Simba kapakatwa pub

Simba kapakatwa pub

Kijitonyama maeneo ya makumbusho barabarani kabisa kuna hii pub mpya imefunguliwa.
Nahisi bia za pale zina raha ya ajabu kutokana na jina lake.


attachment.php

OMG.....meeeen!!!:laugh:
 
Hiyo Pub ni chungu kwa wanasimba maana tutampakata kweli simba hapo j2.
 
Jumapili hiyooooooooo hahahaha yaani haina majotroooooo lazima tupakate mnyama hahahahahaha
 
na bado tumeanza na simba utasikia tu chui amebambiwa..
 
Hahahaha kapakatwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
nilipita pale saa mbili giza liliharibu furaha ya watu lakini njemba moja likamwambia mhudumu awaongezee kila mtu kinywaji anachokunywa na amwambie bei yeye anataka kwenda kumalizana na mpenzi wake ambaye ni shabiki wa Simba,nilicheka sana sijui shemeji yetu aliahidi kutoa nini leo lol!
 
wadau hata mimi nimeshaiona hii pub..,ila sielewi kwanin owner ametumia hili jina,au anautani na washabiki wa Simba,kibiashara ikoje hii,.jamii imelipokeaje hilo jina +picha yake?

Kibiashara haina noma yoyote. Simba SC hana chake pale, endapo Simba SC angekuwa amesajili hiyo picha ama jina 'SIMBA kapakatwa' kama trade marks pale BRELA basi angeweza kufikisha mahakamani jambo hili. Kwa sasa sidhani kama hata hiyo nembo ya Simba SC kama imesajiliwa, anaweza akaibuka mtani siku moja akachumpa pale BRELA na kuisajili rasmi hiyo nembo yao kisha kuwageuzia kibano Simba waache kuitumia nembo hiyo usishangae!
 
Ndoto tuu...hata paka hapakatiki...halafu sio Simba SC aliyepakatwa...mtuache na timu yetu

Pole mdau punguza munkari... sisi tulibebwa jana tumewapakata..... Yametimia yalonenwa kwenye bango la iyo baa!
 
Back
Top Bottom