Sikutarajia kuumizwa namna hii!

Sikutarajia kuumizwa namna hii!

k majaliwa

Senior Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
140
Reaction score
187
Naamini mko poa.
Niende kwenye mada moja kwa moja.

Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa tunapendana sana. Nilikutana nae jijini Mwanza nilipokwenda kikazi July 2015.
Safari yetu ya mapenzi ilipamba moto kila mmoja akiwa na mapenzi ya dhati kwa mwenzio.

Tukiwa tumekubaliana kufunga ndoa hapo baadae. Tulifanya mambo mengi pamoja ikiwa kujenga nyumba na kununua gari pamoja, pia niliweza kufanikiwa kumuhamishia Moro kikazi angalau awe karibu.

Hatukuwa wa imani moja, yeye alikuwa mkristo na mimi muislam lkn hili halikuwa tatizo la kutuzuia kupendana.

Tulitembeleana na kuwasiliana Mara kwa Mara bila kikwazo.
Baada ya kumwambia kuwa wakati umefika tuanze taratibu za kufunga ndoa tulikubaliana kuwa ndoa tutafungia serikalini lkn kila mtu atabaki na imani yake.

Alipowaeleza wazazi wake utofauti wa imani wazazi walilipinga kwa nguvu zote, nikamuuliza yeye mwenyewe anasemaje akajibu ananipenda na asingetamani tuachane lkn pia hawezi kufanya kinyume na wazazi wake.

Basi wakati tunaendelea kulitafakari hilo mwenzangu akabadilika, nikimpigia simu anakata meseji hajibu, baadae akaniblock kabsa.

Kitendo kile kiliniumiza sana, nikaamua kumfuata Moro nikakuta alipokuwa anaishi amehama, kwasababu nilikuwa najua shule aliyokuwa anafundisha nikaamua kumfuata shuleni.

Nilipofika shuleni sikuamini kile nilichojimbiwa...niliumia sana..nikamsihi na kumpigia magoti mbele ya walimu wenzie lakini yeye akanijibu hatoweza kuendelea na mimi tena kwani tofauti za dini hazivumiliki , pia kaendelea kusema kuwa alikuwa na mpenzi wake zamani walipotezana lakini wamekutana tena na kuamua kurudiana.

Maneno yale yalikuwa ni mkuki ndani ya moyo wangu, nillilia kama mtoto, sikuweza kula kwa siku kadhaa.

Nikaamua kujiua maana nilijisemea moyoni sitaweza kumuona mwanamke ninampenda akiolewa na mwanaume mwngine. Lkn nilikuwa nao wakanisihi nisifanye vile. Sikujua nini cha kufanya nilikuwa mtu wa kulia tu.

Sikwenda kazini kwa siku mbili mpaka rafiki yangu ambaye tunafanya nae kazi alipofanya kazi ya ziada.

Baada ya mwezi kupita nilifunga safari tena kumfuata nikiwa na lengo la kutaka kujua kuhusu gari na nyumba ambavyo tulinunua pamoja na vyote vilibaki kwangu.

Alichonijibu nikwamba vyote ameniachia kwasababu alichonitendea anajua kiliniumiza sana. Nikwamwambia achukue gari mimi nimeshapona na sina amani kumiliki Mali ambazo tulichuma pamoja akakubali nikamuachia gari .

Utendaji wangu wa kazi ukawa mbovu sana maana kila nilipokumbuka sikuweza kufanya chochote. Nilikuwa nafanya kazi kwenye NGO ya wa Marekani, kufuatia kuwa na ufanisi mbovu kazini nilisitishiwa mkataba wa kazi.

Mapenzi yanauma sana jamani usiombe ukimpenda mtu halafu akakuzingua.
Hapo ndipo shida ikazidi kuwa kubwa maana sikuwa na cha kunikeep busy ikafika wakati nikawa napoteza mpaka fahamu.

Wazazi walipofahamu shida yangu wakanitumia mtu wa kuwa nae maana nilikuwa naishi peke yangu. Hali ile ilinichukua miezi saba ndipo niliporudi normal. Baadae Mungu akajalia nikapata kazi sehemu nyingine.

