tuacheni chuki na ukasuku. Hivi ukiambiwaa ueleze ufisadi wa lowasa, utauelezea upi? Na kwa ushahidi upi? Avoid dogmatic..
Nyota yake inawaka kwa sasa
Hamna kitu pale Lowassa mweupe tu hivi uchaguzi wa Arusha bado haujawapa somo tu kuhusu Lowassa ama kweli mna roho za paka.
RAIS Jakaya Kikwete amesema hakumteua Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu kwa sababu ya urafiki wao bali kwa sababu ya ufanisi wake.
Kikwete ameyasema hayo kupitia kitabu chake cha JK: A Political Biography, kitabu kinachoeleza kuhusu maisha yake ambacho sasa kinapatikana hapa nchini.
Kikwete ameelezwa kutoa maelezo haya mwaka mmoja baada ya tukio la kujiuzulu kwa Lowassa kufuatia kashfa ya Richmond ambayo ililazimu baraza lote la mawaziri kuvunjwa.
"Sikiliza. Ni kweli kwamba Lowassa ni rafiki yangu na nimemfahamu kwa muda mrefu. Lakini pia ninawafahamu watu wengi zaidi kwa muda mrefu, wanasiasa na wasiokuwa wanasiasa na sikuwachagua kuwa Waziri Mkuu.
"Nilikuwa natafuta mtu ambaye atafanya kazi kwa ufanisi na kutekeleza sera zangu. Lowassa alijitokeza vizuri kama mtu anayeweza kutokana na uzoefu wake," kitabu hicho kinamnukuu Kikwete.
Hii ni mara ya kwanza ambapo Kikwete anaeleza wazi wazi mahusiano yake pamoja na tathmini ya utendaji wa Lowassa, tangu kuibuka kwa kashfa ya Richmond.
Sentensi moja katika maelezo ya Kikwete inaonyesha mtazamo wake kwa waziri mkuu huyo aliyejiuzulu; "Lowassa alikuwa mmoja wa mawaziri wakuu wenye ufanisi mkubwa kabisa nchini."
Tafsiri ya maelezo haya ya Kikwete inaonyesha kwamba mwaka mmoja baada ya kashfa ya Richmond, rais bado alikuwa na imani na Lowassa.
Wakati Kikwete alipochaguliwa kuwa rais mwaka 2005, majina mengi yalitajwa kuchukua nafasi ya uwaziri mkuu ingawa la Lowassa lilitajwa zaidi kutokana na ukaribu waliokuwa nao viongozi hao.
Lowassa pia hakuchukua fomu kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, jambo lililotajwa kama kuonyesha azma yake ya kumuunga mkono mgombea huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa, walidai kwamba uamuzi wa Kikwete kumteua Lowassa ungekuwa na athari kubwa kwake kwa vile ukaribu wake ungeweza kuingia kwenye kazi.
Mara baada ya uteuzi huo, ndipo ilipoibuka dhana ya ‘serikali ya kishkaji' kutokana na baadhi ya watu waliotajwa kuwa maswahiba wa Kikwete, akiwamo Lowassa, kupata nafasi katika baraza lake la kwanza la mawaziri.
Kikwete na Lowassa walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1974 wakiwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wote wakiwa wanachama wa Umoja wa Vijana wa chama cha TANU ingawa Jakaya alikuwa katika mwaka wake wa mwisho wa masomo huku Edward akiwa mwaka wa kwanza.
Wote kwa pamoja walifanya maamuzi ya kujiunga na ajira katika chama cha TANU (sasa CCM) wakati huo mara baada ya kumaliza masomo yao, na wote walichukua fomu kuwania urais kupitia CCM mwaka 1995 wakiwa na umri chini ya miaka 50.
Source: Raia Mwema
Lowasa ni mwizi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mimi huwa nawashangaa sana watu wanaosema EL ana hela sana, hela gani hizo zenye masharti ya kutolewa kanisani na misikitini?Kwenye demokrasia za kibepari ili upate uongozi wa juu kabisa wa nchi lazima uwe na kimoja kati ya vitu vitatu ambavyo ni PRESTIGE, POWER AND MONEY.
Kitu kinachomfanya Edward Lowassa kuwa UNIQUE kwenye siasa za Tanzania ni kuwa na vyote vitatu badala ya kimoja au viwili.
Watch out Lowassa political space.
Mimi huwa nawashangaa sana watu wanaosema EL ana hela sana, hela gani hizo zenye masharti ya kutolewa kanisani na misikitini?
Ni wapi Lowassa alipojenga hata nyumba ya yatima tujue ana Upendo kwa jamii?
Hizo hela za Lowassa wenzetu mnaziona wapi?...wasio waumini wanazifaidi wapi? Amejenga shule gani?, Hopitali gani? Bomba gani la maji au Kisima, Barabara gani?
Kama mtu anasema Lowassa ana hela basi ujue huyo yuko mfukoni mwake, aidha ni mwandishi wa habari au tarishi wake. Mtu wa kawaida hutakaa uone hela ya Lowassa, maana anawekeza pale atakapovuna!
Mtu ananiambia Lowassa ana POWER, power gani? Ile ya kutumia Wasomali kupiga watu?
Au ile ya kukusanya Wamaasai pale Teknico college ili wafanye ukabila?
Power gani, si mseme??
-Angekuwa na Power si angemshindisha Ubunge Mchumba wake Batilda pale Arusha Mjini 2010?
-Si angemshindisha Ubunge mkwewe SIOI SUMARI kule kwao Meru?
-Si angewashindisha udiwani wagombea wao wote hapa Arusha?
POWER ya LOWASSA mnayoiongelea ni ya aina gani?...is it some kinda supernatural or witchcraft oriented?
Mtu angeniambia LEMA ana Power ningekaa kumsikiliza.
Naomba mwenye kujua hata hiyo Prestige mnayoisema huwa anaidisplay akiwa wapi, wakati takwimu za wafuatiliaji wa Bunge zinaonyesha kuwa ni wa tatu toka mkiani kwa Ububu katika Bunge!
Kukaa mfukoni mwa mtu inataka mtu mwenye roho saba kama za Pakashume.
Mkuu Rock City Angelikuwa Mh Lowasa Kiongozi Mzuri kwanini alijiuzulu? Kwa kashfa za Serikali? angalisafisha machafu waliyokuwa wanafanya hao Mafisadi. Mh Lowasa na Marehemu Aliyekuwa Waziri Mkuu ndugu Edward Moringe Sokoine nani zaidi?