Simba inaendelea kudhihirisha ubora wake katika Mashindano ya CAF

Simba inaendelea kudhihirisha ubora wake katika Mashindano ya CAF

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
730
Reaction score
658
HSGu-mGXQAU_yHY.jpg
 
Wanaanza kukushambulia, utopolo wana Roho mbaya goli 6 wanazisikia tu hawajawahi kuzifunga kwenye haya mashindano😃
 
So far Tanzania hakuna timu bora kwenye mashindano ya CAF ngazi ya Vilabu ndo maana ranking za hizi timu zinabadilika kila msimu kuonesha kua kitu pekee cha kujivunia ambacho hakiwezi kupanda wala kushuka ni kubeba kombe tu. Ndo maana Raja, Wydad na TP Mazembe kwenye ranks wako mbali huko lakini wote hao wana ndoo 3 na kuendelea za CAF utawaambia nini? Sisi tumebaki kuringishiana ujinga tu sijui robo fainali 5 sijui kufika fainali, sijui nani anaongoza kwa magoli CAF ujinga ujinga tu
 
Hongera Simba kwa kupata ushindi lakini wachezaji na benchi la ufundi walikuwa na makosa mengi sana kiasi iwapo leo wangekutana na timu nzuri ingewagharimu sana. Kwa mechi ya leo ingekuwa ile Simba ya akina Bocco, Kagere, Chama na wengineo sasa hivi wangekuwa wameshajihahkikishia kusonga mbele. Ila Simba hii tia maji tia maji inajichelewesha yenyewe.

1. Kasali ana foot work mbovu sana lakini anajiamini balaa na chenga yake inatabarika. Ni basi tu ana bahati sio kwenye ligi ya ndani au kimataifa mpaka sasa hajatokea mchezaji wa kuweza kumsoma. Arudi akaangalie baada ya Roger Milla kumsoma Rene Higuitta nini kilitokea. Pia tabia yeke ya kupiga pasi usawa wa kati kati ya goli badala ya pembeni siku sio nyingi atatoa mlio.
2. Mligo naye ni mzigo tu. Huu msimu wa pili kwake lakini bado habadiliki kabisa. Anachojua yeye akipata mpira ni kuwapasia mabeki wake wakati au kiungo mkabaji basi kashamaliza kazi. Kuna muda anapata mpira mbele yake kuna nafasi wazi lakini hatembei kabisa na mpira kuisogeza timu juu. Kibabage sio mzuri sana lakini huwa ana take risk kwenda mbele kusaidia kuipush timu izidi kusogelea lango la adui.
3. Jabaar, Maema na Kagoma wote walikuwa wanacheza chini muda mwing wa mchezo kiasi ikawa shida kwa Simba kupeleka mashambulizi mbele. Mpaka Chama alipoingia ndio walau timu ilianza kusogea mbele.
4. Benchi la ufundi limezingua sana kwa sub ya Mpanzu. Doumbia alipoingia aliwaacha wale mabeki wa kati wa timu pinzani wafanya wanavyotaka kuanzisha mashambulizi kwa sababu walikuwa hawana mtu wa kuwakaba kama alivyokuwa Mpanzu mwanzoni mwa mchezo. Doumbia tatizo lake kubwa hajui kuwa yeye ni mtu wa mwisho anatakiwa asimame na wale mabeki wakati ili wasianzishe mashambulizi na hata ikitokea wamefanya makosa yeye afunge. Badala yake anarudi chini sana na kuwaacha mabeki wa timu pinzani watengeneze mashambulizi kuanzia nyuma.
5. Ni wakati sasa wa viongozi wa Simba kuwaeleza aina ya mkataba alionao Doumbia maana lazima acheze kila mechi wakati akiingia kazi yake kubwa ni kuanguka anguka, kukaba wenzake na kuzuia pasi zisiwafikie wachezajia wenzake. Ni kama vile Doumbia ana mkataba kama aliokuwa nao Saidoo Ntibazonkiza kila mechi lazima acheze.
6. De Reuck ni bonge la beki. Lakini ule upuuzi wake wa kukaa na mpira muda mrefu halafu anaanza kutembea nao anachelewesha sana mashambulizi na inawafanya timu pinzani ijipange. Sio kila mpira lazima uanze kwa build up kuanzia nyuma.
7. Kocha wa viungo hapo Simba aangaliwe vizuri. Timu haina utimamu kabisa wa mwili na hasa dakika za mwishoni timu inapoteana sana wachezaji wanabaki wanakaba kwa macho. Kama wamalawi wangekuwa makini leo kuna aibu ilikuwa inaenda kutoea dakika za mwishoni

Benchi la ufundi la Simba lazima libadilishe mfumo wa uchezaji. Haiwezekani timu inafika kwenye robo ya tatu ya uwanja halafu mpira unarudishwa nyuma. Ndio maana ushindi wa Simba siku zoteunakuwa wa shida sana na akishinda goli nyingi sana ni mbili hata kama wana uwezo wa kuipiga hiyo timu goli kumi. Na hapo utakuta viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wanaridhika kabisa. Wachazeji wanaanza kutembea uwanjani na mpira na kupigiana vipasi vifupi vifupi. Hizi back pass na square pass wanaziweza tu Barcelona kwa sababu wao wanazipiga na timu ina move mbele sasa Simba wanazipiga halafu timu bado ipo inazunguka kwenye eneo lao. Ndio maana wakikutana na timu inayokabia kwa juu wanateseka sana.

Ukiacha Libase, Oura, Chama, Kapombe, Kibabage na Mpanzu wachezaji wote waliobaki wao kazi yao kubwa wakipata mpira kitu cha kwanza ni kugeukia nyuma kwenye lango lao hata kama wapo katikati ya uwanja au hata karibu na lango la adui.

Mwisho ushauri wa bure kwa benchi la ufundi la Simba. Wafundisheni wachezaji wenu counter attack. Simba imeshambuliwa halafu wamepoka mpira eti mchezaji anapooza kwanza wenzake wapate nafasi waanze taratibu nyuma kwenda mbele wakati mshambuliaji wao alikuwa amebakia na beki mmoja tu kule mbele au ameshafungua pembeni. Pia wachezaji wajifunze kuwa sharp kwenye kuanza faulo na mipira ya kurusha. Sio lazima mpira urushwe na beki wakati mshambuliaji yupo karibu na mwenzake anaomba mpira kwenye nafasi.

Ni mtizamo tu.
Huu ndio ulikuwa mtizamo wangu baada ya mechi ya awali kule Malawi. Leo nimeiona Simba ya tofauti kabisa ambayo imeondoa hayo mapungufu almost karibu yote.

Kilichobaki sasa Simba mnipe ajira kwenye benchi lenu la ufundi.
 

 
Timu za Bongo kata stimu sana. Hapo ukimbana vizuri kuhusu mafanikio atakuambia Robo Fainali.

Kama sisi tunaonyesha ubora hao kina Mamelodi, Ahly,Pyramid, Esperance wanaonyesha nini?
 
Back
Top Bottom