Simama imara ni mapito tu, usijichanganye

Simama imara ni mapito tu, usijichanganye

Usikate tamaa, usichanganyikiwe, usipoteze tumaini ni mapito yatapita na utakuwa imara zaidi. Mungu kamwe hawezi kufunga milango yote hata siku moja. Wanasema in the darkest moment there is always a twinkle in of light to lead you through

Changamoto Zipo katika maisha na huwa unakutana na magumu kuzidi ustahimilivu wetu, inafika mahali mtu hukata tamaa na kuamua kuchukua njia za mkato mojawapo ikiwa ni kufupisha maisha yake.

Njia nyingine ni kujaribu tiba mbadala, kuacha kumtegemea Mungu na kutafuta mambo ya giza ambayo hata hivyo ni mabaya Sana na humfanya mhusika kujenga maagano ya milele na kuzimu.

Mambo ya kutolewa nuksi kusafishwa nyota, kupewa kinga na ngekewa ni maagano ambayo kila yakiisha nguvu itabidi ukakoleze tena... Hayafai Simama na Mungu wako

Kuna changamoto za ndoa na familia.. Hili jambo halina maelezo ya kueleweka kuwa kwanini huwa hivi, lakini wanandoa wengi wanepitia kipindi cha changamoto za ugomvi kutoelewana, magonjwa kipato na hata mambo kuharibika tu bila sababu ya msingi.

Usijaribu kutafuta waganga wa kienyeji wataharibu badala ya kutengeneza. Kwakuwa utaingia kwenye maagano mabaya

Kumbuka kuwa mnakutana watu wawili tofauti, huu ni muungano wa kimwili, muungano wa kiroho huja na mengi sio kitu rahisi na hilo ndio huleta changamoto zote hizi.

Mkiweza kupita kipindi hiki salama mtashinda zaidi ya kushinda na mtakuja imara zaidi

Nawatakia Jumamosi njema
Ameeeen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna uzi uliandika january na huu zimegusa maisha yangu na kuniokoa na majanga yaliyokuwa yametegwa dhidi yangu na adui ambaye simtambui ni nani,baadhi ya ndugu walinidharau sana lakin walibaki midomo wazi pale Mungu alivyoamua kuniinua kwa kasi ya ajabu.,Kwa upande mwingine JF imekuwa rafiki kwangu,kila siku nasema Asante Mungu nashukuru kwa yote.
 
Kuna uzi uliandika january na huu zimegusa maisha yangu na kuniokoa na majanga yaliyokuwa yametegwa dhidi yangu na adui ambaye simtambui ni nani,baadhi ya ndugu walinidharau sana lakin walibaki midomo wazi pale Mungu alivyoamua kuniinua kwa kasi ya ajabu.,Kwa upande mwingine JF imekuwa rafiki kwangu,kila siku nasema Asante Mungu nashukuru kwa yote.
barikiwa zaidi

