Simba (Tanzania) vs Ahli Shandy (Sudan)

Hongereni sana SImba Tanzania kwa kuwapa watanzania raha, matokeo mazuri sana hayo
 
Safi sana mnyama...hongereni sana kwa ushindi huu mnono,kwa kweli mnastahili na nawaombea mfike nane bora na baadae final na hatimae mchukue ubingwa na kuliletea sifa taifa letu ambalo kila uchao linaporomoka katika viwango vya FIFA...Am proud of you Simba...Kwa pamoja TUNAWEZA....Go Simba go....Nipo pamoja nanyi mpaka mwisho watani zangu

Hongera sana kwa kuweka unazi pembeni na kutanguliza utaifa. wewe kama mimi, kwani mimi ni mnyama damu lkn ktk mechi za kimataifa siku zote nasapoti timu za Tanzania hata Yanga. Mimi kwangu uzalendo mbele.
 
Hongere sana Mnyama Kwa ushindi mtamu. Zitto 25 (a.k.a Okwi) nakufagilia sana umenipa raha kwa goli la tatu. Pokea busu langu Mwaa mwaa mwaa
 
66,77,88 dakika ambazo al alhly shendi hawawezi kuzisahau

hii ni nadra sana kutokea katika soka. Hii kwa utabiri wa kinyota na bahati inawapa nafasi nzuri tena ya kufika mbali katika mashindano haya timu ya simba.

NAMBA YA BAHATI (6+6+7+7+8+8=42=4+2=6) KWA SIMBA NI 6 (s-perfect number). Namba hii kwa vile huunda na namba 1,2 na 3 inaashiria kuwa Simba katika mashindano haya itakuwa na uwezo wa kufunga kati ya goli 1, 2, 3 au 6 katika michezo yao yote. Ukifuatilia mechi zao za nyuma ndivyo alivyokuwa. Namba 6 huashiria furaha hivyo kila mechi simba watakayocheza tutegemea furaha kutoka kwao.
 
Simba juu, juu, juu zaidi.

Wanastahili kila sifa kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania ipasavyo.
 
Ushindi halali kabisa, vijana wamecheza. Nimependa hii dk ya 66 bao la kwanza, dk ya 77 la pili na dk ya 88 la tatu.
 
Safi sana mnyama...hongereni sana kwa ushindi huu mnono,kwa kweli mnastahili na nawaombea mfike nane bora na baadae final na hatimae mchukue ubingwa na kuliletea sifa taifa letu ambalo kila uchao linaporomoka katika viwango vya FIFA...Am proud of you Simba...Kwa pamoja TUNAWEZA....Go Simba go....Nipo pamoja nanyi mpaka mwisho watani zangu

Bala, kumbe upo Mkuu, nlikuwa sijiakuona, nimeamini kuwa wewe u mzalendo halisi.
 
Simba kumbukeni kuwa mkitwaa ubingwa wa CAF mtawasaidia Yanga kupata nafasi ya kushiriki michezo ya CAF, kwani nyie Simba mtashiriki kama bingwa mtetezi. Hili ndilo dua langu......
 
Back
Top Bottom