Simba mlinda nyumba karibu na shule akamatwa Nigeria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Hebu tafakari hili, unatembea mjini halafu upite karibu na nyumba inayolindwa na simba wala sio mbwa.

Hiyo ndio hali waliokumbana nayo wakazi mjini Lagos, Nigeria baada ya mmiliki wa nyumba moja kuamua kutumia simba kama mlinzi.

Simba huyo wa miaka miwili aliripotiwa kuonekana katika nyumba moja ya makazi iliyo karibu na shule na kundi la jopokazi siku ya Ijumaa.

Simba huyo alikamatwa na kuhamishiwa katika hifadhi ya wanyama ya Bogije Omu mjini Lekki, mkuu wa jopo kazi hilo aliiambia BBC.

Mmiliki wa mnyama huyo ameamriwa kufika katika kituo cha polisi mara moja la sivyo akamatwe.

Kundi hilo linalojihusisha na masuala ya usafi wa mazingira na kitengo cha upambana na uhalifu mjini Lagos liliingilia suala hilo baada ya wakazi kuwasilisha ripoti kwa wizara ya mazingira.

Msimamizi wa shule hiyo amesema kuwa walitilia maanani usalama wa watoto.

Inaaminika kuwa simba huyo aliletwa katika nyumba hiyo miezi miwili iliopita.


Chanzo: BBC Swahili
 
Hiyo ni moja kati ya vituko lukuki vya Nigeria, kama nyumba haina fensi na simba kapiga pozi tu nje analinda mlango hiyo kubwa kuliko, ila kama nyumba ina fensi salama jamaa afuatilie tu kibali cha kummiliki, hiyo ni silaha kama silaha nyingine..
 
Aombe kibali tu,hana tofauti na mtu anayetumia mbwa au aliyeajiri Masai
 
Back
Top Bottom