Sikuruhusiwa kukagua Daftari la Maslahi na Rasilimali la Paul Makonda

Kumbe manara alishawahi kula shavu kupitia Makonda na hasemi!!

Ila kwasababu GSM ni tajri yake kajikuta kasahau yote hayo na kumvaa mazima makonda

A time will come atakuja kumgeuka hata huyo GSM endapo atakuwa chini ya boss mwingine

Yuko wapi MO?
Na huyohuyo Makonda aliwahi kumweka lockup Haji Manara. Nikionacho sasa ni "mbwa kala mbwa!!"
 
17, Oktoba ,2019 niliandika Barua Sekretariati ya Maadili chini ya Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Marehemu Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela nikiomba kukagua Daftari la Maslahi , Rasilimali na madeni pamoja na matamko ya zawadi ya Makonda kama ambavyo kanuni za maadili ya viongozi wa umma za 1996 Na. 168 kifungu cha 6 na 7 kinavyoniruhusu mimi kama Raia kuomba kukagua Daftari hilo.

Barua yangu ilijibiwa tar 15 ,Novemba 2019 ,wakikataa kunipa ushirikiano kukagua Daftari la Makonda nilijua tuu ni kwasababu ya hofu iliyokuwepo na namna Makonda alivyokuwa anaogopwa . Ila suala la kukagua Daftari la mtumishi wa umma katika ofisi ya Sekretariati ya maadili haipaswi kuwa suala la kuomba au la siri, kiongozi akishakuwa mtumishi wa umma tuu kila kitu kuhusu utumishi wake kinapaswa kiwe wazi na umma ujue.

Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007 ,kifungu cha 27 kinasema " Ni kosa mtumishi wa umma kuwa na mali ambazo mwenye nazo hana maelezo ya kuridhisha kuhusu alivyozipata au kuwa na mali au pesa nyingi kuliko kipato chake halali " .

Kwangu mimi binafsi nilikuwa na wasiwasi na fedha na mali za Makonda, alikuwa na nafasi ya Mkuu wa mkoa tuu.Ila hakuna aliyewahi jua wapi kwingine alikuwa anapata fedha kwa namna alivyokuwa anagawa na kutumia.

Msukuma tar 7/Feb 2019 alitoa tuhuma Bungeni kwamba Makonda ana miliki mali nyingi tofauti na kipato chake akataja Gari Lexus ya Mil.400,magorofa Mwanza, ana miliki magari Toyota V 8 ,alikarabati ofisi yake kwa milion 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi (Chanzo Gazeti la mwananchi tar 8 Feb 2017,J.tano.).

Mh.Joseph Selasini Bungeni tar 11 , Feb 2017 kwamba Makonda ana miliki Apartment Viva Towers lenye thamani ya milion 600 (Chanzo Gazeti la Mwananchi February 11,2017).

Blog ya Sauti Kubwa,tar 30 Agosti 2018 aliandika na kuambatanisha na nyaraka mbalimbali za umiliki wa viwanja kwamba Makonda ana miliki Ardhi Dodoma eneo la Iyumbu new Town Center viwanja sita jumla mita za mraba 92,341 .

Pia Kugawa gawa fedha.

Tarehe 3/Juni/2019 alitoa fedha kwa wachezaji wa Simba mil.10 kwa Golikipa Manula,milion moja moja kwa kila mchezaji,mil. 2 kwa mchezaji wa kike,milion 3 kwa msemaji wa simba @hajismanara na septemba 9,2019 akatoa milion 10 kwa Juma Kaseja ,tar 5 Oktoba 2019 uwanja wa uhuru Dar alitoa Shiling Mil.100 kwa wajumbe wa shina wa CCM Mkoa wa Dar.(Chanzo Millard Ayo na EATV).

Tarehe 18/Septemba/2019 siku ya Jumaano kupitia Gazeti la Mwananchi iliandika kichwa cha habari "Makonda aeleza anakotoa fedha". Makonda kwa kauli yake ya mdomoni baada ya watu kuhoji wapi anapata fedha hizo zote za kugawa gawa ikiwa yeye ni mkuu wa mkoa tuu.

