Simba Yapiga Marufuku Mashabiki ''Kupiga Tochi'' Mechi dhidi ya Orlando Pirates

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,991
69,385
DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Simba SC umepiga marufuku Tochi za miale ya kijani, ambazo zimekua zikitumiwa na Mashabiki kuwamulika wachezaji wanapokua kwenye makujumu yao Uwanjani.



Simba SC imepiga marufuku Tochi hizo, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa Jumapili (April 17), Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.



Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema Mashabiki wa Simba SC wanapaswa kuacha mpango wa kuingia na Tochi hizo, ili kuinusuru klabu yao kutozwa faini na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.



“Mchezo wetu uliopita dhidi ya USGN, baadhi ya Mashabiki waliingia Uwanjani na hizi Tochi licha ya kupiga marufuku, Simba kama taasisi na kama klabu hatupendezwi na utamaduni huu, ambao sio utamaduni wetu,”



“Simba SC ina utamaduni wake, sio huu ambao baadhi ya wenzetu waliuchagua katika mchezo uliopita, tunawaomba sana Wanasimba wote huu mpango wa kuja na Tochi uachwe mara moja, ili kuinusuru klabu yetu kuingia kwenye kadhia ya kutozwa faini na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’. Amesema Ahmed Ally alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu (April 11).



Simba SC ilitinga Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’ kwa kishindo, kufuatia kisago kilichoishukia USGN ya Niger cha 4-0 Jumapili (April 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.



Simba SC ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi D ikiwa na alama 10 sawa na RS Berkane ya Morocco, huku ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USGN ya Niger zikitupwa nje ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.


KATIKA HATUA NYINGINE

BAADA ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutangaza michezo yote ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kuamuliwa na teknolojia ya Video Assistants Referee (VAR) kwa Tanzania itahusisha taasisi nne.

Ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa VAR kutumika Tanzania itatumika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya wenyeji Simba na Orlando Pirates kutoka Afrika ya Kusini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ofisa habari wa Simba Ahmed Ally ameeleza kuwa historia hiyo ya kutumia VAR kwa mara ya kwanza Tanzania itawekwa kwa usimamizi wa taasisi nne ambazo ni CAF, TFF, Azam TV na Simba.

“Azam tunafanya nao kazi kwa karibu pia ndio wenye haki za matangazo kwa hapa nchini hivyo tutaungana nao sambamba na CAF, TFF kuhakikisha kila kitu kinaenda ipaswavyo,” alisema Ahmed na kuongeza;

Tayari taasisi hizo zimefanya vikao na zinaendelea na vikao vikubwa vikubwa ili kuhakikisha hakiharibiki kitu na naamini itakuwa hivyo.”

Aidha Ahmed ameweka wazi kuwa bado hawajapata taarifa rasmi, mpinzani wao Pirates anakuja lini nchini lakini kuanzia leo watajulishwa na watatangaza taratibu zinazofuata.

Pia ameendelea kueleza kuwa waamuzi watakaochezesha mwchi hiyo watawasili Tanzania April 14 huku wale wasimamizi wa VAR wakitarajiwa kufika April 15.

Simba itajitupa Uwanja wa Mkapa April 17 kucheza na Pirates mechi ya kwanza ya robo fainali na mechi ya marudiano itapigwa April 24 na mshindi wa jumla atatinga nusu fainali ya michuano hiyo.



MY TAKE: Nawapongeza watani kwa hatua hii nzuri waliyofanya, tunategemea soka uwanjani sio figisu figisu, kama uwezo upo onyesheni sio vitochi/vimulimuli vya mchongo

SOURCE: Globalpublishers
 
Hiyo ni kauli ya kuzuga na unafiki tu ili uongozi wa Simba unawe mikono, lakini nyuma ya pazia uongozi wa Simba ndio wanaratibu uwepo wa tochi kwenye hiyo michezo.
 
Embu tuelimishane hapa.
Toka lini tochi zimezuiwa na CAF michezoni?
Adhabu yake ni nini?
Ni klabu gani imewahi kuadhibiwa kwa mashabiki wake kuhusishwa na tochi?

Ahmed Ally alipaswa kwanza kujibu hayo maswali.
 
Lazima nitinge na litochi tena kubwa kama mchi wa kutwangia udaga, CAF lazima walione
 
Gentamycin vipi mkuu..pole na kifungo ( BAN).
Usiwe mjinga hii ni I'd yangu

Jaribu kulinganisha hand writing,panick na ukali ukali wa huyo jamaa,sifanani nae

Mimi huwa sipost vitu serious Kama huyo jamaa ambaye kila anachosikia lazima alete huku

Mara zangu nyingi ni nyepesi huwa hazibebi uzito kiasi Cha kupigwa ban
 
Back
Top Bottom