganywi mtu hapa.Watabeba na malori mbona mafuta wanabeba na roli?
 
Katika hali ya kusikitisha naibu waziri George Simbachawene anaendelea na porojo zile zile za waziri wake na serikali yake kuhusu gesi ya Mtwara. Leo kaibuka anasema kuwa wananchi wa Mtwara watapata majibu ya hoja zao kama wataruhusu bomba ya gesi lijengwe. Anasema kuwa wanaowavuruga wana Mtwara wengi ni watu wasio na mahusiano yoyote na mkoa wa Mtwara kwa maana ya kuwa si wakazi wa Mtwara. Nadhani hizi ni dharau kwa wana Mtwara na watanzania, maafa yale yote yaliyotokea bado hii serikali dhaifu haioni aja ya kuwasikiliza wana Mtwara.

AFU WANANTWARA W0TE HAWAJAX0MA X0 HAWAWEZ PATA KAZ ATA KM KIWANDA KIKIJENGWA PALE,,ch0chea m0t0 maharagwe yakwive,,
 
Hii kauli ilinifanya nishtuke kidogo!
Sijui aina gani ya viongozi wetu...
Uhuru ulipatikana dar?
Uhuru ulipatikana Daslam au Tanganyika?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
chawenemineralsenergycompesate(3)(1).jpg

Naibu wa Wizara ya Nishati na Madini, George Simbachawene


Naibu wa Wizara ya Nishati na Madini, George Simbachawene, amesema serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakuwa tayari kuhukumiwa na wananchi wa Mtwara katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kama mikakati iliyopangwa na serikali katika kutekeleza mradi wa gesi itakuwa ni ya kuwadanganya.

Alisema hayo juzi wakati akizungumza katika mahojiano kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV kila Jumatatu.

Simbachawene aliseama serikali ya CCM ni makini na inatambua kuwa msingi wa utawala ni watu, hivyo haiwezi kudhalau watu wa Mtwara na Lindi hata kama ni wachache kiasi gani, kinachotakiwa wawe tayari kuelewa, lakini wakiwa hawapo tayari kuelewa wanaipa tabu sana serikali katika utekelezaji wa mradi huu.

Alisema Serikali ya CCM ilishinda uchaguzi kihalaki, haikushinda kidikiteta, kwa hiyo iachwe ifanye kazi na ihukumiwe inaposhindwa kufanya mambo iliyoahidi, wananchi wa Mtwara kama wanasema haya tunayoyaeleza tunawadanganya watusubiri 2015 watuhukumu lakini sisi tunarudia kusema watuelewe waache tutekeleze mradi huu.

“Sisi kama serikali tunao askari, tunalo Jeshi tunaweza kutekeleza kwa nguvu, lakini hatutaki kufika huko, tunaamini tutaelewana, tunaamini katika suluhu,tunaamini huu upotoshaji uliopelekwa kwa wananchi wa Mtwara utakwisha,” alisema Simbachawene.




CHANZO: NIPASHE

 
"Sisi kama serikali tunao askari, tunalo Jeshi tunaweza kutekeleza kwa nguvu, lakini hatutaki kufika huko, tunaamini tutaelewana, tunaamini katika suluhu,tunaamini huu upotoshaji uliopelekwa kwa wananchi wa Mtwara utakwisha," alisema Simbachawene.
Huyu jamaa ni chizi, yaani utumie mabavu halafu utegemee kuwa utaendelea kubaki madarakani, hawa jamaa wamelewa madaraka.
 
Na Mwandishi wa Thehabari.com


SERIKALI imetaja manufaa na faida ambazo wanatarajia kuzipata wananchi wa Mtwara pamoja na Lindi endapo gesi itasafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam.

Imesema Mkoa wa Mtwara ndipo utakapo jengwa mtambo mkubwa wa kusafishia gesi hiyo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa matumizi ya uzalishaji umeme na matumizi ya moja kwa moja viwandani.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipokuwa akizungumza katika Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Radio One jijini Dar es Salaam.

Naibu waziri huyo ameweka wazi kuwa mkoani Mtwara licha ya Serikali kupanga kujenga viwanda vingine kadhaa, inajenga mtambo wa megawati 250 ambao utakuwa ukizalisha umeme na mwingine kujengwa mkoani Lindi eneo la Somanga Funga utakao kuwa ukizalisha megawati 520.

Akifafanua zaidi Simbachawene alisema eneo la Mikindani katika Kijiji cha Msijute mkoani Mtwara kinatarajiwa kujengwa kiwanda kikubwa cha saruji Afrika Mashariki na Kati chenye uwezo wa kutoaji ajira kwa watu 6000 jambo ambalo ni manufaa ya Wanamtwara.

Alisema pia tayari kuna wawekezaji wa viwanda vya mbolea wamejitokeza kujenga viwanda mkoani Mtwara na Serikali itaviacha vinu vya kuchimba na kusindika gesi eneo hilo jambo ambalo bado ni manufaa makubwa kwa wananchi.

"Viwanda vya kusindika gesi hii vimepangwa kujengwa maeneo ya Lubasi, Kishere, Mchinga Bay, Lindi, Sudi Bay, Airport pamoja na Mikindani…viwanda vyote hivi vitatoa ajira kubwa sana," alisema Naibu Waziri.