Katika taarifa hii alisema yeye anatumia watu wenye kipato kikubwa kuwaelezea shida na wao hutoa msaada akitolea mfano milion 10 alizompa Juma Kaseja , Makonda alijibu pia nchi hii ni tajiri na watu wake ni matajiri .Kama fedha alikuwa anapewa na wahisani au marafiki je sheria ya inasemaje mtumishi wa umma anapopokea zawadi ? .

Sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na. 13 ya 1995 kama ilivyofanyiwa marekebisho kuanzia kifungu cha 12(2 na 3) inaeleza utaratibu wa mtumishi wa umma kupokea zawadi ya zaidi ya thamani ya laki mbili, alipaswa kutoa taarifa kwa muajiri wake lakini pia taarifa ya matamko ya zawadi alizopewa yanapaswa kuwepo katika ofisi ya Kamishna Sekretariati ya Maadili.

Hivyo lengo langu nilitaka kujua idadi ya mali alizo nazo na nilitaka kujua kama hizo zawadi anazipokea kama huwa anaziwasilisha kwa Boss wake kwa mujibu wa sheria ya maadili na kanuni zake ,ili ndio nipate facts za kupeleka malalamiko yangu TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru Na.11 ya 2007 kifungu cha 39 kinachonipa mimi mamlaka kama mwananchi kutoa taarifa kwa TAKUKURU popote ninapoona kuna makisio ya uwepo wa Rushwa ,

Ili TAKUKURU ifanye kazi yake ya kuchunguza na kujiridhisha (Prove or disprove the allegations) ni kazi ya TAKUKURU kama ilivyoelezwa katika sheria ya TAKUKURU kifungu cha 7(e),(f),i,ii,iii, na cha 10 (1) a,b,c . Nadhani TAKUKURU bado wanasababu nyingi zaidi kufanya uchunguzi juu ya Allegations na nyingine nyingi dhidi ya Paul Makonda .

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa-ACT Wazalendo.

13/Machi/2022.

Kigoma-Ujiji.View attachment 2148675
Mkuu, Sekretarieti ya Maadili iliyvokataa kukupa habari hizi muhimu ilikupa sababu gani?

Hivi, Tanzania hakuna sheria za uhuru wa habari kutumia kulazimisha kupata habari kama hizi zinazohusu uongozi wa umma?

Katiba inasema wananchi wana hai ya kujua mambo muhimu yanayohusu kuendesha nchi yao. Maadili ya viongo,i pamoja na uadilifu wao ni vitu muhimu sana.
 
Kumbe manara alishawahi kula shavu kupitia Makonda na hasemi!!

Ila kwasababu GSM ni tajri yake kajikuta kasahau yote hayo na kumvaa mazima makonda

A time will come atakuja kumgeuka hata huyo GSM endapo atakuwa chini ya boss mwingine

Yuko wapi MO?
Hizo ndio tabia za chawa.....hawana marafiki wa kudumu ila maslahi tu.
 
Mwanaume unapata wapi muda wa kutaka kujua mali za mwanaume mwenzako?

Kweli wanaume wameisha....vijana tafuteni hela ndio muingie kwenye siasa siasa ukiwa na njaa utaishia kutumika tu.
Sijui hata muda gani, hiki kibwamdogo kishambashamba flani hivi.
Haya ukipewa uhakiki wa mali zake utafanyaje?
 
Ujinga tuu wa mtoa mada. Mnafanya cheap politics jikiteni kwenye ajenda zenu. Mbona hukuomba daftari ya JPM?
Mbona nyie chama chenu kilisajiliwa na mkafanya kampeni nchi nzima pesa mlitoa wapi wewe na mnafiki mwenzio kiongozi wa chama?
 