Jr
 
Ni kweli yaani Mimi Nina miezi mitano sina kazi na ninaishi na mdogo wangu wa kike, Mke wangu na mtoto wangu mwenye wiki tatu, Kilichonifanya nikabaki bila kazi ni aliyekuwa rafiki yangu alinidhulumu haki yangu kwenye biashara tuliyoanzisha wawili ambayo tulianza kwa mtaji Wa milioni moja laki mbili mwaka Jana mwezi Wa pili, mpaka ananidhulumu ni kuibinafsisha biashara na kuifanya yake tulikuwa tushaikuza na kufikia mtaji Wa Milioni ishirini na mbili(22). Ila mwezi Wa nne alinitumia ujumbe Wa msg nikiwa nyumbani mgonjwa ya kwamba me niendelee na mambo yangu nimwachie biashara yake na nimwambie nahitaji bei gani anitumie kama haki yangu, nakwambia nilipona gafla ila ndo hivyo akaniambia ndo msimamo wake na nikizidi mfuatilia atanimaliza kwa kuondoa uhai wangu, ilibidi niitikie kinyonge na akanitumia laki nne na elfu thelathin (430000) ndo kama haki yangu, sikuweza kumjibu bali nilizidi kuchanganyikiwa na sikuweza kumshitaki kwani hatukuandikiana. Nilikaa ndani kama wiki moja nikilia tu, akatokea mtu mmoja akanishauri anipeleke kwa mtaalamu(mganga) ili afanye mambo yake niweze rudishiwa haki yangu kamili japo nilikuwa siaminigi mambo hayo na ikawa Mara ya kwanza kwenda kwa mganga wa kienyeji, ila Huyo mganga alifanya mambo yake na akaanza kuniambia huyu rafiki yako ameshaingia kwenye ushirikina tena mkubwa sana na aliupatia huko anakoagiza bidhaa, na pia anatumia nyota yangu kwenye mambo yake, Alinichaji 2000 tu na kuniambia atajaribu kupambana nae ila arudishe haki yangu japo ni ngumu kwani rafiki yangu yupo vizuri kishirikina na atakapofanikiwa kumuweza ndo nitamlipa ujira wake, nilikaa kama miezi miwili bila kuona mafanikio ikabidi nirudie huko tena na kuuliza kulikoni na alijibu ngoma ni ngumu kwani jamaa kashagundua kuwa nimegundua umafia wake nami namzunguka, akanipa dawa ya kuogea na akaniambia niwe makini kwani jamaa kazidisha vita na Mimi, ndo mwanzo nilianza kupata maswahibu makali mengi, mke wangu aliyekuwa mjanzito nae akapata matatizo makubwa ya tumbo mimba ikiwa na miezi nane, nilipambana haikusaidia ila mke wangu ni mtu Wa maombi sana hakukubali kwenda kwa mganga Wa kienyeji, mimba ilipitiliza hadi miezi 10 na nusu akiwa anateseka nami nikiwa nimefulia sina kitu, Akajifungua salama ila mtoto akulia akahamishiwa Muhimbili, nakuambia mtoto aliwekwa ICU na mashine ya oksijen wiki mbili hajitambui, Mimi na mke wangu tulichanganyikiwa sana na kukata tamaa, Siku moja ya ijumaa mtoto akanyonya gafla kwani alikuwa hawezi nyonya tukasema kapona kumbe ndo mwanzo wa kuzidiwa zaidi, Jumamosi asubu nikamfuata Daktari Wa zamu nikamuomba aniambie kama mtoto wangu atapona au ndo napoteza muda, Daktari akamuita mke wangu akatuambia hivi nyie mnasali kweli tukamuambia ndio, akatuambia hebu angalieni na mambo ya wazee huko isije kuta ndo dawa kwani tatizo la mtoto wenu halionekani, nakwambia nilitoka pale kama chizi na kwenda kuomba ushauri kwa mama mmoja, alinipa namba ya baba mmoja nikampigia nikamweleza tatizo zima akaomba jina la mke wangu ili atumie nyota yake kuangalia tatizo, me nikamuambia anisaidie kwani sitoweza kwenda kwake siku hiyo kwani nashughulika na chakula cha mzazi tutawasiliana baadae na ikiwa poa nitamuomba huyo mama anipeleke kwake kesho yake. Mchana nilipofika hospitali nilishangaa kumkuta mke wangu ana furaha sana nikamuuliza kulikoni akaniambia mtoto anaendelea vizuri na ananyonya mwenyewe na ameshatolewa ICU na kukabidhiwa. Nilienda nyumban kwa furaha ila nilipompigia yule mganga kienyeji ili anipe majibu hakupatikana. Kesho yake asubuhi Mimi na yule mama tukaenda tukamkuta, aliniambi cha kwanza Jana uliona matokeo gani? Nikamueleza akaniambia tena ilikuwa kidogo nichelewe na kupoteza uhai Wa mwanangu, akaniambia matatizo yalianzia tumboni kwa mke wangu na ilikuwa kusudio afe yeye na mtoto ila ni Mungu tu, mbaya zaidi akasema aneyefanya haya ni mtu niliyegombana nae kwenye biashara na anataka kumtoa mwanangu kafara baada ya kunishindwa Mimi, akaniambia siku hiyo hawezi fanya kazi ila kuna dawa atanipa ya kumsaidia mama mtoto ili kuua ule uchafu mwilini kwa mama. Nilipeka ile dawa kesho yake kwa mshangao tukaruhusiwa kurudi nyumbani na mtoto wetu, Nikarudia kwa yule bwana akamalizia tiba na mpaka sasa ananidai kwani nilimlipa 22000 tu, Japo mpaka sasa nipo kwenye shida kwani sina kazi ila Nina Amani mwanangu anaendelea poa. Sijui kama nilifanya kosa kwenda kwa mtaalamu ila nitakwenda Kutubu. Ila naamini uchawi upo. Na nilipanga kumfanyia jambo baya huyo rafiki yangu ila baada ha kusoma hapa nimejikuta nikisema namsamehe bure. Story ya kweli inanihusu Mimi
Haya mambo ya kushare biashara na rafiki sio mazuri kabisa,mimi niliona kwa mama yangu mdogo alishare na rafiki yake ambaye alikuwa hajui iyo biashara lakin alikuwa na 70% ya kama mtaji na 30% mama mdogo kwa makubaliano biashara ikikua wafungue nyingine kila mtu awe kivyake lakin baada ya rafiki yake kujua biashara kidogo tuu akamwambia mama mdogo tuachane nakurudishia mtaji wako,yani nilimuona mama mdogo analia na kusema hajui anaanzia wapi pesa ilikuwa ndogo lakin aliamua kumwachia Mungu kwa moyo wa dhati kabisa na mambo yalimnyookea na yule rafiki yake biashara ilimshinda akapoteza mtaji ikabidi afunge..


