Tetesi: Simba hati hati kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa!

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
13,226
Reaction score
20,578
Wizara ya michezo kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wa michezo imesema huenda club ya Simba ikazuiwa kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa kusherehekea kilele cha wiki ya Simba kwa sababu ya matengenezo yatakayoanza mapema wiki ijayo.

Matengenezo hayo ni maandalizi michuano ya Super League ambayo Simba itashiriki. Hivyo club ya Simba inashauriwa itafute uwanja mwingine ambao utatumika katika mchezo wa kirafiki baina yake na Power Dynamos ya Zambia tarehe 6 mwezi ujao.
 
TIMU kubwaa TIMU kubwaa kabisaa,[emoji1787][emoji1787]inalilia uwanja....KWENYE SUALA LA UWANJA
SIMBA NA YANGA NI TAKATAKA
 
Nilimsikia mayai akigusia hili suala.

MAJALIWA ALISEMA SIKU YA WENYE NCHI 6 AUGUST
 
Ule uwanja bado sana, Yaani sijui waliufunga kufanya shughuli gani.
 
Tamasha lihamishiwe leaders club wanapofanyia Fiesta cloud media.

Kwani shamba la bibi uwanja si upo free?
 
haka kajamaa kameshaanza kuleta uyanga, uwanja waliufungia muda mrefu lakini mpaka Sasa huduma za vyooni ni mbovu. Mashindano yanafanyika oktoba kiherehere chote Cha nini
 
A country with over 60 million population is depending only one quality stadium.
 
Wacheze uwanja wa uhuru, au waende kwenye ule uwanja wao wa Bunju. Maana hilo ni tamasha tu!
Na isitoshe uwanja unaandaliwa kwa ajili yao wenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…