Simba Sc ijiandae na fitna nchini Angola

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,243
103,945
By ELIUS KAMBILI
NILIKUWA pale Luanda, Angola na Namungo iliyokwenda kucheza na Clube Desportivo 1 de Agosto mwaka jana. Lakini wageni hawakugusa mpira hata wa mazoezi kutokana na vihoja kutawala nje ya Uwanja.

Simba msimu huu imepangwa kucheza na klabu hiyo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kati ya Septemba 7-9, mwaka huu jijini Luanda. Ngoja nikupe stori sasa.

Historia ya karibuni ya klabu za Tanzania dhidi ya Clube Desportivo 1 de Agosto, ni tafrani za mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopangwa kuchezwa Februari 14, 2021.

Mchezo huo wa kufuzu hatua ya makundi msimu wa 2020-21, ulipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Novembro 11 uliopo Talatona, pembeni kidogo ya Luanda, Angola.

Kabla ya Namungo kuondoka Dar es Salaam, mchezaji wao mmoja akiwa kwenye ngazi za kupanda kwenye ndege aliwaambia viongozi kwamba hataki kuendelea na safari kwa madai kwamba roho yake inasita. Wakamtema akarudi zake nje, sisi tukaondoka.

NAMUNGO HAIKUGUSA MPIRA ANGOLA
Tukatua Luanda sasa. Chini ya Kocha Hemed Morocco wakati ule, Namungo FC ilifika kwa lengo la kufanya mazoezi ya siku mbili kisha kucheza dhidi ya Clube Desportivo 1 de Agosto.

Msafara ulipowasili Uwanja wa Ndege wa Luanda, usiku wa manane, ulikutana na kigingi cha kipimo Uviko-19. Watu wanne kwa maana ya kiongozi mmoja na wachezaji watatu walikutwa na vimelea vya ugonjwa huo.

Wataalam wa afya waliovalia mavazi ya kijeshi ndiyo waliohusika na upimaji wa Uviko-19, na kwa mujibu wa kanuni za afya za Angola kwa wakati ule, wanne hao wakatakiwa kutengwa.

Pia ikatoka amri ya msafara mzima kwenda karantini, umbali wa kilomita zaidi ya 200 yaani umbali wa kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro. Msafara ulitumia saa zaidi ya tatu kufika huko.
Kumbuka msafara kabla ya haujaondoka Dar es Salaam wakati huo, watu wote walipimwa Uviko-19 na kuonekana hawana maambukizi.

Kasheshe ni kwamba hakuna mtu aliyekubali kushuka katika basi kuingia katika vyumba vilivyotengwa kama karantini ambako ingebidi wote wakae kwa siku saba.

SIMBA IJIANDAE
Kwa hali niliyoiona Luanda wakati ule ni muhimu Simba itazame haraka ratiba za ndege lakini kuwa kwenye mazingira salama zaidi ni bora kukodi ya kwao.

Bado kanuni za afya zinaweza kuigharimu Simba ukizingatia tahadhari ya Uviko-19 ikiwa bado ipo katika nchi nyingi za Afrika, hapo ndipo mahali penye umakini zaidi.

Timu ya Afya ya Simba inatakiwa kujiamini na kushirikiana kwa karibu na watu wa afya watakaokuwa wakipima kwenye uwanja wa ndege mara tu baada ya kuwasili Angola na hapa ni muhimu sana kutanguliza watu mapema na kuweka mazingira mazuri na Ubalozi wetu kwa lolote litakalotokea.

Timu nyingi za Afrika Kaskazini hufanya hivi zinapofika Tanzania na uhakika wa daktari katika kusimamia zoezi la upimaji hupunguza hujuma za wapinzani. Ingawa wenzetu wameweka mbele zaidi masilahi ya timu zao.

Clube Desportivo 1 de Agosto ni timu iliyoanzishwa Agosti Mosi, mwaka 1977 ikiwa sehemu ya Jeshi la Angola na inadhaminiwa na jeshi hilo. Inaendeshwa kiraia lakini kuna mikono ya jeshi katika utawala.

Labda wabadilike safari hii kwa kuhofia jina la Simba. Lakini umbali wa kutoka Luanda mpaka kutakapochezwa mechi ni mbali. Na hii hufanyika kimkakati kumdhohofisha mgeni.
 
Hao waliifanyia namungo sababu walijua ni maamuma wa hii michuano. Simba watu wao wataenda mapema. Na hata Red Arrows walipokwenda kucheza nao mechi ya marudiano, hawakukutana na huu undezi.

Na boli lilipigwa, ngoma ikaisha pacha 1-1. Agosto wakanufaika kwa mechi ya kwanza waliyoshinda. Hizi figisu wanaangalia timu za kuzifanyia.
 
Sio kwa Simba ya sasa.
Kweli kabisa. Hivi simba ni timu ya kuishauri kuhusu figisu za nje ya uwanja kweli!!!

As Vita Club wanawafahamu vizuri simba!!Juzi tu hapa Nyasa Big Bullets walilalamikia kuwekewa sumu kwenye chakula, halafu leo hii simba ipewa ushauri wa kujiepusha na figisu!!

Mbaya zaidi simba yenyewe inaanzia ugenini!!
 
By ELIUS KAMBILI
NILIKUWA pale Luanda, Angola na Namungo iliyokwenda kucheza na Clube Desportivo 1 de Agosto mwaka jana. Lakini wageni hawakugusa mpira hata wa mazoezi kutokana na vihoja kutawala nje ya Uwanja...
Kwani Angola hatuna balozi? Balozi wa Tanzania yupo atakuwa mwenyeji No 1 pia simba ni club kubwa hizo figisu washauri yanga
 
ahsante kwa ushauri ila nikuhakikishie tu Simba iko makini na ina uzoefu wa figisu za namna yoyote ile,tofauti na jamaa zetu waliofanyiwa zengwe mechi yao ya marudiano na Rivers utd wakapigwa goli moja sababu kuu hawana wanachokijua kuhusu figisu kwenye michuano ya caf.
 
Kweli kabisa. Hivi simba ni timu ya kuishauri kuhusu figisu za nje ya uwanja kweli!!!

As Vita Club wanawafahamu vizuri simba!!Juzi tu hapa Nyasa Big Bullets walilalamikia kuwekewa sumu kwenye chakula, halafu leo hii simba ipewa ushauri wa kujiepusha na figisu!!

Mbaya zaidi simba yenyewe inaanzia ugenini!!
Kweli sifa namba moja ya kuwa mwanayanga ni kujitoa ufahamu,ume comment kama kigelegele tu..
 
Kweli sifa namba moja ya kuwa mwanayanga ni kujitoa ufahamu,ume comment kama kigelegele tu..
Leo nimejua tafsiri ya Makolo kusema utopolo hatuna akili, kumbe mtu akitoa data au taarifa sahihi za kuiponda Simba tu tayari hana akili!

kweli nimeamini nyie Makolo ni mbumbumbu FC , sijasema mimi kasema Kolo mwenzenu mbumbumbu Ishmael m-adeni ya maha-rage
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom