Sikuruhusiwa kukagua Daftari la Maslahi na Rasilimali la Paul Makonda

17, Oktoba ,2019 niliandika Barua Sekretariati ya Maadili chini ya Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Marehemu Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela nikiomba kukagua Daftari la Maslahi , Rasilimali na madeni pamoja na matamko ya zawadi ya Makonda kama ambavyo kanuni za maadili ya viongozi wa umma za 1996 Na. 168 kifungu cha 6 na 7 kinavyoniruhusu mimi kama Raia kuomba kukagua Daftari hilo.

Barua yangu ilijibiwa tar 15 ,Novemba 2019 ,wakikataa kunipa ushirikiano kukagua Daftari la Makonda nilijua tuu ni kwasababu ya hofu iliyokuwepo na namna Makonda alivyokuwa anaogopwa . Ila suala la kukagua Daftari la mtumishi wa umma katika ofisi ya Sekretariati ya maadili haipaswi kuwa suala la kuomba au la siri, kiongozi akishakuwa mtumishi wa umma tuu kila kitu kuhusu utumishi wake kinapaswa kiwe wazi na umma ujue.

Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007 ,kifungu cha 27 kinasema " Ni kosa mtumishi wa umma kuwa na mali ambazo mwenye nazo hana maelezo ya kuridhisha kuhusu alivyozipata au kuwa na mali au pesa nyingi kuliko kipato chake halali " .

Kwangu mimi binafsi nilikuwa na wasiwasi na fedha na mali za Makonda, alikuwa na nafasi ya Mkuu wa mkoa tuu.Ila hakuna aliyewahi jua wapi kwingine alikuwa anapata fedha kwa namna alivyokuwa anagawa na kutumia.

Msukuma tar 7/Feb 2019 alitoa tuhuma Bungeni kwamba Makonda ana miliki mali nyingi tofauti na kipato chake akataja Gari Lexus ya Mil.400,magorofa Mwanza, ana miliki magari Toyota V 8 ,alikarabati ofisi yake kwa milion 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi (Chanzo Gazeti la mwananchi tar 8 Feb 2017,J.tano.).

Mh.Joseph Selasini Bungeni tar 11 , Feb 2017 kwamba Makonda ana miliki Apartment Viva Towers lenye thamani ya milion 600 (Chanzo Gazeti la Mwananchi February 11,2017).

Blog ya Sauti Kubwa,tar 30 Agosti 2018 aliandika na kuambatanisha na nyaraka mbalimbali za umiliki wa viwanja kwamba Makonda ana miliki Ardhi Dodoma eneo la Iyumbu new Town Center viwanja sita jumla mita za mraba 92,341 .

Pia Kugawa gawa fedha.

Tarehe 3/Juni/2019 alitoa fedha kwa wachezaji wa Simba mil.10 kwa Golikipa Manula,milion moja moja kwa kila mchezaji,mil. 2 kwa mchezaji wa kike,milion 3 kwa msemaji wa simba @hajismanara na septemba 9,2019 akatoa milion 10 kwa Juma Kaseja ,tar 5 Oktoba 2019 uwanja wa uhuru Dar alitoa Shiling Mil.100 kwa wajumbe wa shina wa CCM Mkoa wa Dar.(Chanzo Millard Ayo na EATV).

Tarehe 18/Septemba/2019 siku ya Jumaano kupitia Gazeti la Mwananchi iliandika kichwa cha habari "Makonda aeleza anakotoa fedha". Makonda kwa kauli yake ya mdomoni baada ya watu kuhoji wapi anapata fedha hizo zote za kugawa gawa ikiwa yeye ni mkuu wa mkoa tuu.

Katika taarifa hii alisema yeye anatumia watu wenye kipato kikubwa kuwaelezea shida na wao hutoa msaada akitolea mfano milion 10 alizompa Juma Kaseja , Makonda alijibu pia nchi hii ni tajiri na watu wake ni matajiri .Kama fedha alikuwa anapewa na wahisani au marafiki je sheria ya inasemaje mtumishi wa umma anapopokea zawadi ? .

Sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na. 13 ya 1995 kama ilivyofanyiwa marekebisho kuanzia kifungu cha 12(2 na 3) inaeleza utaratibu wa mtumishi wa umma kupokea zawadi ya zaidi ya thamani ya laki mbili, alipaswa kutoa taarifa kwa muajiri wake lakini pia taarifa ya matamko ya zawadi alizopewa yanapaswa kuwepo katika ofisi ya Kamishna Sekretariati ya Maadili.

Hivyo lengo langu nilitaka kujua idadi ya mali alizo nazo na nilitaka kujua kama hizo zawadi anazipokea kama huwa anaziwasilisha kwa Boss wake kwa mujibu wa sheria ya maadili na kanuni zake ,ili ndio nipate facts za kupeleka malalamiko yangu TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru Na.11 ya 2007 kifungu cha 39 kinachonipa mimi mamlaka kama mwananchi kutoa taarifa kwa TAKUKURU popote ninapoona kuna makisio ya uwepo wa Rushwa ,

Ili TAKUKURU ifanye kazi yake ya kuchunguza na kujiridhisha (Prove or disprove the allegations) ni kazi ya TAKUKURU kama ilivyoelezwa katika sheria ya TAKUKURU kifungu cha 7(e),(f),i,ii,iii, na cha 10 (1) a,b,c . Nadhani TAKUKURU bado wanasababu nyingi zaidi kufanya uchunguzi juu ya Allegations na nyingine nyingi dhidi ya Paul Makonda .

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa-ACT Wazalendo.

13/Machi/2022.

Kigoma-Ujiji.View attachment 2148675
Wanasiasa wengi wana mali ambazo hawawezi zitolea hesabu zake. Hata hawa kina Zitto, Faru John na magenge yao wakikwapuliwa mataulo yao ni aibu tupu. Siku hizi mpaka watendaji wa vijiji mafisadi ndo itakuwa hawa wenye nyazifa. Corrupted system, huzaa corrupted people's.
 
17, Oktoba ,2019 niliandika Barua Sekretariati ya Maadili chini ya Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Marehemu Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela nikiomba kukagua Daftari la Maslahi , Rasilimali na madeni pamoja na matamko ya zawadi ya Makonda

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa-ACT Wazalendo.

13/Machi/2022.

Kigoma-Ujiji.View attachment 2148675
Mkuu mdogo wangu Abdul Nondo, kwanza habari za siku?.
Pili bila kuingilia, your right to information, taarifa ya mali za viongozi, inalindwa na haki za the right to privacy, hivyo ili mwananchi uruhusiwe kukagua mali za kiongozi yoyote, maombi yako yaliza yaambatane na the the motive behind ya wewe kuzitaka taarifa confidential za mtu.
Ili kuwa fare kwa Makonda, you should have shown unazitafuta taarifa hizo in good faith just for the quest for info, tena ungepaswa, kuonyesha charity begins at home, kwa kukagua kwanza mali za viongozi wako wa chama, kisha uende kwa viongozi wa kitaifa, national level, ndipo uje regional level.

Kitendo cha kutaka kumchunguza Makonda tuu, sio kumtendea haki.
Sasa kwa kukusaidia wewe na wengine ambao hamjui source ya utajiri wa Makonda, karibu mitaa hii HAPA!.

Kama hoja yangu hiyo ya source ya utajiri wa Makonda ni bonafide genuine, nakushauri, achana na Makonda na yasiyokuhusu, fuatilia viongozi wako.
Ni ushauri tuu!.
P
 
Kama kweli NCHI hii hakuna aliye juu ya SHERIA kwanini PAULO MAKONDA HACHUNGUZWI?
Inategemea hivi, Je anayoyajua Unayajua? Je ataikayechunguza yuko tayari kufukua makaburi? Unajuaje walipoonyeshwa makaburi ya kufukua walikimbia?
 
Mashabiki wa mpira mna akili za Ndezi, yaani hapa tayari Usimba na Uyanga umeanza. Nani hajui Manara aliwekwa ndani Kwa amri ya Makonda akiwa DC Kinondoni?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
Mkuu, umejua ana umri gani huyu kashimbe inawezekana wakati hili la Manara kuswekwa ndani kwa amri ya Makonda, huyu kashimbe alikua hajaanza kufuatilia haya mambo ya nchi na hakuweza kulijua hili. Ingawa hakupaswa kukanusha jambo asilolijua. Mtu huwezi kujua kila kitu.
 
