Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,115
Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa uamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuifungua Simba SC kusajili mpaka itakapolipa madai ya klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu Mchezaji Pape Ousmane Sakho, klabu ya Simba imesema ilimuuza Mchezaji Sakho kwa klabu ya Quevilly Roven Metropole ya Ufaransa mwezi August 2023 na kwamba makubaliano ya malipo ni ya awamu mbili.
“Malipo ya awamu ya kwanza (50%) yalilipwa tarehe 2 October 2023 , Klabu ya Simba ilikuwa inasubiri awamu ya pili ili kuilipa asilimia 15% ya mauzo kwa klabu ya Teungueth ya Senegal”
“Klabu ya Simba inakiri kuwa kulikuwa hakuna mawasiliano na klabu ya Teungueth ya Senegal yaliyopelekea kadhia hii, hata hivyo, Klabu ya Simba inapenda kujulisha umma kuwa iko mbioni kukamilisha malipo hayo hivi punde, klabu ya Simba itaendelea kuheshimu sheria, kanuni na kanuni na taratibu za mpira wa miguu kama ambavyo imekua ikifanya”
Pia soma: Simba Sport Club yafungiwa kusajili kisa Pape Ousmane Sakho