Simba tujitahidi sana kumlinda kocha Fadlu Davids

Simba tujitahidi sana kumlinda kocha Fadlu Davids

Mngoni asiyepiga gambe

Senior Member
Joined
May 4, 2017
Posts
168
Reaction score
334
Kwa kile nilichokiona jana mbali na kuwa na mchezo mgumu ila jambo moja la uhakika ni kuwa Simba tuna kocha wa maana sub ya kipindi cha pili ya kumtoa Kibu na kumuingiza Nouma ilikuwa kete muhimu sana kulinda timu kutokana na maafa ambayo yangeweza kutukuta ,kuna mambo mawili kocha alitaka kuyasolve

1.Counter attack threat
Kocha aliona jinsi mohamed Hussein anavyoteseka kwa kukutana na 1v1 nyingi na kumfanya kuwa vulnerable kwenye attacks za berkane na hii ni kutokana na mfumo wa inverted wings style of play ya Simba(kibu na mpanzu) so ili kumuongezea support alihitaji kumuongezea mtu mwenye energy ya kurudi nyuma na ambaye hatokuwa inverted bali anaishia kwenye chaki na kupiga krosi(ili kumaintain idadi ya wachezaji nyuma ya mpira inapotokea counter attack)

2.Build up
Ili kushinda pressing ya Berkane namna moja bora ilikuwa ni kuwa na namba kubwa ya wachezaji kwenye phase ya kwanza (kuwa na option nyingi za pasi) na hiki kitu kiliwork kwa sababu Zimbwe sasa alikuwa na option nzuri za pasi ya mbele ama karibu(kwa nouma) at the same time alikuwa anabaki kama spare man kwenye build up na ulinzi hivyo mzigo mkubwa wa ulinzi ulipungua(mfumo wa kuwa na spare man kwenye ulinzi unatumika sana kushinda pressing na timu kama Man city (Ake ama Gvadiol) na Inter Milan( Damian).

Overall big up kwa kazi nzuri hususan,Ngoma(confidence and leadership presence yake ni muhimu sana) , Kagoma na Ahoua(work rate zao safi),Chamou pia alikuwa vzr nilitamani pia sub ya Mutale ingewahi kdg.by the way timu imepata test nzuri na improvement zinaonekana.
 
simba na yanga bado sana kuwalinganisha na level za RSB.

Wale jamaa mpira wanaujua aisee. Sema walivyopata zile goli 2 wakapoa.

Mpira wetu bado wa makelele na kutumika ki siasa.

Hongera kwa kujitahidi ila kipigo kitabaki palepale.
 
Pamoja na ubora wa Fadlu ila bado Simba ikapokea kichapo na mbeleko ya refa juu kupotezea penati mbili za wazi!! Hakika Simba ni timu mbovu yenye mipango na bahati!!

Hapa nimekumbuka ule msemo
"ukiona Kobe juu ya mti ujue kuna mtu kamuweka huko juu"

Makolo kwa mbinu za nje ya uwanja wako next level, Simba ichukue tu kombe lake la wamama isilostahili
 
Simba bado kwenye wachezaji hawana kiwango kikubwa sana labda yule mmoja mapanzu yupo vizuri ila wengine ni tia maji tia maji tu..
Mo ajipange pale hakuna timu ya kujivunia bado.
 
Simba na Yanga mshazoea kudekezwa na TFF, sasa kuleni dozi hiyo 😂

Na inatakiwa simba wagome kucheza Zanzibar mana caf wamebadili uwanja ghafla ili caf warudishe mechi Daslamu 😂
 
Fadlu ndio man of the match kwangu aongezewe wachezaji wa maana kwenye usajili
 
Fadlu ndio man of the match kwangu aongezewe wachezaji wa maana kwenye usajili
Atatoa pesa? Umsajili mtu kama Camara wa berkane..mwendo wa miln 600 na kuendelea ..tusema akina mpanzu kama 7 hivi ...shida za kusajili kwa kubahatisha wachezaji wengine waliosajiliwa hawaonekani
 
Pamoja na Mazuri yote ya Fadru kuna makosa alikuwa ameyafanya.

Alijua Ubora wa Berkane Dakika 20 za kwanza na Alisema kwenye Press Ila alishindwa kabisa kukabiliana na Berkane kipindi cha kwanza.

Kama ningekuwa mimi ningeanza na mabeki wa kati 3
Wing bak 2.
Viungo wakabaji 4
Nouma na Debora wasingekosekana kipindi cha kwanza
Mbele angekaa kibu peke yake.
 
Nadhan alitaka kushikilia bomba kipindi cha kwanza angalau iwe bila bila then kipindi cha pili aje na mfumo wa back 3 kama suprise angeanza na huo mfumo mapema huenda angekuwa amewahi kucheza karata yake ya siri ,ila kama kocha unapanga lako ila hauwezi ku control kinachotokea uwanjani
 
Fadlu ni kocha ila kama ilivyo kwa wengine nae atafukuzwa ama kutoongezwa mkataba
Nchi haitaki akili hii
Wakati mwingine ni namna ya kuanza upya au ukuaji wa timu au huenda kocha akatamani kupiga hatua zaidi sitegemei Fadlu kukaa zaidi ya miaka miwili au mitatu
 
Moja ya sababu ya kumtoa kibu ni, upumbavu wa kibu kudondoka Kila wakati anapopata mipira huku akimuangalia referee kutafuta hisani ya mwamuzi, Jana haikufanya kazi hio mbinu.

Hata ukabaji wake ni wa mihemko Kila akikaba alikua anakuta mpira haupo anabaki kushangaa.

angali Jana Kapombe alionekana akikaba kwa Kasi na kukurupuka akizifanya zile slide tackle hewa .

Kumuinguza nouma iliokoa sana ndipo tulipomuona Chamou akishika nafasi kubwa kukaba upande wa kulia zaidi.
 
Kapombe anakamia kukaba hajui wao ndio zile hamsa za miaka ile waliosababisha
 
Atatoa pesa? Umsajili mtu kama Camara wa berkane..mwendo wa miln 600 na kuendelea ..tusema akina mpanzu kama 7 hivi ...shida za kusajili kwa kubahatisha wachezaji wengine waliosajiliwa hawaonekani
Camara dau lake ni Bilion 36
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom