Usikate tamaa, usichanganyikiwe, usipoteze tumaini ni mapito yatapita na utakuwa imara zaidi... Mungu kamwe hawezi kufunga milango yote hata siku moja... Wanasema in the darkest moment there is always a twinkle in of light to lead you through
Changamoto Zipo katika maisha na huwa unakutana na magumu kuzidi ustahimilivu wetu, inafika mahali mtu hukata tamaa na kuamua kuchukua njia za mkato mojawapo ikiwa ni kufupisha maisha yake.
Njia nyingine ni kujaribu tiba mbadala, kuacha kumtegemea Mungu na kutafuta mambo ya giza ambayo hata hivyo ni mabaya Sana na humfanya mhusika kujenga maagano ya milele na kuzimu.. Mambo ya kutolewa nuksi kusafishwa nyota, kupewa kinga na ngekewa ni maagano ambayo kila yakiisha nguvu itabidi ukakoleze tena... Hayafai Simama na Mungu wako
Kuna changamoto za ndoa na familia.. Hili jambo halina maelezo ya kueleweka kuwa kwanini huwa hivi, lakini wanandoa wengi wanepitia kipindi cha changamoto za ugomvi kutoelewana, magonjwa kipato na hata mambo kuharibika tu bila sababu ya msingi. Usijaribu kutafuta waganga wa kienyeji wataharibu badala ya kutengeneza. Kwakuwa utaingia kwenye maagano mabaya
Kumbuka kuwa mnakutana watu wawili tofauti, huu ni muungano wa kimwili, muungano wa kiroho huja na mengi sio kitu rahisi na hilo ndio huleta changamoto zote hizi... Mkiweza kupita kipindi hiki salama mtashinda zaidi ya kushinda na mtakuja imara zaidi
Nawatakia jumamosi njema