"Sikutegemea" Nimeamini kila jambo lina sababu

"Sikutegemea" Nimeamini kila jambo lina sababu

Kitombise

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
8,652
Reaction score
25,849
Wasalamu wana MMU natumaini mu wazima wa afya, nawatakia weekend njema na maandalizi ya X-mass pamoja na mwaka mpya.
*************
Kipindi nko chuoni nilikuwa na GF wangu ambaye tulipendana sana.. na malengo yetu ilikuwa ni kuja kuoana baada ya kumaliza chuo. mapenzi yetu yakaenda hivyo hvyo kwa upendo wa juu kabisa... siunajua tena mapenzi ya kiscul scul jinsi yalivyo, yani ni full maigizo na mbwembwe nyingi.. huku tukiwa tunaongozana ongozana ovyo kama kumbikumbi vile. ilikuwa ni GOOD COUPLE Kwa kwel.

Sasa wakati tumemaliza chuo mwaka 2011 huku tukiwa tunaishi pamoja gheto na tukiendelea kutafuta kazi huku na kule. Siku mojo narudi home kutokea kwenye mishe zangu za kutafuta kazi, nkashangaa gheto liko ovyo kinoma alaf na mwenyewe hayupo.

nikiangalia begi lake la nguo na viatu vyake havipo.. Ndo nkapigwa na butwaa!! na kukumbuka kuna hela zangu 750000 zilikuwa chini ya godoro nimeziweka tokea kitambo. kwenda kuangalia sizioni, nikatafuta huku na kule wapi.. sikuziona. Nikajua tayari huyu demu kashaniibia.. ikabidi nmpigie simu lakini hakawa hapatikani, nkapiga kila mara sikumpata pamoja na kumtumia txt.

ikapita siku mbili tatu, nkamcheki hewani simu ikaita.. alafa akapokea nkamwambia "vip, inakwaje umeondoka na mkwanja wangu alafu hukuniaga? akanijibu "amepata dili la kwenda Canada hvyo pesa zangu atanirudishia soon" basi nkamwambia Poa.

nikamisikilizia dakika,saa mwezi, miaka na miaka lakini wapi... No kunorudishia mkwanja No nini!!!..

*****BACK TO POINT******
sasa leo wakati niko church ukafika muda wa kutoa sadaka, nikaingiza mkono mfukoni nkachambua chambua nikatoa pesa bila kuiangalia nmetoa sh. ngapi nikaitumbukiza kwenye kapu la sadaka.

Heeee!!! ile tumetoka naangalia pesa zilizopo mfukoni nakuta nna buku mbili tuuu, huku wakati natoka home kuja church nilikuwa ma 12000, nijlkajua yesss kwenye sadaka nmetoa 10000 badala ya 2000 na huku salio kweny account liko empty nkajiuliza leo nitaishi vipi wakati hii 10000 nilikuwa nmeipangia nikitoka church nipitie shop nnunue mazagazaga ya msosi.

akili ikanituma niende ofisi ya kanisa nkawaeleze labda wanaweza kunisaidia. nilipomweleza mzee wa kanisa akasema "sasa nitaamini vipi kama ulitoa 10000?

ila akasema kama ni kwel basi acha tuu, huwezi jua Mungu anakusudio gani juu yako. nikaona isiwe noma.. nikasepa zangu.
nilipofika home nikafunga mlango nikaenda kwa mshikaji wangu ili niangalie uwezekano wa kuimaliza siku ya leo. nikafika home kwangu nikamkosa, nikampigia cm akasema "ametoka kidogo na atachelewa kurudi" nikabidi nirudi zangu home.

ile nafika tuu namkita yule EX wangu aliyeniibiaga kipindi kile amekaa kwenye kiti ananisubiri. hapo sa hiyo hasira zimeshanipanda najiuliza kichwani "hivi nimfanye ninu huyu" kufika akanisakimu kwa furaha huku akinikumbatia lakini mimi sikuonyesha kujali.. nkamuuliza nani amekuelekeza hapa ninapoishi? akajibu "kwa mtu umpendaye lazima ajue tuu. Ok nikamkaribisha ndani tulupofika akanipa bahasha akasema nmekuletea fedha zako, mimi nikajifanya kama vile haikuwa na haja kwani nilikwisha msamehe tokea kitambo.. akaning'ang'aniza nikabidi nizipokee ile kuhesabu nikakuta ni 1000000 nkamwambia mimi nakudai laki 7 tuu hvyo hizi laki 3 chukua akasema " hizo ni riba" nikaona poa nikachukua..

