Simba Sc hatujamalizaa. Saa 7 Mchana kinashuka chuma

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,241
103,918
Ins52160607660_4a1201f5c3d54c51be4d2a404810d707_362328429_165539406542189_3721156522173103136_n.jpg

Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa kipa wa kimataifa wa Brazil 🇧🇷 JEFFERSON LUIS kwa Mkataba wa miaka miwili.
. Jefferson (29) maarufu kama Mikono ya Sumaku anatua Simba kushindania namba na Aishi Manula aliye majeruhi.
 
View attachment 2696770

Achana na Bonanza la jana. Leo saa 7 mchana kinashuka chuma kingine.

Tetesi zinasema viongozi wameamua kuvunja benki. Taarifa ni kwamba katika kambi Uturuki ametua kipa kutoka Brazil 🇧🇷 Jafferson Luis aliyetambulishwa kwa wachezaji wenzake, lakini jana saa 7 mchana, Luis Mkandaji Miquissone naye alitambulishwa.

Tofauti na ilivyoripotiwa jana kwamba Simba imemsainisha kipa Mcameroon Simon Omossola anayetokea Saint Eloi Lupopo ya DR Congo. Ukweli ni kwamba Wekundu hao wamebadili gia na kumvuta Mbrazili Jafferson Luis mwenye miaka 29 aliyetambulishwa jana kambini Uturuki.

Kipa huyo Bora amesajiliwa kutoka Resende na baada ya Simba kumpiga chini Mcameroon, ambaye awali alipewa nafasi kubwa. Kipa huyo anatua Msimbazi kushindania namba na Aishi Manula aliye majeruhi.
tushaona jana tuna vikosi viwili na nusu hatuna presha...TABU YENU MAKOLO IPO PALE PALE kanjibai si anakaribia kukata tamaa!msimu huu ile tamaa ndo tunaikata mazima
 
SIJAWAHI kuwa na Imani na wachezaji wanaokuja Tanzania kutoka Nje ya Africa.

Simba wanaitaka KU bland Timu na kushindana na Akina MAMELOD

GOLIKIPA WA CAMEROON ALIKUWA MZURI MNO.
FC LUPOPO.
 
Mimi ni Yanga damu Ila safari hii Simba mmeamua tuna hofu kubwa sana na kosi lenu, sema ndo vile tunajitutumua tu mmetisha sana watani tuoneeni huruma kidogo..
Ila wewe jamaa kwa umalaya hakuna anayekufikia. Ulikuwa na Simba, ukawa na Rivers, ukawa na Marumo, ukawa na USMA, sasa hivi unajifanya upo na Yanga.
 
Back
Top Bottom