Nyie ACT ni watu wa ajabu sana na wanafiki. Wewe mbona haujahoji chama chenu kilisajiliwa na hapohapo kikaweka wagombea nchi nzima, zile hela mlitoa wapi? ZZK kapewa pesa na Kikwete aanzishe chama mbona sijakuona ukishupaa!
 
Mwanaume unapata wapi muda wa kutaka kujua mali za mwanaume mwenzako?

Kweli wanaume wameisha....vijana tafuteni hela ndio muingie kwenye siasa siasa ukiwa na njaa utaishia kutumika tu.
Mzigo ni wake itakuwa alimtumia mwenzake kwenye kuuset sasa akasahau kubadili umiliki akiwa kwenye madaraka sasa mwenzake anataka kumzima.
 
Yameisha rudini kwenye maada msiahamishe goli
Halafu familia ya Mo ikatoa tamko lao, mwamba akaonekana roporopo. Haji anamaisha ya kujipendekeza sana kwa mabosi ndiomana kumtetea inakuwa kazi sana, kauli zake zinapingana na kesho hauwezi jua atakuwa upande upi.
 
Kama kweli NCHI hii hakuna aliye juu ya SHERIA kwanini PAULO MAKONDA HACHUNGUZWI?
Na kwanini awe makonda peke yake mnayetaka achunguzwe mali zake!!?? anzeni na marais wastafu na watoto wao kama kweli nyie sio wanafiki na chuki binafsi.
 
17, Oktoba ,2019 niliandika Barua Sekretariati ya Maadili chini ya Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Marehemu Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela nikiomba kukagua Daftari la Maslahi , Rasilimali na madeni pamoja na matamko ya zawadi ya Makonda kama ambavyo kanuni za maadili ya viongozi wa umma za 1996 Na. 168 kifungu cha 6 na 7 kinavyoniruhusu mimi kama Raia kuomba kukagua Daftari hilo.

Barua yangu ilijibiwa tar 15 ,Novemba 2019 ,wakikataa kunipa ushirikiano kukagua Daftari la Makonda nilijua tuu ni kwasababu ya hofu iliyokuwepo na namna Makonda alivyokuwa anaogopwa . Ila suala la kukagua Daftari la mtumishi wa umma katika ofisi ya Sekretariati ya maadili haipaswi kuwa suala la kuomba au la siri, kiongozi akishakuwa mtumishi wa umma tuu kila kitu kuhusu utumishi wake kinapaswa kiwe wazi na umma ujue.

Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007 ,kifungu cha 27 kinasema " Ni kosa mtumishi wa umma kuwa na mali ambazo mwenye nazo hana maelezo ya kuridhisha kuhusu alivyozipata au kuwa na mali au pesa nyingi kuliko kipato chake halali " .

Kwangu mimi binafsi nilikuwa na wasiwasi na fedha na mali za Makonda, alikuwa na nafasi ya Mkuu wa mkoa tuu.Ila hakuna aliyewahi jua wapi kwingine alikuwa anapata fedha kwa namna alivyokuwa anagawa na kutumia.

Msukuma tar 7/Feb 2019 alitoa tuhuma Bungeni kwamba Makonda ana miliki mali nyingi tofauti na kipato chake akataja Gari Lexus ya Mil.400,magorofa Mwanza, ana miliki magari Toyota V 8 ,alikarabati ofisi yake kwa milion 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi (Chanzo Gazeti la mwananchi tar 8 Feb 2017,J.tano.).

Mh.Joseph Selasini Bungeni tar 11 , Feb 2017 kwamba Makonda ana miliki Apartment Viva Towers lenye thamani ya milion 600 (Chanzo Gazeti la Mwananchi February 11,2017).

Blog ya Sauti Kubwa,tar 30 Agosti 2018 aliandika na kuambatanisha na nyaraka mbalimbali za umiliki wa viwanja kwamba Makonda ana miliki Ardhi Dodoma eneo la Iyumbu new Town Center viwanja sita jumla mita za mraba 92,341 .

