SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,151
- 7,922
Uongozi wa Klabu ya Simba baada ya kuona upweke wa kila msimu kuvuka hatua ya makundi hadi Robo Fainali katika mashindano ya CAFCL na kila mara kuwa timu pekee kutoka Tanzania, umeamua kuanzia msimu huu kuanza kuambatana na timu mojawapo ya ligi ya NBC itakayokidhi vigezo itakavyoweka.
Msimu huu upendeleo na bahati hii umeiangukia Yanga Afrika. Kumekuwa na mgawanyiko mkubwa ndani ya uongozi wa Simba kuhusu huu uchaguzi wa Yanga huku nusu ya wajumbe wakipinga na nusu wakiunga mkono wakitumia sababu za kizalendo.
Bado haijajulikana ni timu gani ambayo Simba itaamua iambatane nayo msimu ujao katika hatua hizi za wakubwa wa soka la Africa ila kuna uwezekano isiwe tena Yanga maana toka Simba iichague Yanga, hawa wateule wameonekana kulitia aibu taifa kwa kwenda kushangaa shangaa vikombe na jezi za Al Ahly huku wakiwatabiria mengi makubwa ambayo hata wenyewe hawajitabirii, jambo lililoitia aibu sana taifa.