Simba Sport Club yafungiwa kusajili kisa Pape Ousmane Sakho

Kabla ya Kukutana na Yanga tulikuwa Unbeaten na furaha ilikuwepo..!!

Baada ya Kukutana na Yanga
-Tumekula Tano
-Tumefukuza Kocha
-Tume Draw Mechi Ya Leaue
- Now Tumefungiwa Kusajiri.

Yanga Ruined our Club, I hate Yanga Africa Official..

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
Na tumetoa jezi yenye matangazo ya Mo jersey yote.
 
Klabu ya ligi Kuu ya NBC YA Simba imefungiwa kusajili mpaka itakapolipa madai ya Klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mchezaji Pape Ousmane Sakho.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho. Kabla ya kujiunga na Simba, Sakho ambaye hivi sasa anacheza timu ya Quevilly Reuen Metropole ya Ufaransa alikuwa mchezaji wa Simba.

Klabu hiyo ilifungua kesi FIFA dhidi ya Simba ikidai sehemu ya malipo kutokana na mauzo ya Sakho. Simba ilitakiwa iwe imetelekeza uamuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa, lakini haikufanyika hivyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, TTF limeifungia Simba kufanya uhamisho wa ndani.

TTF inazikumbusha klabu kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za mpira wa miguu ili kuepusha adhabu mbalimbali, ikiwemo kufungiwa usajili wachezaji

Cliford Mario Ndimbo
Ofisa Habari na Mawasiliano, TTF
Novemba 23, 2023

View attachment 2822429
Janja Janja FC.
 
Simba yetu ilipofikia kwa sasa tunaona sawa hata ikifungiwa kwasababu usajili wenyewe unaofanyika hauleti mabadiliko kwenye ufanisi uwanjani.

Kramo = Juma Balinya
Onana = Patrick Sibomana
Saido = Sidney Urikhob
Ayoub = Kindoki

Sajili mbovu walizokua wanafanya wenzetu ndo wanafanya viongozi wetu sasa hv. Sidhani kama kuna mwanasimba ataumizwa na hii taarifa kwa sasa labda baadae machungu ya 5g yakiisha.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Simba ilipe hilo deni ili tufunguliwe usajili ili Jan kikosi kiimarishwe ila kama hatuna hela ya usajili mpya basi tutembee na huo upepo mpaka pesa itakapopatikana ila isiwe sababu ya kudhulumu, dawa ya deni ni kulipa.
 
Back
Top Bottom