akasema "nmekumiss sana hivyo leo nitalala hapa.. nkamwambia poa..
yani mpaka muda huu ninavyiandika hapa niko naye.. na tayari nmeshapasha kiporo tayari.
SASA NDO NIKAKUMBUKA MANENO YA YULE MZEE WA KANISA ALIPONIAMBIA "KILA JAMBO LINA SABABU.

ona sasa elfu 10 imezaa milioni 1.

Ninafuraha ajabu na nmeshasahau kitu alichonifanyia kipindi cha nyuma. YANI LEO NI MWENDO WA KUPASHA KIPORO KWA SANAAAA, NA WEEKEND YA LEO TUNAIMALIZIA KWA MAUTAMUZI KWA KWENDA MBELEEEEE.

nawasilisha jamani na nitakuwa nawapa Updates


********UPDATES************
Jamani msishangae ni kwa nini nilikuwa kimya!! simnajua tena mambo ya kupasha kiporo, cm inakubidi iwe mbali na ww.
kwa muda kama huu nikiiendekeza sana cm nitakuwa narusha stimu, yale MAUTAMUZ sasa sitayapata..

Ok sasa baada ya kupasha kiporo, si mtoto akaanza tena kuleta zile story za zilipendwa.. mara oooh! naomba turudiane tuwe kama zamani..
mara "ni shetani tuu alinipitia, ila yote maneno mingi ila wimbo ni ule ule wa kutaka kurudiana tuu.
ok, nkaona nisimtese sanaaaa, nikabidi NIFUNIKE KOMBE MWANAHARAMU APITE tuu... alafu mtoto sasa hiv alivyotusua kimaisha..!!! yani bussines zake ni nje ya nchi to bongoland, China, Dubai--Tanzania.
halimashauri yangu ya kichwa ikaona siyo mbaya na mimi kujisogeza kwenye uwaridi, siunajua ni must na mimi ninukie tuu.
yani mtoto ni mtamu balaaa, sasa sijui alikuwa ajapigwa siku nyingi Kwichi Kwichi? siunajua tena chuma kikiaa sana bila kusafishwa ni lazima kipate kutu, hivyo nikaona na mimi niondoe kutu...
Sasa muda huu ndo tumemaliza kuoga hapaa, ndo nafikiria nimpeleke kiwanja kipi, nikajilie Mautamuzi##"
**Updates zinafata kulingana na matukio yanayoendelea


