Kwanini Mungu kwa mapenzi yake bila sisi kumuomba akatuumba ili atutese? Kwani tulimuomba au kumlazimisha atuumbe?

Atlast nimempata

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
282
455
Nimeikuta sehemu ikabidi niizoom hapa! Nimecheka aliposema kwanini Mungu kwa mapenzi yake bila sisi kumuomba akatuumba ili atutese?

Kwani tulimuomba au kumlazimisha atuumbe? ! Wee jamaa!

Look! Mungu alitoa sehemu yake ya uungu akaumba mwanadamu! "akampulizia pumzi ikawa nafsi hai" kwa ufupi sisi tulikuwapo ndani ya Mungu.

Kwa waliosoma chemistry kuna theory inasema "matter can neither be created nor destroyed but it can be transformed from one form to another!

Binadamu ni pumzi ya uhai wa Mungu (immortal) kama Mungu alivyo immortal, kinachokufa ni mwili ambao ni mavumbi na kurudia ardhi!

Ukifa unaendelea kuishi ama maisha mazuri au mabaya kadri utakavyochagua kwasababu una nafsi yenye utashi wa mazuri na mabaya! Roho haifi!
 
Kwan unazan wote tunateseka mkuu? Wengine fresh tunafurahi mkuu. Anyway kuishi ni kupambana na ukipambana utashinda na kuishi kwa raha, kumbuka ulikuwa mmoja wa mamilion ya shahawa na ukatoboa sasa kwanin uteseke dunian??

Lakin pia kama unapingana nae ili uache kuteseka, unaweza jiondoa kwenye hiz mbio za maisha.

Note, huu n msimamo wangu binsfsi sijajibu kidin kumtetea Mungu, naamin kama yupo ananguvu za kujitetea mwenyewe.
 
Lengo la Mungu halikuwa hivi! Ila Adam na Hawa walivyotenda Dhambi hali hii ndio ikatokea,Lakini hata hivyo Mungu akatuandalia wokovu mwingine! Kupitia YESU kristo pale msalabani tukapata neema nyingine! Hivyo tumuabudu Mungu na kuzishika amri na Sheria zake! Tutende yaliyo mema Hapa duniani, Tuwe na hofu juu ya Matendo mabaya na Yeye ameahidi kuwa mkitenda mema na kuacha Dhambi mtaurithi ufalme wa mbinguni amina
 
Mungu alitoa sehemu yake ya uungu akaumba mwanadamu
Means na wewe au sisi Mimi na wewe ni Young God & Goddess Ila tumenyimwa ile nguvu yenyewe ya kimungu mfano kutokufa na kuexist milele kwenye mwili wenye nyama wanaita immortal au immortality

Na tungekua na hio hali ya immortality au immortal nahisi dunia isingekua sehemu salama pa kuishi nafkiri kuna Maisha baada ya kifo na kuna Uzi mwembamba sana unaotenganisha kati ya Kifo na Uhai na km tungepewa hio nguvu ya kutokufa ndani huu mwili wenye nyama dunia ingekua imeshaangamizwa kitambo sana,

Chukulia mfano tu Israel & Palestine jamaa wanatunguana kwa visa na visasi ingekua hawafi nje na ndani ya miili threat target number 2 ingekua ni nini km sio kuifumua dunia ili wote tupotee?
 
Lengo la Mungu halikuwa hivi! Ila Adam na Hawa walivyotenda Dhambi hali hii ndio ikatokea,Lakini hata hivyo Mungu akatuandalia wokovu mwingine! Kupitia YESU kristo pale msalabani tukapata neema nyingine! Hivyo tumuabudu Mungu na kuzishika amri na Sheria zake! Tutende yaliyo mema Hapa duniani,Tuwe na hofu juu ya Matendo mabaya na Yeye ameahidi kuwa mkitenda mema na kuacha Dhambi mtaurithi ufalme wa mbinguni amina
Ila lengo la Mungu halikua hilo Mungu alitaka binadamu waishi kwa Uhuru wa kuamua na kuchagua pasipo kwenda kinyume na yeye Ila katika engineering ya Mungu kwenye mfumo wa mwanadamu aliplug in kitu kinaitwa kusahau sasa hapo ndio balaa linapoanzisha amemuumba mwanadamu kusahau ni rahisi sana mwanadamu kusahau mwanadamu anasahau kwamba yeye hakujiumba Ila aliumbwa dhumuni la Mungu halikua tuishi kisha tufe Ila uasi ulipoanza akaplug in life span ya mwanadamu inamaana ukiasi ukafanya yale yote ya kimungu umeambiwa usifanye lazima ufe, we're Young God's & Goddesses
 
Lengo la Mungu halikuwa hivi! Ila Adam na Hawa walivyotenda Dhambi hali hii ndio ikatokea,Lakini hata hivyo Mungu akatuandalia wokovu mwingine! Kupitia YESU kristo pale msalabani tukapata neema nyingine! Hivyo tumuabudu Mungu na kuzishika amri na Sheria zake! Tutende yaliyo mema Hapa duniani,Tuwe na hofu juu ya Matendo mabaya na Yeye ameahidi kuwa mkitenda mema na kuacha Dhambi mtaurithi ufalme wa mbinguni amina
Mungu ni Alfa na Omega anajua Mwanzo na Mwisho so wakati anamuumba mwanadamu alijua yote hayo ya kuwa mwanadamu wakat anaumbwa lazima tu atakuja kuanguka Dhambini. Kwangu ili ni swali ambalo halina majibu sahihi toka kwa wanadamu zaid ni nadharia tu za majibu ya kukariri na majibu ya fikra za mwanadamu anavoona. lkn swali hili halijawahi kuwa na majibu sahihi ndo maana pengine maandiko yanasema Mengine ni SIRI ya Mungu mwenyewe yaliyo juu yetu tusiyoyajua tumuachie kikubwa tujitahidi tu kuishi anavotaka na siku kwa watakaopata ama tutakaopata nafasi ya wokovu basi tutamuuliza haya tukiwa nae uko mbinguni.
 
Back
Top Bottom