Sikuwai kuwa chimbo lakini nilikamatwa kwa kosa la kuwa chimbo

Bin wamakamo

Member
Dec 12, 2021
77
92
Soma upate funzo

Darasa la tano na miezi nane yake ilikwisha katika, masomo yalipamba moto miezi hiyo, kila mwalimu alijizatiti kumaliza topic zake kabla muda hujawa watupa mkono, fimbo zilitembea usipimee

Jumatatu ya nongwa kama nilivyokuwa naiitaga ilinikuta mchalo kweli kweli kwa kipindi kile kumiliki elfu tano haswa kwa shule zetu za sant kayumba ilikuwa gumu, achana kuwa nilizipata wapi zingatia kuwa siku ziiba zilikuwa pesa halali kabisa kwa matumizi ya mtanzania

Asubuhi nikawai visheti kabisa na bagia nikazitafuna haswa, kisha kengele ya mstalini ikatukasanya pamoja, wala sikuwa na chembe ya shaka siku hiyo unaijua pesa wewe ?mie sikuwai itunuku kuwa na tuzo ya sabuni ya roho hata siku moja, lakini kama mtu akisema ni sabuni ya mavazi na vikolo kolo vyengine sita funga kibwe bwe kubishana nae utazani mayele kafunga goli la offside na refa kaweka kati

Kwa kuwa pesa ni sabuni ya mavazi na vikolo kolo vyengine basi hata mie zilinifanya nijisafishe haswa shati langu piga pasi safi kata kucha tena siku hiyo asubuhi subuhi niliyakoga maji wakati haikuwa kawaida yangu, kutoka mguu mmoja umepakwa mafuta mwengine chwee! ndivyo nilivyozoeleka

Hivyo lilipoanza kupigwa bendi la “wachafu watoke mbelee” wala sikuwa pamoja nao kuugulia viboko vya mwalimu masalu na mwita maana hao ndiyo waliokuwa wakisifika kwa uchapaji pale shuleni

Matangazo ya hapa na pale yakapita tukaruhusiwa kila mmoja akaingia katika darasa lake kuendelea na ratiba ya masomo ya kila siku.

Kutoka saa mbili ya kuingia darasani mpaka saa nne ya mapumziko hapa kuwa mbali, lakini siku hiyo niliona kama saa yangu inaongopa, kila dakika niliangalia saa yangu mara tatu mpaka mara nne nne, lakini majibu hajakuwa na ziada yeyote zaidi kutia gazabu moyo wangu kwanini siku hiyo saa nne iligoma kufika haraka

Sikuwa wa kwanza kutoka darasani baada ya kengele ya mapumziko kugongwa lakini katika kwenye kumi bora ungenikosa katika mitihani tu lakini si hapo

Nikatoka na begi langu mgongoni pesa yangu kwenye soksi lenye buti juu, toka nilipo ipata ilini amuru vitu vya ovyo nikavifanya lakini ilipofika katika udhaifu wangu toka darasani akili ilikosa utulivu kabisa, azikuwaza kachori tamu za mama kibuyu wa miogo ya mzee chongo na ile pilipili yake.

Nikatoka kwa dhamila moja tu iliyonishika ubongo haswaa kwenda kwenye play station gemu, nikasuka mpango wangu, ambao kichwani ulikuwa rahisi tu hata kumsukuma mlevi ni kazi ngumu mnoo kisha ukafatwa utekelezaji.

Nikavuka geti la shule shangwe na vigele gele uko kichwani vilipamba moto haswa, nilitamani aliyetoa lile wazo kichwani hata ajitokeze ni mnunulie miogo kwa mzee chongo aniambie na yeye kuhusu pili pili yake kama ya Kado Cool au

Mpango wangu ulikuwa mrahisi mno utasema Rambo tu anavyo watoroka wa Vietnam katika first blood zake , nikaingia katika mjumba mmoja hivi uliyoko karibu na shule nikaficha begi langu kisha nikavua pensi ya shule nakubaki na bukta niliyo valia ndani ,juu nikabaki na shati lile lile la shule plan yangu A ikafikia asilimia zote 100 nikafika zangu katika gemu play station na kukuta watu nyomi kila mmoja akigombania kucheza Daah kwanza nikachoka na kwa kuwa nilikuwa kiuhalisia ile sio tabia yangu uchimbo basi, sikuwa na chaguo lengine zaidi ya kurudi nichukue begi langu na kwenda darasani kuendelea na vipindi

Nikafika nilipoficha begi langu sikulikutaa
Nilichanganyikiwa nikalia haswaa mpaka kamasi, kisha nikamuona mama mmoja akiinita kuwa niende kule alikokuwa nilipofika akaniuliza “wewe ndo umeficha begi umo mjumbani” nikaitikia kwa kichwa akaongea kwa sauti akaita “juma njoo upeleke huyu chimbo shuleni”
Roho ililipuka haswa yule Juma alinishika mkono pamoja na begi langu kisha akagoma kunipa ile bukta niliyoificha mule katika begi, bukta ya shule daa juma yule alikuwa kauzu utazani ile kazi aliyopewa ali ahidiwa donge nono
Akanifikisha mpaka shule, katika ofisi za walimu nikawakuta wamejazana koo mimacho yote mlangoni pindi naingia msobe msobe, Juma akatoa maelezo yote moja kwa moja sikuwa na lakuji tetea, nikapigwa viboko vyangu vilivyonitia mapepe mpaka nikaitoa ile pesa katika soksi kisha nikampa mwalimu na kumwambia ela ya tuition kisha akanigeuzia kibao kuwa nataka kumpa rushwaaa, nilijuwa kuandamwa siku hiyo kila neno likawa neno, ndo siku yangu ya kwanza kufanya jambo kama hilo tena si kwa Kupenda pesa wewe kweli mwanaharamu.

Mara mzee dakika si nyingi akaingia pale katika ofisi ya walimu sijui taharifa zile alimpa nani, tena ubaya zaidi alinikuta na pesa zile mkononi nimezishika baada ya mwalimu kukata kuwa nampa rushwa, akazichukuwa baada ya maelezo yangu kujitosheleza kuwa siku ziiba, kesi ikaisha kwa viboko lakini hata walimu walistaajabu inawezekana vipi chimbo mimi niliandika masomo na madaa zote za kusahisha nilihisha, stajabu yao aikufanya waache kunitembeza kila darasa kuwa mimi ni chimbo tena nilivyo kuwa maarufu kutokana ukoo wangu kuitwaa dondola ilikuwa haibu tosha.

Note: binadamu tunabadilika dakika tu changamoto zote tunazo pitia tusikose kusamehe na kutoa nafasi nyingine, sikila kitu ulichofanyiwa uyo aliyefanya alifanya kwa Kupenda, usihukumu moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom