Elections 2010 SIMANJIRO: JK ajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,427
911,172
JK amewaahidi wakaazi wa Simanjiro kuwarudishia ardhi iliyoporwa na wawekezaji wa TANZANITE ONE mara baada ya mwekezaji huyo kumaliza kuyachimbua madini yote ya TANZANITE yaliyomleta hapa nchini.

HAta hivyo, kulingana na takwimu zao wenyewe TANZANITE ONE uhai wa mgodi huo ni kati ya miaka 50 hadi 100 ikiashiria ya kuwa katika uhai wetu hatutaona ardhi hiyo ikirejeshwa kwa wamiliki halali.

JK hakutoa ahadi ya jinsi gani kama akifanikiwa tena kuendelea na kipindi kingine cha Uraisi ataboreshaje mapato yatokanayo na madini hayo hali ambayo inamaanisha anaridhika na makombo kidogo ambayo Halmashauri ya Simanjiro hutupiwa na mwekezaji huyo.

Kwa hiyo na kwa kifupi sana miaka mitano ya JK na CCM yake itakuwa "business as usual" na wala hakuna mabadiliko makubwa ya kisera au kisheria ili kufanikisha njozi ya watanzania wote ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA."
 
Unajua ccm sasahivi hawatoi ahadi tena, wanachofanya ni kulaghai watu. Kama huo mgodi uta-exist kwa miaka 50-100 ni kusema kwamba watu wa simanjiro wataendelea kukosa maeneo ya kuchimba madini au ardhi ya kufanyia shughuli zao kwa muda wa miaka takribani 80 ijayo. Kama mgodi umeanza kuchimbwa mwanzoni mwa miaka ya 90 hadi sasa ni takribani 20 kwahiyo, kikwete anaahidi kutekeleza ahadi yake baada ya miaka 80 na kwa namna yoyote ile haitarajiwi awe hai miaka 80 ijayo.

Kweli ccm ni waongo sana, na ahadi zao hazitekelezeki.
 
Jamani,
Ukipita barabara ya kwenda Simanjiro, utalia machozi.
Barabara ni mbaya aibu! Umasikini wa watu ni wa kutupwa! Yaani sielewi nini lengo la CCM kwa Watanzania kwa kweli.....
 
hivi kuna watu walikuwa wanamsikiliza kweli?? Kwenye huo mkutano? Wangemrushia hata mawe aua tshirt zanawatosha hawa jamaa wa simanjiro
 
Hilo jimbo si la ole sendeka yule mbunge "machachari" ambaye hana mpinzani ama?
 
Umachachari autoe wapi pumbavu tu naye..JK hana cha kusema kwa wananchi na CCM wameshikwa pabaya yaani kwa dadkika hizi msuli ushawadondoka uko magotini...Kuinana kuuokota wanaogopa nyuma yao wako watu wa pwani ...hahaaaa
 
Ahadi za JK ni usanii kwa ari zaidi, uongo kwa kasi zaidi, na ubabaishaji kwa nguvu zaidi. Dr. Slaa alishawapa angalizo kwamba ni maafa kuiacha sisiemu madarakani, kuweni makini
 
JK amewaahidi wakaazi wa Simanjiro kuwarudishia ardhi iliyoporwa na wawekezaji wa TANZANITE ONE mara baada ya mwekezaji huyo kumaliza kuyachimbua madini yote ya TANZANITE yaliyomleta hapa nchini.

HAta hivyo, kulingana na takwimu zao wenyewe TANZANITE ONE uhai wa mgodi huo ni kati ya miaka 50 hadi 100 ikiashiria ya kuwa katika uhai wetu hatutaona ardhi hiyo ikirejeshwa kwa wamiliki halali.

JK hakutoa ahadi ya jinsi gani kama akifanikiwa tena kuendelea na kipindi kingine cha Uraisi ataboreshaje mapato yatokanayo na madini hayo hali ambayo inamaanisha anaridhika na makombo kidogo ambayo Halmashauri ya Simanjiro hutupiwa na mwekezaji huyo.

Kwa hiyo na kwa kifupi sana miaka mitano ya JK na CCM yake itakuwa "business as usual" na wala hakuna mabadiliko makubwa ya kisera au kisheria ili kufanikisha njozi ya watanzania wote ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA."

Red Quote : Nimechoka, nimechanganyikiwa na kwa sasa naona giza..... So tunaachiwa ardhi as SCRAPER!!!!
 
