Simama imara ni mapito tu, usijichanganye

Simama imara ni mapito tu, usijichanganye

Right message at the right time!!mshanajr barikiwa Kwa hili,kuna wakati MTU unaweza dhani kuwa dunia yote iko mgongoni mwako, ujumbe kama huu unatukumbusha mengi na kutufundisha!be blessed bro
 
Ndg yangu Mbuna pole ila hakuna watu hatari km Waganga wakienyeji ukiweza niPM nitakupa majanga ya waGANGA yaliyonikuta hapa Barazani sivyema kuyaweka yote ila Tambua waganga ni mawakala wa Shetani....Nakitu cha kwanza ukienda kwa Mganga anachoangalia ni NYOTA yako kumbuka NYOTA ndio inayobeba Kila jema alilokujalia MUNGU kumbuka kila mtu humu Duniani hazaliwi kwa Bahati mbaya so waganga wakisoma Nyota yako wakiiona inang'aa Umekwisha hakuna kitu utafanya kifanikiwe....Naongea haya sikwakuhadithiwa yalinikuta Shukrani kwa MKE wangu alietangulia kumjua MUNGU wa kweli nilikwisa so Nakushauri achana na waganga utazidi kuangamia

Pouwa Kaka nishakupm
 
Last edited by a moderator:
Ni kwasababu ubaya ni roho ya giza na Mungu ni nuru... Ukiwa mtenda mabaya hata uso huonekana wazi, kuna gaze fulani ya kutisha lakini ukiwa mtu mwema hata uso hupata nuru na mwili kuwa na afya
Sasa mshana jr mtu anakudhulumu haki yako na anajua kabisa anachokifanya sio sahihi halafu ndio hicho unacho kitegemea,halafu unaambiwa samehe saba mara sabini!!!!!!!

Basi tu inabidi kusamehe
 
Ni kweli yaani Mimi Nina miezi mitano sina kazi na ninaishi na mdogo wangu wa kike, Mke wangu na mtoto wangu mwenye wiki tatu, Kilichonifanya nikabaki bila kazi ni aliyekuwa rafiki yangu alinidhulumu haki yangu kwenye biashara tuliyoanzisha wawili ambayo tulianza kwa mtaji Wa milioni moja laki mbili mwaka Jana mwezi Wa pili, mpaka ananidhulumu ni kuibinafsisha biashara na kuifanya yake tulikuwa tushaikuza na kufikia mtaji Wa Milioni ishirini na mbili(22). Ila mwezi Wa nne alinitumia ujumbe Wa msg nikiwa nyumbani mgonjwa ya kwamba me niendelee na mambo yangu nimwachie biashara yake na nimwambie nahitaji bei gani anitumie kama haki yangu, nakwambia nilipona gafla ila ndo hivyo akaniambia ndo msimamo wake na nikizidi mfuatilia atanimaliza kwa kuondoa uhai wangu, ilibidi niitikie kinyonge na akanitumia laki nne na elfu thelathin (430000) ndo kama haki yangu, sikuweza kumjibu bali nilizidi kuchanganyikiwa na sikuweza kumshitaki kwani hatukuandikiana. Nilikaa ndani kama wiki moja nikilia tu, akatokea mtu mmoja akanishauri anipeleke kwa mtaalamu(mganga) ili afanye mambo yake niweze rudishiwa haki yangu kamili japo nilikuwa siaminigi mambo hayo na ikawa Mara ya kwanza kwenda kwa mganga wa kienyeji, ila Huyo mganga alifanya mambo yake na akaanza kuniambia huyu rafiki yako ameshaingia kwenye ushirikina tena mkubwa sana na aliupatia huko anakoagiza bidhaa, na pia anatumia nyota yangu kwenye mambo yake, Alinichaji 2000 tu na kuniambia atajaribu kupambana nae ila arudishe haki yangu japo ni ngumu kwani rafiki yangu yupo vizuri kishirikina na atakapofanikiwa kumuweza ndo nitamlipa ujira wake, nilikaa kama miezi miwili bila kuona mafanikio ikabidi nirudie huko tena na kuuliza kulikoni na alijibu ngoma ni ngumu kwani jamaa kashagundua kuwa nimegundua umafia wake nami namzunguka, akanipa dawa ya kuogea na akaniambia niwe makini kwani jamaa kazidisha vita na Mimi, ndo mwanzo nilianza kupata maswahibu makali mengi, mke wangu aliyekuwa mjanzito nae akapata matatizo makubwa ya tumbo mimba ikiwa na miezi nane, nilipambana haikusaidia ila mke wangu ni mtu Wa maombi sana hakukubali kwenda kwa mganga Wa kienyeji, mimba ilipitiliza hadi miezi 10 na nusu akiwa anateseka nami nikiwa nimefulia sina kitu, Akajifungua salama ila mtoto akulia akahamishiwa Muhimbili, nakuambia mtoto aliwekwa ICU na mashine ya oksijen wiki mbili hajitambui, Mimi na mke wangu tulichanganyikiwa sana na kukata tamaa, Siku moja ya ijumaa mtoto akanyonya gafla kwani alikuwa hawezi nyonya tukasema kapona kumbe ndo mwanzo wa kuzidiwa zaidi, Jumamosi asubu nikamfuata Daktari Wa zamu nikamuomba aniambie kama mtoto wangu atapona au ndo napoteza muda, Daktari akamuita mke wangu akatuambia hivi nyie mnasali kweli tukamuambia ndio, akatuambia hebu angalieni na mambo ya wazee huko isije kuta ndo dawa kwani tatizo la mtoto wenu halionekani, nakwambia nilitoka pale kama chizi na kwenda kuomba ushauri kwa mama mmoja, alinipa namba ya baba mmoja nikampigia nikamweleza tatizo zima akaomba jina la mke wangu ili atumie nyota yake kuangalia tatizo, me nikamuambia anisaidie kwani sitoweza kwenda kwake siku hiyo kwani nashughulika na chakula cha mzazi tutawasiliana baadae na ikiwa poa nitamuomba huyo mama anipeleke kwake kesho yake. Mchana nilipofika hospitali nilishangaa kumkuta mke wangu ana furaha sana nikamuuliza kulikoni akaniambia mtoto anaendelea vizuri na ananyonya mwenyewe na ameshatolewa ICU na kukabidhiwa. Nilienda nyumban kwa furaha ila nilipompigia yule mganga kienyeji ili anipe majibu hakupatikana. Kesho yake asubuhi Mimi na yule mama tukaenda tukamkuta, aliniambi cha kwanza Jana uliona matokeo gani? Nikamueleza akaniambia tena ilikuwa kidogo nichelewe na kupoteza uhai Wa mwanangu, akaniambia matatizo yalianzia tumboni kwa mke wangu na ilikuwa kusudio afe yeye na mtoto ila ni Mungu tu, mbaya zaidi akasema aneyefanya haya ni mtu niliyegombana nae kwenye biashara na anataka kumtoa mwanangu kafara baada ya kunishindwa Mimi, akaniambia siku hiyo hawezi fanya kazi ila kuna dawa atanipa ya kumsaidia mama mtoto ili kuua ule uchafu mwilini kwa mama. Nilipeka ile dawa kesho yake kwa mshangao tukaruhusiwa kurudi nyumbani na mtoto wetu, Nikarudia kwa yule bwana akamalizia tiba na mpaka sasa ananidai kwani nilimlipa 22000 tu, Japo mpaka sasa nipo kwenye shida kwani sina kazi ila Nina Amani mwanangu anaendelea poa. Sijui kama nilifanya kosa kwenda kwa mtaalamu ila nitakwenda Kutubu. Ila naamini uchawi upo. Na nilipanga kumfanyia jambo baya huyo rafiki yangu ila baada ha kusoma hapa nimejikuta nikisema namsamehe bure. Story ya kweli inanihusu Mimi