Nyingine ni last year binamu yake binamu yangu alifariki ghafla na kuacha mke na watoto kisa ni walishare biashara na rafiki yake Mpemba baada ya biashara kwenda vizuri kadhulumiwa ikabidi aende mahakamani akaambiwa auze nyumba ya uyo mpemba ilikuwa haijaisha bado ili arudishe pesa yake ,mteja alivyopatikana kabla hajalipia uyo binamu akafa ghafla
 
Haya mambo ya kushare biashara na rafiki sio mazuri kabisa,mimi niliona kwa mama yangu mdogo alishare na rafiki yake ambaye alikuwa hajui iyo biashara lakin alikuwa na 70% ya kama mtaji na 30% mama mdogo kwa makubaliano biashara ikikua wafungue nyingine kila mtu awe kivyake lakin baada ya rafiki yake kujua biashara kidogo tuu akamwambia mama mdogo tuachane nakurudishia mtaji wako,yani nilimuona mama mdogo analia na kusema hajui anaanzia wapi pesa ilikuwa ndogo lakin aliamua kumwachia Mungu kwa moyo wa dhati kabisa na mambo yalimnyookea na yule rafiki yake biashara ilimshinda akapoteza mtaji ikabidi afunge..


Nyingine ni last year binamu yake binamu yangu alifariki ghafla na kuacha mke na watoto kisa ni walishare biashara na rafiki yake Mpemba baada ya biashara kwenda vizuri kadhulumiwa ikabidi aende mahakamani akaambiwa auze nyumba ya uyo mpemba ilikuwa haijaisha bado ili arudishe pesa yake ,mteja alivyopatikana kabla hajalipia uyo binamu akafa ghafla
Mmh...

Jr
 
Mshana jr we ni mganga wa kienyeji au mtumishi wa Mungu nashindwa kukuelewa
 
Mkuu
Ndg yangu Mbuna pole ila hakuna watu hatari km Waganga wakienyeji ukiweza niPM nitakupa majanga ya waGANGA yaliyonikuta hapa Barazani sivyema kuyaweka yote ila Tambua waganga ni mawakala wa Shetani....Nakitu cha kwanza ukienda kwa Mganga anachoangalia ni NYOTA yako kumbuka NYOTA ndio inayobeba Kila jema alilokujalia MUNGU kumbuka kila mtu humu Duniani hazaliwi kwa Bahati mbaya so waganga wakisoma Nyota yako wakiiona inang'aa Umekwisha hakuna kitu utafanya kifanikiwe....Naongea haya sikwakuhadithiwa yalinikuta Shukrani kwa MKE wangu alietangulia kumjua MUNGU wa kweli nilikwisa so Nakushauri achana na waganga utazidi kuangamia
Naomba uweke icho kisa hapa na mm nfaidike maana ni mhanga wa hilo jambo pia natanguliza shukurani
 
Back
Top Bottom