ormystatus
Senior Member
- Nov 3, 2019
- 108
- 221
Nimepata fursa ya kufika eneo la MAGHALANI -MTWARA. Eh bwana eeh nilichokishuhudia imenifanya nijiulize mara mara mbili mbili kwa nini MTWARA mpaka sasa ipo nyuma kimaendeleo namna hii.
Yani maghala yamejaa magunia ya korosho na bandari ipo bize usiku na mchana. Order za watu zinasubiri meli zisepe, sawa tufanye hilo sio suala vipi kuhusu magari ya makaa ya mawe na Saruji yanayoingia na kutoka maghalani 24/7 mwaka mzima?.
Nadhani Serikali inapaswa kuongeza nguvu MTWARA ili kuharakisha maendeleo ukizingatia mikoa ya kusini ipo nyuma kimaendeleo.
MAPENDEKEZO.
Kuna maeneo yametengwa mtwara kwa ajiri ya Viwanda, hivyo basi kama Sekta binafsi zimeshindwa kufanya uwekezaji Serikali ijikakamue ijenge hata kiwanda kikubwa kimoja cha magunia (hasahasa ya katani) kwa sababu pesa nyingi tunapoteza kuagiza magunia ULAYA na ASIA.
Serikali itaweza hata kufanya ubinafsishaji mbele kwa mbele wakati huo uzalishaji ushaanza kama kuna muwekezaji atatokea. Na uzuri wake eneo la uzalishaji halitokuwa mbali na itakapotumika hiyo bidhaa ya magunia.

SEREKALI IJENGE KIWANDA KIKUBWA CHA MAGUNIA.

Kwa kujenga kiwanda cha magunia tutapiga ndege wawili kwa jiwe moja, tutaongeza zao lingine la biashara tofauti na Korosho ambalo ni Mkonge na ndo litakalolisha kiwanda cha magunia.SERA NZURI ZA KUFUFUA ZAO LA MKONGE MTWARA ZIWEKWE.
KUJENGA VIWANDA VIDOGO VYA KAMBA .