Maisha yakaendelea tatizo ikawa ni ile nyumba kila nikiona namkumbuka , nikaamua kuiuza na kujenga sehemu nyingine. Maisha yakaendelea nikamtoa moyoni kabisa nikawa namuona wa kawaida sana. Baada ya mwaka mmoja kupita akaanza kunitafuta nakuomba turudiane maana jamaa amemtosa na kuoa mwanamke mwngine.

Nimemkatalia mara kadhaa lkn bado ananing'ang'ania , kila nikitaka kumkubalia nakumbuka mateso niliyopata kwasababu yake.

Naomba ushauri wenu wakuu nipo njia panda sitaki kuumia tena.
 
Sasa Ndugu Majaliwa, unataka ushauri wa namna gani?? Kama mlifikia hatua ya kuchuma Mali pamoja, still akakuacha na kurudiana na mpenzi wake wa zamani, hakujali maumivu yako, wala ulivyojitoa kwake. Kweli Unaomba ushauri??? Au unataka tukutusi tuonekane hatuna busara?? Sikiliza moyo wako tu.
 
Moyo sukuma damuu.....

hakuna mapenzi hapo, ila mwamuzi wa mwisho ni wewe kwa sababu ulivyoandika kwa hisia inaonyesha dhahiri shairii bila kupepesa macho kuwa bado unampenda ila tu unachoogopa ni kuumizwa tena.

Lakini ki-uhalisia ni kuwa hana mapenzi ya dhati kama wewe unavyodhani na ipo siku utakuja kuumia zaidi ya ulivyo-umia mwanzo.

Mwisho, kuwa na subira na utampata mwenye mapenzi ya dhati na kukupenda kuliko huyo. Hata hapa JF wapo wadada wenye mapenzi ya dhati na ni wazuri sana kwa tabia na muonekano; hivyo usiwe na papara kwa sasa tafuta pesa muda ukifika Mungu atakupa chaguo bora na sahihi.
 
Haya mapenzi ni ya mwendo kasi! Hata miaka miwili kupita mmependana, mmejenga nyumba, mmenunua gari,

uhamisho wa ualimu umefanikiwa, umepoteza kazi, umepona mapenzi miezi baada ya mmiezi saba, umeuza nyumba na kujenga nyingine katika kipindi cha mwaka mmoja, mmpenzii katoswa anataka mmrudiane...

Duh! hapa kwa mtiririko wa matukio haya lazima uchanganyikiwe tu... Ila hii stori ...ngoja ninyamaze tu
 
Mtu aliyethubutu kukuacha mara ya kwanza hawezi shindwa kukuacha mara ya pili, sikiliza nafsi yako lakini uwe na taadhari kubwa.
Kabisa. Nami namshauri Majaliwa asikubali kuumizwa mara ya pili. Songa mbele, tafuta mpenzi wa dini yako mnayependana kwa dhati uendelee mbele
 
Mkubalie kwa moyo mmoja na muanze kuishi maisha mapya.Muonyeshe unampenda zaidi ya mwanzoni.Hakikisha unampenda na kumuonyesha kuwa unamjali sana na yeye ndo kila kitu katika maisha yako.Hata ikibidi pangeni tarehe ya harusi haraka iwezekanavyo.Wakati maandalizi ya ndoa yakiendelea,tafuta kipindi hayuko ameenda safari uza kila kitu na uhame kabisa eneo.Then badilisha number zote za simu na uanze maisha mapya.

Tit for Tat is a fair game.
 
Hakuna hata mmoja anayetarajia kuumizwa kwenye mapenzi,,.... Na kama yupo anayetarajia kuumizwa halafu akasubiria kuumizwa huyo taahira....
Sasa mwanzo hukutarajia kuumizwa lakini uliumizwa,.. Sasa iweje kwa sasa unavyotarajia kuumizwa?...
 
Hizi ndoa za dini tofauti Mara nyingi zinaleta maumivu baadae kama hamtakubaliana kuwa katika imani moja.

Nilisoma na watoto mama yao alikuwa mwislami wa sala tano baba mkristo, waliamua watoto watachagua dini wakiwa wakubwa. Baba aliwapeleka wale watoto katika shule ya Roma, watoto wale wote sasa wamekuwa wa kubwa wote wameolewa kanisani wanamwambia mama yao wamezoea sala za kikristo.
 
Back
Top Bottom