*******UPDATES*********
oooh!! yan hapa nilipo ni full hang over kwa kwenda mbeleee. uchovu siyo uchovu, alafu ndo kwanza ndo tunaamka sasa hivi...
Enewei, sasa baada ya kutoka tukaenda club flani hivi amaizing tukatulia cool bar huku tunapiga masanga kidogo bila kusahau tumeshaweka oder jikoni. sa hiyo mtu mzima najimwaya mwaya kumbe show kasimamia mamaaa, kwanza ukinicheki nmepiga cheni ya silver nzito alafu na zile swaga flani hivi za kizimba..!!!
kumbe wapi.. the big boss ni boss lady. basi muhudumu akaleta rosti ya kutosha iliyosheheni kila kitu, mara kuku,mishikaki, chips kidizaini.. unaweza ukaiita mvurugo. basi mchizi nkawa nakula ile kislow motion utafikiri labda na mimi niko kwenye zile idara za wale wa makontena.
sa hiyo tunalishana utafikiri kama makinda ya ndege yanavyolishwa na mama yao..!!! basi mtoto mara acheke, atabasamu, aongee out of the point.. nikajua yessss huyu bia zimeshamnasa, sa hiyo mimi nmeshapiga kama chupa 4 hivi bila kusahau vile viroba vyangu vya nyagi nilivyovificha mfukoni.. yani demy akienda chooni tuu, bas mimi najichanganyia kiroba changu kwenye glass ya bia ili nizidi kudata zaidi. mtoto ile amerudi akasema twende sasa tukajirushe kwenye dance flow, mchizi sikuona noma ikabidi ninyanyuke ile kiulevi ulevi yani hatua mbili mbele tatu nyuma.
muda huo washikaji kibao wanaishia kula kwa macho jinsi demu alivyofungashia mzigo, yani kila tukidensi hivi, ndo jinsi mtoto anazidi kuwachanganya wale kwa macho. basi tukacheza weee, bila kusahau huku some time tunaenda kaunta kugusa bia mbili tatu, muda huo mtoto kalewa mbayaaaa hadi kutembea shida na muda huo ilikuwa ni kama saa 9 hivi za usiku.
basi nikaona kwa hali aliyokuwa nayo demu asije akamwaga razi mana kalewa mbayaa ikabidi nichukue tax ili turudi home, siunajua tena sikutaka mbuzi afie kwenye kidonda..
Basi ile kufika home tuuu mtoto ni kutapika mbayaaa nikabidi mmpe huduma ya kwanza then tukapanda kitandani kulala. usiku huo sikuweza kufanya lolote kwa kuwa tulikuwa tumelewa mbayaa ile kupanda tuu kitandani ni kukoroma tuu.
mida kama ya saa 2 asubuhi mkaamka huku nikimwacha mtoto akiwa amelala, basi nkaenda buchani kununua nyama na mazagazaga mengine ya kufungulia kinywa nkarudi home kuandaa muda huo kichwa kinauma mbayaa huku nikiwa mchovu balaa. hapo bila kusahau nilipoenda dukani nilikatia kiroba kikubwa kimoja..!!! basi baada ya kuandaa nkamuamsha mtoto kukabiga breakfast then kuoga after that tukarudi tena kitandani kupasha kiporo.
tukapasha weeeeeeee, alafu tuapitiwa tena na usingizi mzito, yani muda huu ndo tumeamka hapaa. demu kaenda kuoga huku mimi nikiwa kitandani natupia Updates namna hii.
 
2011-2015,700000-1000000, kaswende,kisonono,Hiv,mikosi,abortion...no matter, 12000_2000,nk. 2011 ulupomaliza chuo alikuwa 25age, 2015 @ 29...bado.. pambana...
 
Ha ha ha nyani haoni kundule?Mara hii hujui alikuwa wapi,kimahusiano alikuwa na nan? Haya kijana pasha kipolo yawezekana Siku ya Leo ukaijutia milele kupewa na VVU(vina vikali usipime)
 
Ha ha ha nyani haoni kundule?Mara hii hujui alikuwa wapi,kimahusiano alikuwa na nan? Haya kijana pasha kipole yaw ex ?lan a Sikh ya Leo ukaijutia milele kupewa VVU(vina vikali usipime)
ukiishi kwa kuogopa huwezi kufanikiwa kamwe..
 
Jitahidi jitahidi hivi hivi...
 
Ninachojua hakuna binadamu mkamilifu! kusameheheana ndio jambo la msingi chini ya jua. mwacheni jamaa ajilie tunda lake! msimtishe na maneno yenu!
 
Ninachojua hakuna binadamu mkamilifu! kusameheheana ndio jambo la msingi chini ya jua. mwacheni jamaa ajilie tunda lake! msimtishe na maneno yenu!

aah! hawa nmeshawazoea.. wanajua ku-UNLIKE na cyo KU-LIKE
 
Updates plz......hizi ndio akili zetu haswaa sisi wabongo! Anayebisha anyooshe mkono juu!
 
Yaani haya maisha hatari sana, yani hapo ulipoishia ndio yanapoanza yangu. Basi baada ya kunilipa million yangu tukaanza kupasha kuporo bwana, jana kucheki kwenye kamkoba kake nakuta ARVs tobaaaa.sorry nilikuwa naota
 
Kwa hiyo huyo mungu amekusaidia leo amekusaidia kwa zawadi kuu mbili
  • Ulipwe pesa yako na riba juu
  • "upashe kiporo"
Kweli ibada yako ya leo ilifika juu kwa mungu
 
Back
Top Bottom