Ili TAKUKURU ifanye kazi yake ya kuchunguza na kujiridhisha (Prove or disprove the allegations) ni kazi ya TAKUKURU kama ilivyoelezwa katika sheria ya TAKUKURU kifungu cha 7(e),(f),i,ii,iii, na cha 10 (1) a,b,c . Nadhani TAKUKURU bado wanasababu nyingi zaidi kufanya uchunguzi juu ya Allegations na nyingine nyingi dhidi ya Paul Makonda .
Kijana, unao uwezo mzuri wa kuelezea jambo kwa mpangilio na kueleweka vizuri; kama alivyo Kiongozi Mkuu wa chama chako. Hili naliachia hapa.
Uliyoyaeleza hapo juu ya Makonda, siyo yeye tu, uozo umeenea karibu kila sehemu ndani ya serikali. Sheria zipo, lakini utekelezaji wake ni mbovu.
Ungepeleka malalamiko yako kuchunguza akina Sumaye na Lowassa wakati ule, pengine ungefanikiwa zaidi kuliko ulivyofanya kuhusu Makonda
Hadi hapo tutakapokuwa na utaratibu wa kuruhusu sheria zifanye kazi kama ilivyonuiwa, hali ya nchi yetu bado itaendelea kuwa siyo nzuri hata kama viongozi wanabadilishwa toka mmoja anayebweka kila mahali huku vitendo viovu vikishamiri; hadi mwingine anayetoa maneno matamu matamu ya kuwaweka usingizi wananchi, huku uozo huo huo ukiendelea ndani ya serikali.

Wewe umechukua upande wa mali za Makonda. Itapendeza sana pakijitokeza mwingine atupe habari za Makonda kuhusu alipokuwa siku Lissu anapigwa risasi Dodoma; na pia kuhusu mkasa wa kupotea kwa Ben Saanane. Haya yote yanahitaji kuelezwa vizuri watu wayajue.
 
Mawazo ya ajabu sana juu ya viongozi wezi na majambazi wa mali za watu. Kwa mawazo haya, nchi hii haitaendelea.
Mwanaume unapata wapi muda wa kutaka kujua mali za mwanaume mwenzako?

Kweli wanaume wameisha....vijana tafuteni hela ndio muingie kwenye siasa siasa ukiwa na njaa utaishia kutumika tu.
 
17, Oktoba ,2019 niliandika Barua Sekretariati ya Maadili chini ya Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Marehemu Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela nikiomba kukagua Daftari la Maslahi , Rasilimali na madeni pamoja na matamko ya zawadi ya Makonda kama ambavyo kanuni za maadili ya viongozi wa umma za 1996 Na. 168 kifungu cha 6 na 7 kinavyoniruhusu mimi kama Raia kuomba kukagua Daftari hilo.

Barua yangu ilijibiwa tar 15 ,Novemba 2019 ,wakikataa kunipa ushirikiano kukagua Daftari la Makonda nilijua tuu ni kwasababu ya hofu iliyokuwepo na namna Makonda alivyokuwa anaogopwa . Ila suala la kukagua Daftari la mtumishi wa umma katika ofisi ya Sekretariati ya maadili haipaswi kuwa suala la kuomba au la siri, kiongozi akishakuwa mtumishi wa umma tuu kila kitu kuhusu utumishi wake kinapaswa kiwe wazi na umma ujue.

Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007 ,kifungu cha 27 kinasema " Ni kosa mtumishi wa umma kuwa na mali ambazo mwenye nazo hana maelezo ya kuridhisha kuhusu alivyozipata au kuwa na mali au pesa nyingi kuliko kipato chake halali " .

Kwangu mimi binafsi nilikuwa na wasiwasi na fedha na mali za Makonda, alikuwa na nafasi ya Mkuu wa mkoa tuu.Ila hakuna aliyewahi jua wapi kwingine alikuwa anapata fedha kwa namna alivyokuwa anagawa na kutumia.

Msukuma tar 7/Feb 2019 alitoa tuhuma Bungeni kwamba Makonda ana miliki mali nyingi tofauti na kipato chake akataja Gari Lexus ya Mil.400,magorofa Mwanza, ana miliki magari Toyota V 8 ,alikarabati ofisi yake kwa milion 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi (Chanzo Gazeti la mwananchi tar 8 Feb 2017,J.tano.).

Mh.Joseph Selasini Bungeni tar 11 , Feb 2017 kwamba Makonda ana miliki Apartment Viva Towers lenye thamani ya milion 600 (Chanzo Gazeti la Mwananchi February 11,2017).

Blog ya Sauti Kubwa,tar 30 Agosti 2018 aliandika na kuambatanisha na nyaraka mbalimbali za umiliki wa viwanja kwamba Makonda ana miliki Ardhi Dodoma eneo la Iyumbu new Town Center viwanja sita jumla mita za mraba 92,341 .