Aiseeee!!!!!! milioni nne tu inataka kunifanya nimtoe mtu roho ingekuwa kama wewe si ningekuwa nimesha chizika?

Ila kweli msamehe Mungu atakupatia zaidi ya alichokudhulumu
 
Kwa fedha za kodi zetu,wananunua Viongozi wetu waandamizi,wamewanunua wasanii wa muziki na maigizo,wamenunua vyombo vya habari kutangaza Live upuuzi na unafiki,wametafuna kodi zetu,wameuza wanyama wetu,wameuza migodi yetu,wamegawana nyumba zetu,wamemaliza twiga na tembo wetu,wamemaliza makaa yetu ya mawe,wamebinafsisha viwanda vyetu,wamehujumu madawa yetu,wamefilisi halmashauri zetu,wamewahujumu wataalamu wetu,wamewaharibu watoto wetu,wamewazeesha wazazi wetu,daaah!!Tumechooookaaaaa!!CCM sasa baaaasiiiiiiii!Namchagua Lowassa!!
 
Sasa mshana jr mtu anakudhulumu haki yako na anajua kabisa anachokifanya sio sahihi halafu ndio hicho unacho kitegemea,halafu unaambiwa samehe saba mara sabini!!!!!!!

Basi tu inabidi kusamehe

Somo la kusamehe kwa vitendo ni gumu sana lakini ukifaulu lina impact kubwa
 
Sasa mshana jr mtu anakudhulumu haki yako na anajua kabisa anachokifanya sio sahihi halafu ndio hicho unacho kitegemea,halafu unaambiwa samehe saba mara sabini!!!!!!!

