Simbachawene kalidanganya bunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simbachawene kalidanganya bunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makoye Matale, Jun 24, 2011.

 1. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Simbachawene mbunge wa Kibakwe CCM ameliambia bunge kuwa kwa sasa hakuna Mtanzania anayeshindwa kunywa chai kwa siku. Sisi kule kwetu, kulingana na hali ngumu ya uchumi chai ni 'mashikalo mageni'. Wana JF huko mliko hali ikoje? Mimi nadhani amelidanganya bunge na Watanzania kwa ujumla. Wana JF mliko bungeni mmbaneni athibitishe au afute kauli.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ana maanisha wananchi wa jimboni kwake,si ndio maana walimchagua.
  wana raha kweli
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Nilifikiri ni mimi pekee nilnote hili jambo...kweli mwenye shibe hafai kumsemea mwenye njaa!
   
 4. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyo jamaa amechanganyikiwa na posho. Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Yaani kelele zote zinazopigwa hata na wabunge wenzake wa magamba hazieleweki. Huyu ni miongoni mwa wale wanaolala ndani ya bunge. Malizeni Budget muje huku vijijini mtatukuta . Wananchi wameandaa bakora, peoples power itawashughulikia.
   
 5. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sindio kauli za kila siku za wabunge wa CCM, unashangaa nini? ambao hawana uwezo wa kunywa chai ni kwauvivu wao tu, kwanini wasiende pale langoni bungeni kusubiri wabunge watoke ili wawasaidie pesa ya sukari na mboga? mbona ni jambo rahisi sana. Bravo Simbachawene kwa ukweli na uwazi.
   
 6. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hapo yuko kwenye ubnafsi hata kama anazungumzia kwa watu wa jimbo lake bado hana usahihi asemalo
   
 7. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Jimboni kwake wamechoka tu kule..wagogo wana shida sana..tatizo akili zao zimekaa kuomba omba tu (samahani sana watani zangu wagogo, ila ndio ukweli). Nimewahi kuwa Kibakwe kule hadi Wota kule mlimani kwa wagogo wahehe (huko wanajua ushirikina tu!!)
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Aache upuuzi wake
  Watu wanalala bila kula sembese chai?
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ameamua kusema kilichofika kinyani mwake!nafikiri hajafanya utafiti wa kutosha!!
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hao sijui ni Watanzania wa wapi, maana huku kwetu ni uji wa chumvi kwa wachache.....
   
 11. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Inaonekana hajui shida za mtanzania wa kawaida!!
   
 12. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  masikini chawene.....uenyekiti wa kamati unakuponza!
   
 13. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Labda kikombe kimoja kikavu cha chai, au chai maana ya chai, chai ya maziwa, Supu, vitafunio, matunda?
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  <br>Inabidi aombe radhi kwa kweli...<br>Nadhani ambao wanalala na njaa wakimsikia wanaweza kumpiga...
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  On a serious note,

  Nadhani ametumia tafsida, chai ni rushwa kwa hiyo ana maana hakuna Mtanzania anayeshindwa kupokea rushwa.


  Kwa hiyo hajadanganya bunge hata kidogo
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  .....Hivyo ulivyotaja Chatu Dume vinapatikana kwa wenye uwezo tu, huku kwetu Kavifuti ni msamiati huo...
   
 17. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 1,044
  Trophy Points: 280

  Mkuu,

  Kibakwe iko Mpwapwa na nimebahatika kuishi huko kwa muda mreeefu sana na hali halisi ni hii:

  • Watanzania wengi huko wanakula chakula chao cha jioni saa 12 jioni, si-kwasababu wanapenda laa hasha bali ni kwavile wanakosa hata sh 150= ya kununulia japo koroboi moja ya mafuta ya taa. Hivyo inawalazimu wale mapema na kulala kabla ya giza kuingia.
  • Kuna Watanzania wengi kule, wanafunzi na watu wazima ambao wanatembea pekupeku (bila viatu), kwa kushindwa kununua hata Katambuga (viatu vya matairi ya gari) kwa kukosa sh 1000= ya kununulia viatu hivyo.
  Je, kama wanashindwa hayo madogo hapo juu wataweza kununua sukari ya Sh 2000@ kilo?

  Mh. Simbachawene, acha unafiki hali halisi ya Mpwapwa na jimbo lako la Kibakwe vinajulikana sana. Unatukera kwa hili.
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  inawezekana kibakwe wako well off!
   
 19. z

  zamlock JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hana adabu mimi mwenyewe sijanywa chai mpaka sasa
   
 20. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa nini ccm mps na wanapenda kusema uongo! yani akisimama kiongozi yeyote toka ccm huwa asilimia kubwa ya atakachoongea ni uongo! ile ahadi waliigeuza!! yani badala ya "kusema uongo kwao mwiko" wanasema "kusema ukweli kweo mwiko" kama ni hivyo magamba hayatoki.
   
Loading...