Pia Kugawa gawa fedha.

Tarehe 3/Juni/2019 alitoa fedha kwa wachezaji wa Simba mil.10 kwa Golikipa Manula,milion moja moja kwa kila mchezaji,mil. 2 kwa mchezaji wa kike,milion 3 kwa msemaji wa simba @hajismanara na septemba 9,2019 akatoa milion 10 kwa Juma Kaseja ,tar 5 Oktoba 2019 uwanja wa uhuru Dar alitoa Shiling Mil.100 kwa wajumbe wa shina wa CCM Mkoa wa Dar.(Chanzo Millard Ayo na EATV).

Tarehe 18/Septemba/2019 siku ya Jumaano kupitia Gazeti la Mwananchi iliandika kichwa cha habari "Makonda aeleza anakotoa fedha". Makonda kwa kauli yake ya mdomoni baada ya watu kuhoji wapi anapata fedha hizo zote za kugawa gawa ikiwa yeye ni mkuu wa mkoa tuu.

Katika taarifa hii alisema yeye anatumia watu wenye kipato kikubwa kuwaelezea shida na wao hutoa msaada akitolea mfano milion 10 alizompa Juma Kaseja , Makonda alijibu pia nchi hii ni tajiri na watu wake ni matajiri .Kama fedha alikuwa anapewa na wahisani au marafiki je sheria ya inasemaje mtumishi wa umma anapopokea zawadi ? .

Sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na. 13 ya 1995 kama ilivyofanyiwa marekebisho kuanzia kifungu cha 12(2 na 3) inaeleza utaratibu wa mtumishi wa umma kupokea zawadi ya zaidi ya thamani ya laki mbili, alipaswa kutoa taarifa kwa muajiri wake lakini pia taarifa ya matamko ya zawadi alizopewa yanapaswa kuwepo katika ofisi ya Kamishna Sekretariati ya Maadili.

Hivyo lengo langu nilitaka kujua idadi ya mali alizo nazo na nilitaka kujua kama hizo zawadi anazipokea kama huwa anaziwasilisha kwa Boss wake kwa mujibu wa sheria ya maadili na kanuni zake ,ili ndio nipate facts za kupeleka malalamiko yangu TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru Na.11 ya 2007 kifungu cha 39 kinachonipa mimi mamlaka kama mwananchi kutoa taarifa kwa TAKUKURU popote ninapoona kuna makisio ya uwepo wa Rushwa ,

Ili TAKUKURU ifanye kazi yake ya kuchunguza na kujiridhisha (Prove or disprove the allegations) ni kazi ya TAKUKURU kama ilivyoelezwa katika sheria ya TAKUKURU kifungu cha 7(e),(f),i,ii,iii, na cha 10 (1) a,b,c . Nadhani TAKUKURU bado wanasababu nyingi zaidi kufanya uchunguzi juu ya Allegations na nyingine nyingi dhidi ya Paul Makonda .

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa-ACT Wazalendo.

13/Machi/2022.

Kigoma-Ujiji.View attachment 2148675
Usicheze na Makondakta. Mwenzako kiwanda cha magodoro kimeingia moto huko.
 
Kama haya yote yanayosemwa ni kweli basi hii nchi bado tuna safari ndefu sana kufikia kwenye haki ya kweli !! Je hii ndio sababu watu wengi wanakimbilia kwenye siasa ??! Au ?? Bandugu twendeni polepole hapa duniani tunapita tu !! Hata ukijilimbikizia Mali kiasi gani ujue utaziacha tu tena utaishi bila kuwa na peace of mind mpaka unaondoka !! Ukiishi kwa kutenda haki utapata peace of mind kinyume chake utapata tabu sana Ndugu !!
Umeandika maneno ya maana sana lakini ni wachace sana watakaokuelewa.

Maadili yameporomoka Tanzania yetu kiasi mema yanakuwa maovu na maovu yanakuwa mema.
 
Back
Top Bottom