Basi tu inabidi kusamehe

Ndg yangu hili Somo lakusamehe hata huko makanisani Linahubiriwa kwa msisitizo sana kwa sababu kwaakili zakibinadamu ni Ngumu lazima MUNGU ahusike zaidi...usiposamehe mtaishia kuuana...Hasira zikiisha unajikuta sehemu sio utajisikiaje....!!,
 
Kwa kweli bila Mungu kuingilia kati na mawazo toka kwa watu hii kitu ni ngumu sana
 
Kwa kweli bila Mungu kuingilia kati na mawazo toka kwa watu hii kitu ni ngumu sana

Lakini pia ni lazima mtendwa akubali kumwachia Mungu kwa dhati ya moyo wake kwakuwa hakuna kitu kibaya kama roho ya kisasi hasa pale shetani anaposimamia ukucha
 
Lakini pia ni lazima mtendwa akubali kumwachia Mungu kwa dhati ya moyo wake kwakuwa hakuna kitu kibaya kama roho ya kisasi hasa pale shetani anaposimamia ukucha

Moyo kukubali kuachana na roho ya kisasi nikikumbuka kweli nahisi nanyimwa haki

Ee Mungu simamia suala hili maana ni ngumu sana kila ninapokumbuka
 
Moyo kukubali kuachana na roho ya kisasi nikikumbuka kweli nahisi nanyimwa haki

Ee Mungu simamia suala hili maana ni ngumu sana kila ninapokumbuka

Kwa akili na uwezo wa kawaida wa kibinadamu ni ngumu ila unapomshirikisha Mungu miujiza hutokea
 
Kuna wimbo mmoja mzuri sana wa dini usemao
Tazama wewe ni Bwana Mungu wa vyote vyenye mwili.. Je kuna gumu lolote usiloliweza...!!!
Hakika hakuna Mungu hashindwi na hajawahi kushindwa.. Alisema wazi kuwa hatatujaribu kuliko uwezo wetu, kwakuwa kuna wakati magumu tunayopitia ni kipimo tu cha imani kwake

Lakini Tukumbuke vilevile katika maisha kuwa, Mungu huwa hawahi wala hachelewi katika kujibu maombi bali hujibu katika wakati uliokubalika... Siku moja kwa Mungu ni sawa na siku elfu kwa mwanadamu

Kuna wakati tunasongwa na mambo na kudhani kuwa Mungu katuacha kabisa lakini hebu jaribu kutembelea sehemu Kama muhimbili segerea gerezani utatoka na picha tofauti.... Haya ni mapito tu jipe moyo utayashinda yana mwisho vumilia kitu kimoja cha muhimu sana Usikate tamaa
Mshana Jr Umeshawahi Kupitia Magumu? Na Kama Ndio Huwa Unakabiliana Vipi Na Mapito Hayo...Nipo Kwenye Kipindi Cha Mpito Huu Mwaka Wa 3 Sasa Aisee Acha Tuuu..Imani Ni Kitu Kigumu Sana Yataka Moyo Kusimama Na Imani Yako Hadi Mwisho Wa Safari Ila Nitashinda Naamini
 
Mshana Jr Majibu Tafadhali
 
Jr
 
Usikate tamaa, usichanganyikiwe, usipoteze tumaini ni mapito yatapita na utakuwa imara zaidi. Mungu kamwe hawezi kufunga milango yote hata siku moja. Wanasema in the darkest moment there is always a twinkle in of light to lead you through

Changamoto Zipo katika maisha na huwa unakutana na magumu kuzidi ustahimilivu wetu, inafika mahali mtu hukata tamaa na kuamua kuchukua njia za mkato mojawapo ikiwa ni kufupisha maisha yake.

Njia nyingine ni kujaribu tiba mbadala, kuacha kumtegemea Mungu na kutafuta mambo ya giza ambayo hata hivyo ni mabaya Sana na humfanya mhusika kujenga maagano ya milele na kuzimu.

Mambo ya kutolewa nuksi kusafishwa nyota, kupewa kinga na ngekewa ni maagano ambayo kila yakiisha nguvu itabidi ukakoleze tena... Hayafai Simama na Mungu wako

Kuna changamoto za ndoa na familia.. Hili jambo halina maelezo ya kueleweka kuwa kwanini huwa hivi, lakini wanandoa wengi wanepitia kipindi cha changamoto za ugomvi kutoelewana, magonjwa kipato na hata mambo kuharibika tu bila sababu ya msingi.

Usijaribu kutafuta waganga wa kienyeji wataharibu badala ya kutengeneza. Kwakuwa utaingia kwenye maagano mabaya

Kumbuka kuwa mnakutana watu wawili tofauti, huu ni muungano wa kimwili, muungano wa kiroho huja na mengi sio kitu rahisi na hilo ndio huleta changamoto zote hizi.

Mkiweza kupita kipindi hiki salama mtashinda zaidi ya kushinda na mtakuja imara zaidi

Nawatakia Jumamosi njema

Hali ninayopitia sahivi huu uzi unanifariji asee, maisha yana changamoto sana
 
Back
Top Bottom