Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
JK amewaahidi wakaazi wa Simanjiro kuwarudishia ardhi iliyoporwa na wawekezaji wa TANZANITE ONE mara baada ya mwekezaji huyo kumaliza kuyachimbua madini yote ya TANZANITE yaliyomleta hapa nchini.
HAta hivyo, kulingana na takwimu zao wenyewe TANZANITE ONE uhai wa mgodi huo ni kati ya miaka 50 hadi 100 ikiashiria ya kuwa katika uhai wetu hatutaona ardhi hiyo ikirejeshwa kwa wamiliki halali.
JK hakutoa ahadi ya jinsi gani kama akifanikiwa tena kuendelea na kipindi kingine cha Uraisi ataboreshaje mapato yatokanayo na madini hayo hali ambayo inamaanisha anaridhika na makombo kidogo ambayo Halmashauri ya Simanjiro hutupiwa na mwekezaji huyo.
Kwa hiyo na kwa kifupi sana miaka mitano ya JK na CCM yake itakuwa "business as usual" na wala hakuna mabadiliko makubwa ya kisera au kisheria ili kufanikisha njozi ya watanzania wote ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA."