Simba waliokula watu katika bonde la Rufiji

nimecheka sana icho kilio cha fisi akilia mamaaaa nakufaaa
 
Siku nyingine porini humo Selous Simba aliwakorofisha nini sijui mbwa mwitu.
Hakuna kitu Simba anaogopa ka hao wanyama.
Aloo wametoka huko kibati wanamkimbiza kimya kimya.
Sisi kwenye tenti letu tuko watatu mle ndani mlango tumeacha wazi.
Vuup Simba kazama ndani anahema.
Wala hakutuangalia kageuka kakausha anapiga chabo nje.
Baada ya muda wale mbwa mwitu wamekatiza mbio wanamfwata huku wanahema balaa.
Fikiria Simba Dume liko ndani mla limetugeuzia matako yake nalo linahema.
Lilikaa km saa nzima alafu badae kulipotulia hilo likatoka taratibu likatambaa mdogo mdogo.
Mda huo mle ndani wa kukojoa,kuhara alifanya.
Yule Simba sidhani km hakutuona,alitudharau tu kapita zake baada ya kuepuka kipondo cha mbwa mwitu.
Kama angeongea labda angesema "asante sana washkaji zangu binadamu mmeniokoa siku ingine msiache mlango wazi😆"
 
Kuna watu wanazaliwa ni wachamungu wa asili, Allah akuongoze na akusamehe wewe na mimi ndugu yangu.
 
Habari hii imenikumbusha sana kitabu cha "The Man-Eaters of Tsavo" cha John Henry Patterson. Kilikuwa kinazungumzia tafrani za simba wawili waliokuwa wanasumbua sana watu waliokuwa wakijenga reli huko Kenya, kilichapishwa mwaka 1907.

Nilipokisoma kile kitabu, na baadaye kuangalia filamu iliyotokana na kitabu hicho "The Ghost and The Darkness", nilifikiria sana kwamba simulizi kama hizi hazitakosa kuwapo na kwetu.

Nimefurahi kuona watu wameziandika, zinenikumbusha sana Muhoro Rufiji ambako mimi nilitembelea miaka ya 1990. Labda zinaweza kutengenezewa filamu nzuri kama "The Ghost and The Darkness".

Kitu kingine nilifikiria sana ni kauli ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliposema kwamba dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukila nyama ya mtu huachi utarudia tu. Nilifikiri sana Nyerere anajua vipi habari za kula nyama ya mtu? Baadaye nikagundua alisoma sana hizi habari na zilikuwa zimeenea sana miaka ya nyuma Simba walipokuwa wengi, na ilijulikana kuwa simba mla watu ni lazima auawe, kwa sababu akishaonja nyama ya mtu, lazima atataka tena kula mtu.

Ndiyo maana wamesema “Madhali maiti yameondolewa, simba yule atakwenda kumtafuta mtu mwingine amle.”

Ilinisaidia kuelewa muktadha wa Nyerere kusema vile kwa kusikia habari kama hizi na pengine kusoma vitabu kama "The Man-Eaters of Tsavo" ambacho kilikuwa maarufu sana wakati yeye anasoma.

Poppy Hatonn

View: https://youtu.be/FRnUzzQn2NI?is=5VqD_uXqXhUmqKA6
 
Huu ndiyo uzuri wa vitabu, vinakupa maarifa au mtazamo ambao hukutarajia. Unasoma habari za simba wala watu lakini unapata kuelewa vizuri kauli ya Nyerere.
 
Yule Mwandishi alikua ana waita Simba "Nyamamume"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…