Alisema licha ya manufaa hayo, gesi itakapopelekwa Dar es Salaam itazalisha umeme wa uhakika pamoja na kutumika moja kwa moja viwandani jambo ambalo litailetea taifa tija kubwa ikiwa ni pamoja kupunguza ukali wa maisha.

"Ni kweli gesi imepatikana Mtwara lakini ni lazima uipeleke sokoni ili iweze kupata soko (wateja)…Dar es Salaam ndio kwenye soko, huwezi ukaiacha Mtwara ambako hakuna soko; mbali na kuzalisha umeme kuna viwanda 37 na hoteli kadhaa zinataka ziitumie moja kwa moja ni lazima iletwe huku, Mtwara pale hakuna soko," alisema.

Aidha alitolea mfano kuwa zipo nchi mbalimbali ambazo zimegundua gesi lakini zimelazimika kuisafirisha kwa mabomba kwenda eneo la soko. Alibainisha kuwa nchi ya Urusi inasafirisha gesi yake hadi nchini Ujerumani huku Iran ikisafirisha hadi India gesi yake kutafuta soko lilipo.

Alisema miundombinu mikubwa ya umeme ipo jijini Dar es Salaam hivyo kuna kila sababu ya gesi hiyo kuletwa jijini humo ili iweze kuzalisha umeme na matumizi ya viwandani moja kwa moja pamoja na matumizi mengine, ambapo tayari wateja wamepatikana.

Aidha aliongeza kuwa uzalishaji umeme wa kutosha kwa kutumia gesi utapunguza bei ya umeme na kuuzwa kati ya senti 6 na 8 za Marekani jambo ambalo litapunguza ugumu wa maisha na pia bei ya bidhaa nchini.

Pamoja na hayo amevitaka baadhi ya vyama vya siasa na taasisi zisizo za Serikali (NGO's) zinazowapotosha Wanamtwara juu ya mradi huo kuacha kitendo hicho kwani hakuna asiyejua umuhimu wa gesi hiyo kuja Dar es Salaam.

"Hivi ni nani asiyejua kuwa tatizo la kutokua na umeme wa uhakika nchini ndilo linalokwamisha uchumi wa nchi…Tanzania inapoteza bilioni 4.5 kwa ajili ya kununua mafuta ya kuzalisha umeme kwenye mitambo yake, sasa gesi itaokoa fedha hizi," alisema Simbachawene.

Hata hivyo amesema Serikali haiwezi utekeleza mradi huo kwa nguvu bali itaendelea kuwaelimisha Wanamtwara umuhimu na manufaa ya gesi hiyo kuletwa Dar es Salaam na inaimani wataelewa na malumbano kumalizika.
 
Simbachamwene ni mwehu tu. Na lazima aropoke kwani anamkingia kifua bosi wake kwa sababu akiongea otherwise atanyimwa ugali.
 
Huyu jamaa ni chizi, yaani utumie mabavu halafu utegemee kuwa utaendelea kubaki madarakani, hawa jamaa wamelewa madaraka.
Kaa kimya acha walewe madaraka, wasipolewa tutachelewa kuwamwaga mavi
 
waeleze, huenda wataelewa. na hao wanasiasa uchwara waone aibu.
 
Gama na Kyenju hawatachelewa kuwaporomoshea matusi japo mko sawa asilimia mia.
 
Last edited by a moderator:
Gama na Kyenju hawatachelewa kuwaporomoshea matusi japo mko sawa asilimia mia.

Hata kama wakinitukana, ukweli unabaki palepale, lazima ifike wakati waelewe kile wanachoambiwa siyo kukomaa komaa tu.
 
Last edited by a moderator:
Aidha aliongeza kuwa uzalishaji umeme wa kutosha kwa kutumia gesi utapunguza bei ya umeme na kuuzwa kati ya senti 6 na 8 za Marekani jambo ambalo litapunguza ugumu wa maisha na pia bei ya bidhaa nchini.

Maneno yanayofanana na hayo si yalizungumzwa pia kipindi cha Gesi ya Songosongo? Kilichofuatia ni nnini!

Halafu mbona hawa watu hawazungumzii gesi kutumika majumbani ili kupunguza uharibifu wa mazingira? Ama wizara husika haina mawasiliano na Wizara ya Nishati ama gesi ni maalum kwa watumiaji wakubwa tu au mazingira ni kwenye fukwe tu?
 
Kusafirishwa kwa gesi kutoka Mtwara mpaka Dar siyo sababu ya kupunguza ugumu wa maisha ya mtanzania. Tuna madini lukuki, makaa ya mawe, nk., mbona maisha bora hatuyaoni?
 
Hapo kama bado hawajaelewa, basi watakuwa na sababu zao.
Kwanini asingetoa elimu hii kwa wana Mtwara/Lindi mwanzoni kabla ya maandamano na uvunjifu wa amani kupotea? Na kwanini azungumzie kwenye ITV badala ya kwenda kunako husika, wakati anajua wazi kuwa siyo wananchi wote vijijini wana ving'amuzi na umeme?
 
Back
Top Bottom