Unajua ccm sasahivi hawatoi ahadi tena, wanachofanya ni kulaghai watu. Kama huo mgodi uta-exist kwa miaka 50-100 ni kusema kwamba watu wa simanjiro wataendelea kukosa maeneo ya kuchimba madini au ardhi ya kufanyia shughuli zao kwa muda wa miaka takribani 80 ijayo. Kama mgodi umeanza kuchimbwa mwanzoni mwa miaka ya 90 hadi sasa ni takribani 20 kwahiyo, kikwete anaahidi kutekeleza ahadi yake baada ya miaka 80 na kwa namna yoyote ile haitarajiwi awe hai miaka 80 ijayo.

Kweli ccm ni waongo sana, na ahadi zao hazitekelezeki.

Mbona sasa hata yeye atakuwa hayupo duniani. Uwiii, huyu mkwere ameanza kula ugoro nini??
 
Naona mkulu, alikosa la kuongea akaona basi walau atamke chochote. Wamasai na samaki wapi na wapi! Nashindwa kuelewa kama huyu mzee alikuwa serious kweli. Yaani anadanganya watu mchana kweupe peee!
 
Umachachari autoe wapi pumbavu tu naye..JK hana cha kusema kwa wananchi na CCM wameshikwa pabaya yaani kwa dadkika hizi msuli ushawadondoka uko magotini...Kuinana kuuokota wanaogopa nyuma yao wako watu wa pwani ...hahaaaa

Malaria Sugu kaipata hii?Wainame waone kimbembe chake...wameshika Simba sehemu nyeti hao CCM....
 
Kwa kweli hapo jeykey amepotoka kupita kiasi na huo ni uongo uliokithiri. Sheria ya madini ya 2010 inasema migodi ya madini ya vito imilikiwe na watanzania kwa asilimia 75 na leseni ya uchimbaji inatolewa kwa muda wa miaka 25 na unaruhusiwa kisheria kuhuisha leseni yako. mining licence ya afrigem inakwisha 2015 na wanaruhusiwa ku re-new hiyo leseni.. hichi alichofanya huyu msanii ni kiini macho kikubwa
 
Vita ikitokea kama angola, rwanda,ivor coast, etc.. Ndio tutajua umuhimu wa democrasia na tatakuwa na maendelea ya haraaka mana tumeshindwa kuwatoa ccm
 
vita hatuiwezi ndugu. Tukisikia milio ya risasi tunajikunyata.
 
Ukitaka kufahamu kweli JK amechanganyikiwa soma habari hii kutoka Tanzania daima
JK awakoroga Wamasai

na Irene Mark, Simanjiro

amka2.gif

MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, amesema iwapo atapata tena ridhaa ya kurudi madarakani atahimiza ufugaji samaki kwa jamii ya Wamasai ili kujiongezea kipato.
Kikwete, alitoa kauli hayo katika mkutano wa kampeni kwenye Jimbo la Simanjiro ambapo alisema ufugaji wa samaki kwa jamii ya Wamasai ni jambo geni lakini litawasaidia kuongeza kipato kitakachowasaidia kupambana na umaskini. Alisema watakapoanzisha mradi wa ufugaji wa samaki watapata soko ndani na nje ya nchi.
Hivi Jamani huyu JK hafahamu kabisa hata mila tamaduni za makabila yetu Tanzania. Wamasai wapi na wapi na SAMAKI?! Kwanza Masai akikuta tu nyumbani kwako umepika samaki kamwe hatakula wala kunywa maji kwako kamwe. Samaki ni HARAMU kwa Masai. Leo eti unamwambia Masai wafuge samaki bandala ya ng'ombe huu sio udhalilishaji wa hali ya juu kama sio umbumbumbu wa kupindukia.? Nimebaki kichwa wazi.!!

Ni sawa na JK aende Zanzibar ambako wakazi wake 98% ni waislamu halafu awahamasishe kufunga nguruwe ili kujiongezea kipato hivi kweli watakuelewa?! Hata kama nina washauri wabovu kiasi gani nitatumia akili zangu kutambua kwamba hapa ninaingizwa mjini, kwa ushauri huu nitaukataa on the spot na kum fire huyo aliyenipatia.

Nyerere aliwahi kusema mtu akikushauri jambo la kipumbuvu na wewe ukalifuata basi wewe ndiye mpumbavu wa kupindikia. JK anasitahiri kupumzika naona hawezi kufikiri sawasawa tena.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom