Soka Ndio Maisha Yangu
Senior Member
- Nov 27, 2024
- 110
- 377
Kama kuna wachezaji ambao ilituuma kuondoka Simba basi ni hawa wafuatao, Deo Njohole, marehemu Method Mogella ‘Fundi’, marehemu Hamis Gaga Gagarino, Zamoyoni Mogella let alone akina Chuji, Chama, Barnabas Sekelo, nashangaa sana media zinamkuuuza Zimbwe, kijana uwezo wake ni wa kawaida sana ss hv, kuna vijana wanazima sana upande wake ila wanaogopa kuja kwa sababu ya kuchezewa nje ya uwanja, lkn hakuna athari yoyote ile Simba ikitafuta mabeki wa pembeni wapya, cha msingi mashabiki wawapokee na wawape sapoti ili wazoee mazingira ya timu, unaweza kuwa mchezaji mzuri sana lkn jina la timu na presha ikakufanya uonekane ww sio kitu, mfano ni Omary Omary, kiungo aliyerudishwa kwa mkopo Mashujaa, Omary anajua sana mpira lakini mazingira yamemfanya ashindwe kucheza mpira, ana body nzuri sana, anajua kureceive mpira, ana nguvu shida mazingira tu.