Pia Kugawa gawa fedha.

Tarehe 3/Juni/2019 alitoa fedha kwa wachezaji wa Simba mil.10 kwa Golikipa Manula,milion moja moja kwa kila mchezaji,mil. 2 kwa mchezaji wa kike,milion 3 kwa msemaji wa simba @hajismanara na septemba 9,2019 akatoa milion 10 kwa Juma Kaseja ,tar 5 Oktoba 2019 uwanja wa uhuru Dar alitoa Shiling Mil.100 kwa wajumbe wa shina wa CCM Mkoa wa Dar.(Chanzo Millard Ayo na EATV).

Tarehe 18/Septemba/2019 siku ya Jumaano kupitia Gazeti la Mwananchi iliandika kichwa cha habari "Makonda aeleza anakotoa fedha". Makonda kwa kauli yake ya mdomoni baada ya watu kuhoji wapi anapata fedha hizo zote za kugawa gawa ikiwa yeye ni mkuu wa mkoa tuu.

Katika taarifa hii alisema yeye anatumia watu wenye kipato kikubwa kuwaelezea shida na wao hutoa msaada akitolea mfano milion 10 alizompa Juma Kaseja , Makonda alijibu pia nchi hii ni tajiri na watu wake ni matajiri .Kama fedha alikuwa anapewa na wahisani au marafiki je sheria ya inasemaje mtumishi wa umma anapopokea zawadi ? .

Sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na. 13 ya 1995 kama ilivyofanyiwa marekebisho kuanzia kifungu cha 12(2 na 3) inaeleza utaratibu wa mtumishi wa umma kupokea zawadi ya zaidi ya thamani ya laki mbili, alipaswa kutoa taarifa kwa muajiri wake lakini pia taarifa ya matamko ya zawadi alizopewa yanapaswa kuwepo katika ofisi ya Kamishna Sekretariati ya Maadili.

Hivyo lengo langu nilitaka kujua idadi ya mali alizo nazo na nilitaka kujua kama hizo zawadi anazipokea kama huwa anaziwasilisha kwa Boss wake kwa mujibu wa sheria ya maadili na kanuni zake ,ili ndio nipate facts za kupeleka malalamiko yangu TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru Na.11 ya 2007 kifungu cha 39 kinachonipa mimi mamlaka kama mwananchi kutoa taarifa kwa TAKUKURU popote ninapoona kuna makisio ya uwepo wa Rushwa ,

Ili TAKUKURU ifanye kazi yake ya kuchunguza na kujiridhisha (Prove or disprove the allegations) ni kazi ya TAKUKURU kama ilivyoelezwa katika sheria ya TAKUKURU kifungu cha 7(e),(f),i,ii,iii, na cha 10 (1) a,b,c . Nadhani TAKUKURU bado wanasababu nyingi zaidi kufanya uchunguzi juu ya Allegations na nyingine nyingi dhidi ya Paul Makonda .

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa-ACT Wazalendo.

13/Machi/2022.

Kigoma-Ujiji.View attachment 2148675

Bahati mbaya huyu Nsekela alishafariki,tunge muuliza hapa alimaanisha nini? Kuna kitu kimoja cha mhimu watu wenye madaraka huwa wanasahau kuwa wao pia ni "WANADAMU". Ukiwa ni mwanadamu ukipewa dhamana,Hasa pale kwamba hicho unachokifanya alikuwa anafanya mwenzako muda ukapita akaondoka, jua na wewe muda utafika utaondoka. so muda ndiyo huratibu maisha yako.unaweza kujisahaulisha tuu,ila sheria ya asili inabaki pale pale.

Kuna mtu namfahamu sasa kwa jinsi alivyoishi kwa kujishusha hata pale alipokuwa na nyazifa kubwa huko kazini.baada ya kustaafu anaishi maisha mazuri zaidi mara mbili naweza kusema zaidi ya alipokuwa kazini.

Ukiwa kwenye nafasi ya umma itumikie kwa hofu.hujui kabisa kesho yako,unaweza sema mbona nimeshawekeza vya kutosha nina uhakika wa maisha.I tell you,hutaamini jinsi maisha yanvyogeuka.

Namfahamu DED mstaafu ambaye nilimkuta anaendesha baskeli amebeba tenga la machungwa anapeleka sokoni kutafuta mia mia.
Kumbuka siku zote wewe ni "MWANADAMU"
 
Back
Top Bottom