A
Anonymous
Guest
Huku Tanzania ikiendelea kujiandaa kwa ajili ya mashindano makubwa ya AFCON 2027, muundo wa Uwanja wa Arusha Stadium umeibua mjadala mzito miongoni mwa wadau na mashabiki wa soka nchini. Sababu kubwa ni uwepo wa njia kubwa ya riadha inayozunguka uwanja na kutenganisha wanja wa mchezo na majukwaa ya mashabiki.
Tukilinganisha na Uwanja wa Zanzibar Stadium unaojengwa Fumba Town, tofauti inaonekana wazi. Zanzibar Stadium imeundwa mahsusi kwa ajili ya mpira wa miguu pekee, bila njia ya riadha. Hii inaruhusu mashabiki kuwa karibu na wanja, hivyo kuleta hamasa, msisimko na shinikizo halisi la soka ambalo linahitajika wakati wa michuano mikubwa kama AFCON.
Kwa upande mwingine, Arusha Stadium inaonekana kufuata mfumo wa Olympic Stadium kama vile vilivyo viwanja vya Benjamin Mkapa na New Amaan. Muundo huu unaweka umbali mkubwa kati ya pitch na mashabiki. Hoja inayotolewa ni kwamba uwepo wa running track ni uwekezaji wa muda mrefu ambao utasaidia michezo mingine kama riadha hata baada ya AFCON 2027.
Lakini hapa ndipo swali linatokea. Kenya ni nchi inayojulikana zaidi kwa riadha Afrika, lakini katika ujenzi wa uwanja wao mpya wa Talanta Stadium kwa ajili ya AFCON 2027, wameamua kutoa njia ya riadha. Pia tukitazama viwanja vikubwa kama vile vya Atlanta, vimejengwa maalum kwa ajili ya soka bila kuchanganya na riadha.
Hii inatufanya tujiulize, je ni sahihi kuendelea na mfumo wa viwanja vya michezo yote au ni wakati wa kuwa na viwanja mahsusi vya soka? Zaidi ya hapo, kwa nini wadau wa michezo, wataalamu na mashabiki hawakushirikishwa katika kupanga miundo hii tangu mwanzo? Tumekuwa tukiona Benjamin Mkapa ikiwa na running track, lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanaona hakuna manufaa makubwa yamepatikana kutokana na hilo kwa upande wa soka.
Kwa mtazamo wangu, tunapaswa kuweka kipaumbele kwenye soka kwanza wakati wa AFCON. Siku hizo chache za mashindano ndizo zitakazotangaza Tanzania duniani. Baada ya hapo tunaweza kujenga viwanja maalum vya riadha.
Je, wewe unaonaje? Je, viwanja vyetu vipya vya AFCON 2027 vinapaswa kuwa mahsusi kwa soka kama Zanzibar Stadium, au ni sawa tuendelee na mfumo wa michezo yote kama Arusha Stadium?